Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/94 kur. 3-4
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1994
Huduma Yetu ya Ufalme—1994
km 12/94 kur. 3-4

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Septemba 5 hadi Desemba 19, 1994. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila moja ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Kwa ujanja Shetani anashawishi watu watosheleze tamaa zao za kawaida kwa njia mbaya. [uw-SW uku. 65 fu. 9]

2. Sheoli, Hadesi, na Gehena ni kaburi la wanadamu kwa ujumla. [uw-SW uku. 72 fu. 6]

3. Kwa kuwa utimizo wa Zaburi 110:1, 2 huendelea hadi siku za mwisho za ulimwengu huu, mistari hii yatusaidia tuelewe kwamba unabii wa Yesu juu ya umalizio wa mfumo wa mambo haukuwa utimizwe kwa uharibifu wa Yerusalemu katika 70 W.K. tu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 2/15 uku. 12 fu. 17.]

4. Sanhedrini ilikuwa ile Mahakama Kuu ya Kiroma yenye washiriki 71 iliyokutana Yerusalemu. [gt-SW sura. 119]

5. Wale “watawala wa ulimwengu” wanaorejezewa kwenye Waefeso 6:12 (NW), ni viongozi wa kisiasa waliotengwa na upendeleo wa Mungu. [uw-SW uku. 63 fu. 4]

6. Mamilioni watakaofufuliwa kutoka kwa wafu watahukumiwa kulingana na matendo yao waliyofanya kabla ya kufufuliwa kwao. [uw-SW uku. 75 fu. 12]

7. Zaidi ya kutumika akiwa Mpatanishi wa agano jipya, Yesu mwenyewe alifanya agano pamoja na mitume wake waaminifu-washikamanifu kwa ajili ya Ufalme. [gt-SW sura 115]

8. Ubatizo wenyewe, ni uhakikisho wa wokovu. [uw-SW uku. 100 fu. 12]

9. Yesu aliposali: “Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki,” alikuwa akiomba kuepuka kufa. (Luka 22:42) [gt-SW sura 117]

10. Kulingana na Zaburi 58:4, fira hawezi kusikia. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona it-1 uku. 485.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Kujua kwamba Yehova hulisha ndege na huvika kwa urembo maua kwapaswa kupunguzia watumishi wa kibinadamu mahangaiko gani? [uw-SW uku. 87 fu. 3]

12. Kama inavyofafanuliwa kwenye Zaburi 58:3-5, ni katika njia gani waovu ni kama nyoka? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 10/15 uku. 30.]

13. Kupatana na Waefeso 5:3-5, ni kwa msingi gani Mkristo mwenye utambuzi anaweza kukataa muziki fulani ambao huenda ukawa na sauti tamu, mwendo wenye kuvutia, au mdundo wenye kurudiwa-rudiwa? [uw-SW uku. 67 fu. 12]

14. Biblia humaanisha nini kwenye Ufunuo 20:14, ambapo husema kwamba Hadesi “ikatupwa katika lile ziwa la moto”? [uw-SW uku. 75 fu. 12]

15. Kondoo na mbuzi wanahukumiwa kwa msingi gani katika mfano wa Yesu kwenye Mathayo 25:31-46? [gt-SW sura 111 fu. 43]

16. Ikiwa Nisani 11, 33 W.K., iliisha kwenye mshuko-jua Jumanne, Nisani 14 ilianza na kwisha lini? [gt-SW sura 112]

17. Kubatizwa kwa jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu kwamaanisha nini? [uw-SW uku. 98 fu. 9]

18. Ni katika njia gani wanafunzi wa Yesu wangefanya kazi kubwa kuliko ile aliyofanya, kama alivyotaarifu kwenye Yohana 14:12? [gt-SW sura 116 fu. 6]

19. Ni nini “mahali pa siri pake Aliye juu” panaporejezewa kwenye Zaburi 91:1, nasi lazima tufanye nini ili tukae humo? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 12/15 uku. 12; w86-SW 12/15 uku. 29.]

20. Kwa nini Yesu alisema kwenye Yohana 16:33 kwamba alikuwa ameushinda ulimwengu? [gt-SW sura 116 fu. 37]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Kama kisa cha Ayubu kinavyoonyesha, Shetani abisha kwamba tunapendezwa hasa na mali za _________________________ , raha yetu wenyewe na hali njema ya kibinafsi, na kwamba nia yetu ya kumtumikia Mungu ni ya _________________________ . [uw-SW uku. 93 fu. 13]

22. Yesu alipohukumiwa isivyo haki, _________________________ alikuwa gavana wa Yudea, na _________________________ alikuwa mtawala wa Galilaya. [gt-SW sura 121, 122]

23. Kupatana na yale ambayo _________________________ alieleza kwenye Luka 3:16, katika Pentekoste 33 W.K., wanafunzi wa Yesu kwanza walipata ubatizo kwa _________________________ ; katika 70 W.K., Wayahudi wasiotubu walibatizwa kwa _________________________ . [uw-SW uku. 96 fu. 4]

24. Ubatizo wa Yesu katika _________________________ ulianza katika 29 W.K. lakini haukumalizika mpaka alipo_________________________ hakika na _________________________ . [uw-SW uku. 97 fu. 6]

25. Vikundi kwa ajili ya agano jipya ni _________________________ na _________________________ . [gt-SW sura 114]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Kwa wazi, “miungu” wanaorejezewa katika Zaburi 82 ni (Shetani na mashetani; miungu ya kipagani ya mataifa; wanaume waliokuwa mahakimu wa Israeli). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 12/15 uku. 28.]

27. Kusudi kuu la kuja kwa Yesu ulimwenguni lilikuwa (kuokoa wanadamu; kufanya wanafunzi; kuitolea kweli ushahidi). [gt-SW sura 122]

28. Tukipatwa na taabu iliyo kubwa ya kimwili au kupoteza vitu vya kimwili, Ibilisi angetaka kuona (tukimheshimu Yehova na kumthibitisha Ibilisi kuwa mwongo; tukimlaumu Mungu na kuwa wasio waaminifu-washikamanifu; tukivumilia kama vile Ayubu). [uw-SW uku. 60 fu. 13]

29. Mojapo lile shtaka lenye sehemu tatu lililofanyizwa na viongozi wa kidini wa Kiyahudi dhidi ya Yesu, kama ilivyorekodiwa kwenye Luka 23:2, shtaka lililohangaisha Pilato lilikuwa kuhusu Yesu (kupotosha taifa la Kiyahudi; kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi; akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo mfalme). [gt-SW sura 121]

30. Kwenye Zaburi 63:3, Daudi kwa hakika alikuwa akisema kwamba kuwa na uhusiano mzuri pamoja na Yehova kulikuwa (jambo lililo na ubora wa pili maishani; ni kama uhai; hata jambo bora zaidi kuliko uhai wenyewe). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w85-E 4/1 uku. 4.]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Zab. 86:1, 2; Mt. 26:52; Yn. 13:1-17; Yn. 15:8; Ebr. 13:5, 6

31. Kujapokuwa bei za juu na kuenea kwa kutoajiriwa, kadiri tunavyojitahidi wenyewe kupatana na imani yetu, Yehova atahakikisha kwamba tuna yale tunayohitaji. [uw-SW uku. 89 fu. 6]

32. Wakristo wa kweli si sehemu ya ulimwengu; kwa hiyo, hawatumii silaha za kimwili. [gt-SW sura 118; ona w94-SW 6/1 uku. 12.]

33. Ingawa huenda tukateseka kutokana na mahangaiko na mshuko wa moyo kwa sababu ya matatizo tuliyo nayo, twaweza kuwa na uhakika kwamba Yehova atatoa uangalifu duniani na kusikiliza sala zetu za unyenyekevu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 12/15 uku. 9 maf. 3, 4.]

34. Twaweza kumtukuza Mungu kikweli kwa kuonyesha sifa kama za Kristo, hasa upendo, na kushiriki kikamili iwezekanavyo katika utendaji wa kufanya wanafunzi. [gt-SW sura 116 fu. 19]

35. Tukiwa Wakristo twapaswa kuwa tayari kuwatumikia wengine bila upendeleo, hata kazi iwe ni ya umaana mdogo au isiyopendeza. [gt-SW sura 113]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki