Matangazo
◼ Fasihi ya kutumiwa wakati wa Septemba: Kitabu Kuishi Milele kitatumiwa, na jitihada zapasa kufanywa ili kuanzisha mafunzo ya Biblia nyumbani. Oktoba: Maandikisho ya Amkeni! au Mnara wa Mlinzi. Novemba: Toa New World Translation pamoja na kitabu Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu? TAARIFA: Makutaniko ambayo bado hayajaagiza vifaa vya kampeni vilivyotajwa juu yapaswa kufanya hivyo katika Agizo la Fasihi lao la kila mwezi litakalofuata (S-14-SW).
◼ Mwangalizi-msimamizi au mtu fulani aliyewekwa naye apaswa kukagua hesabu za kutaniko katika Septemba 1 au upesi iwezekanavyo baada ya hapo. Tangazieni kutaniko jambo hilo lifanywapo.
◼ Wahubiri wanaopanga kutumikia wakiwa mapainia-wasaidizi katika Oktoba wapaswa kutoa maombi yao mapema. Hili litaruhusu wazee wafanye mipango inayohitajiwa kwa ajili ya fasihi na eneo.
◼ Wazee wanakumbushwa watekeleze maagizo yaliyotolewa kwenye kurasa 21-23 za Mnara wa Mlinzi la Aprili 15, 1991, kuhusu watu wowote waliotengwa au waliojitenga na ushirika ambao huenda wana mwelekeo wa kutaka kurudishwa.
◼ Orodha ya Bei mpya imetayarishwa, na nakala nne zinapelekewa kila kutaniko. Zinapaswa kugawiwa kwa mwandishi na kwa ndugu wanaotunza fasihi, magazeti, na hesabu.
◼ Kuanzia na toleo la Agosti 1, 1995, chapa ya kila mwezi ya Mnara wa Mlinzi itapatikana katika lugha ya Punjabi.
◼ Tunafurahi kuwajulisha kwamba mipango imekamilishwa ya kufanya ziara za matembezi kwenye mahali pa ujenzi wa majengo ya Betheli Nairobi. Kwa sasa ziara zitawezekana kila Jumatano hadi Jumamosi pekee kutoka 2:00 hadi 5:30 asubuhi na kutoka 7:00 hadi 10:00 alasiri. Mpango huu utaanzia Jumatano, Septemba 6, 1995. Tafadhali hakikisheni kuja na Mwelekezo wa Mapema Kuhusu Tiba/ Ondoleo la Hatia ili kuingia katika mahali pa ujenzi.
◼ Vichapo Vinavyopatikana:
Gujarati: Ni Nani Hasa Anayeutawala Ulimwengu? (Trakti Na. 22). Kihindi: Je! Ulimwengu Huu Utaokoka? (Trakti Na. 19); Faraja kwa Walioshuka Moyo (Trakti Na. 20); Furahia Maisha ya Familia (Trakti Na. 21); Ni Nani Hasa Anayeutawala Ulimwengu? (Trakti Na. 22).
◼ Kaseti Zinazopatikana:
Kiswahili: Kumsikiliza Mwalimu Mkuu (kaseti moja katika paketi)
◼ CD (Diski-Songamano) mpya zinazopatikana:
Kiingereza: Sing Praises to Jehovah on Compact Disc (seti ya disketi nane).