Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/95 kur. 5-6
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1995
Huduma Yetu ya Ufalme—1995
km 4/95 kur. 5-6

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Januari 2 hadi Aprili 17, 1995. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Mungu alipokubali toba ya Daudi kwa kufanya dhambi na Bath-sheba, Daudi na nyumba yake hawangepatwa na matokeo mabaya ya mwenendo wake wenye kosa. [uw-SW uku. 127 fu. 5]

2. Kanuni ya msingi ya Mithali 11:1 ni kwamba twapaswa kuwa wenye adili na wanyoofu katika mazoea yetu yote ya kibiashara ikiwa twataka upendeleo wa Yehova. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 11/15 uku. 19.]

3. Kukubali shauri ni ishara ya udhaifu. [uw-SW uku. 127 fu. 4]

4. Mithali 14:17 hutoa uangalifu kwanza kwa hisia za moyoni kwa sababu mara nyingi hizo hutangulia matendo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 8/15 kur. 20-21.]

5. Wote wanaomwita Yesu Bwana wataokolewa. [uw-SW uku. 105 fu. 5]

6. Katika 33 W.K., alipofufuliwa na kutwaa mahali pake kwenye mkono wa kuume wa Mungu, Yesu alianza kutawala wakati huo juu ya wanafunzi wake watiwa-mafuta. (Kol. 1:13) [gt-SW sura 132]

7. Yapata miaka 3,000 kabla wanasayansi hawajavumbua msimbo-jeni, Zaburi 139:13-16 lilionyesha ujuzi wa jambo hilo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 5/15 uku. 4.]

8. Mithali 8:22-31 ni ufafanuzi tu wa hekima. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 5/15 uku. 28.]

9. Mkristo wa kweli hapaswi kuchukia kitu chochote. [Usomaji wa Biblia kila juma; w92-SW 1/1 uku. 21.]

10. Mithali 11:25 ni kielelezo cha fikira au mawazo yenye ulingani katika mtindo wa kishairi wa Kiebrania, na Mithali 10:7 ni kielelezo chenye ulingani tofauti. [si-SW uku. 107 fu. 7]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Kwa nini Zaburi ni zaidi ya kuwa fasihi kuu? [si-SW uku. 104 fu. 23]

12. Yesu alipata manufaa gani kwa kujua Zaburi? [si-SW uku. 105 fu. 30]

13. Ni nani aliyempa Sulemani hekima yake, na hilo lapaswa kutufanya tuthamini nini tusomapo Mithali? [si-SW uku. 106 fu. 1]

14. Mariamu Magdalene alifikiri ni nani aliyekuwa Yesu aliyefufuliwa alipoongea naye bustanini, na nini kilichomsaidia amtambue kwa usahihi? [gt-SW sura 128]

15. Ni washiriki gani wawili wa Sanhedrini waliokuwa waoga kutambuliwa wakiwa na Yesu waliosaidia kutayarisha mwili wake kwa ajili ya maziko? [gt-SW sura 127]

16. Twaweza kuonyeshaje kwamba katika utendaji wetu wa kila siku kwamba tuna upendo wa kujidhabihu kwa ajili ya ndugu zetu? [uw-SW kur. 132-133 maf. 3, 4]

17. Ni tukio gani la kihistoria linalosimuliwa na Zaburi 136:10-15, na nini kilichompata Farao? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 6/15 uku. 5.]

18. Ni makusudi gani mawili ambayo damu ya Kristo iliyomwagwa hutimiza? [uw-SW uku. 115, fu. 13]

19. Kwa nini mitume waaminifu, Yakobo ndugu-nusu wa Yesu, na wanafunzi zaidi ya 500 walisadiki kwamba Yesu alikuwa amefufuliwa? [gt-SW sura 131]

20. Ni nini kilichomfanya Yesu Kristo kuwa yule mtu mkuu zaidi aliyepata kuishi? [gt-SW maelezo ya utangulizi]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Katika hotuba yake yenye kujulikana sana kwenye Pentekoste 33 W.K., Petro alinukuu kwa kurudia kutoka kitabu cha _________________________ ; katika pindi hiyo watu karibu _________________________ walibatizwa na wakaongezwa kwenye kutaniko. [si-SW uku. 105 maf. 25, 26]

22. Zaburi ilitabiri kwamba Yesu angepewa ________________________ anywe, kwamba kura zingepigwa kwa ajili ya ________________________ yake ya nje, na kwamba angeonekana kana kwamba ameachwa na ________________________ . [si-SW uku. 105 fu. 30]

23. Tengenezo la Yehova ni la kitheokrasi, ikimaanisha kuwa _________________________ ; Yehova huandaa mwelekezo kupitia Kichwa cha kutaniko, _________________________ , kupitia Neno Lake, ________________________ ; na Yesu amemkabidhi daraka la kipekee “ _________________________ .” (Mt. 24:45) [uw-SW kur. 118-119, maf. 4-6]

24. Wakiwa tofauti na wale 144,000 wanaochukuliwa kwenda mbinguni, “ ________________________ ,” ambao hakuna mtu angeweza kuuhesabu, wataokoka ile _______________ papa hapa _________________________ . (Ufu. 7:9, 14, Habari Njema kwa Watu Wote) [uw-SW uku. 104 maf. 3, 4]

25. Ili kufikia uamuzi wenye upendeleo wa Mungu, baraza liongozalo la karne ya kwanza lilifikiria kwa uangalifu yale ambayo _________________________ yaliyopuliziwa yalisema juu ya fundisho lililotokea pamoja na uthibitisho wa utendaji wa _________________________ . (Mdo. 15:6-29) [uw-SW uku. 120 fu. 8]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Wakati wa kutundikwa kwake, Yesu alipewa divai ikiwa na manemane, lakini alikataa kuinywa kwa sababu (Sheria ilikataza; alikuwa Mnathiri; alitaka kuwa na nguvu zake zote za kufikiri). [gt-SW sura 125]

27. Kufua mavazi yetu na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo kwamaanisha kwamba (tuache kufanya dhambi; tuone uhitaji wetu wa ubora wenye kufunika dhambi wa dhabihu ya Yesu; tutoe maisha zetu wakfu kwa Mungu na kubatizwa). [uw-SW uku. 106 fu. 7]

28. Yesu alitangazwa kuwa asiye na hatia angalau mara tano na (Herode; Pilato; Feliki), ambaye baadaye alikubali madai ya ukatili ya Wayahudi na akamtoa Yesu ili auawe. [gt-SW sura 124]

29. Watumishi wote waaminifu wa Mungu waliokufa na waliobaki wakiwa wafu kabla ya Pentekoste (36; 35; 33) W.K. hawakutiwa mafuta kwa roho takatifu kwa ajili ya maisha ya kimbingu. [uw-SW uku. 111 fu. 5]

30. Shetani hubisha kwamba wanadamu wote wanahamasishwa na (upendo; chuki; tamaa ya kupata faida ya kibinafsi) na kwamba hangaikio lao kuu ni la (jina la Mungu; wengine; ubinafsi). [uw-SW uku. 124 fu. 14]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Mit. 3:27, 28; Yn. 19:4-6; 19:25-27; Rum. 15:2, 3; Ufu. 7:16, 17

31. Wakristo wana daraka la kutunza wazazi wao waliozeeka. [gt-SW sura 126]

32. Sisi twahangaika kikweli jinsi kuonekana kwetu kunavyoweza kuathiri wengine, kwa hiyo twaacha kwa hiari kujipendeza wenyewe. [uw-SW uku. 130 maf. 10, 11]

33. Tupatapo fursa ya kufanyia wengine mema, iwe ni katika njia ya kiroho au ya kimwili, twapaswa kutwaa fursa na kusaidia wanadamu wenzetu, hasa ndugu zetu wa kiroho. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 12/15 uku. 20.]

34. Fahari ya unyamavu na utulivu tunapokabili uadui kwaweza kumletea Yehova heshima na kupata heshima ya wanadamu. [gt-SW sura 123]

35. Tayari twaanza kufurahia hali zilizoahidiwa ambazo zaitwa kwa kufaa “paradiso ya kiroho.” [uw-SW kur. 107-108 maf. 9-11]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki