Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/94 uku. 11
  • Wahubiri wa Ufalme Wapendwa:

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wahubiri wa Ufalme Wapendwa:
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1994
Huduma Yetu ya Ufalme—1994
km 10/94 uku. 11

Wahubiri wa Ufalme Wapendwa:

Ramani inayoandamana yaonyesha mahali pa mradi wa majengo yote yaliyo kwenye jengo tata jipya la ofisi ya tawi. Bila shaka unatambua kwa urahisi Jumba la Ufalme, Bohari, na Banda la Motokaa. Jengo la Makao larejezea nyumba za makao ya Betheli. Utumishi wa Makao utatia ndani jikoni, chumba cha kulia, mahali pa kusafishia nguo, na mahali pa kutunzia wagonjwa. Jengo la Usimamizi ni mahali ambapo ofisi za utafsiri na ofisi nyingine zitakuwa. Jumba la kwanza la kudumu litakalojengwa litakuwa Jumba la Ufalme nalo latazamiwa kuanzwa kufikia wakati wa mkusanyiko. Mradi wote mzima watazamiwa kukamilika kwa muda wa miaka miwili.

Kwa sababu ya jitihada zenu zenye bidii shambani na baraka za Yehova tumeona idadi ya wahubiri wa Ufalme ikiongezeka kutoka 5,493 katika Afrika mashariki mnamo 1979 upanuzi wa sasa wa Betheli ulipokamilishwa kufikia zaidi ya 22,000 leo. Kwa kweli hili laonyesha uhitaji wa majengo makubwa zaidi.

Inatazamiwa kwamba kazi ya ujenzi itakamilishwa na wajitoleaji wenyeji wakisaidiwa na Wajitoleaji wa Kimataifa wa Kazi ya Ujenzi. Kwa wakati ufaao makutaniko yatapokea habari zaidi za jinsi programu hii ya wajitoleaji inavyofanya kazi. Pia, kwa kufuata violezo vilivyowekwa nyakati za Biblia na sehemu nyingine za ulimwengu, michango ya kujitolea itasaidia kutegemeza kifedha mradi huu. (Ona Kutoka 36:4-7.) Michango kama hiyo ya watu mmoja-mmoja au ya kutaniko yaweza kupelekwa kwa ofisi ya tawi na yapaswa kutiwa alama “Michango ya Ujenzi wa Betheli.”

Twaomba baraka za Yehova ziwe kwa mradi huu kwa utukuzo na heshima ya jina Lake lenye thamani.

Ndugu zenu,

Ofisi ya Tawi ya Nairobi

[Picha katika ukurasa wa 11]

MAKAO HOSTEL

UTUMISHI HOSTEL WA MAKAO SERVICES

SEBULE LOBBY

JENGO LA ADMINISTRATION

USIMAMIZI BUILDING

BOHARI STORAGE

JUMBA LA KINGDOM UFALME HALL

BANDA LA MOTOKAA GARAGE

MAKAO YA CONSTRUCTION WAJENZI HOSTEL

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki