Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 11/95 uku. 1
  • Wahubiri Wa Ufalme Wapendwa:

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wahubiri Wa Ufalme Wapendwa:
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1995
Huduma Yetu ya Ufalme—1995
km 11/95 uku. 1

Wahubiri Wa Ufalme Wapendwa:

Alhamisi, Juni 22, 1995, ilikuwa siku yenye kusisimua sana katika mahali pa ujenzi pa Betheli mpya. Saa 8:00 hivi usiku ile kreni ya tani 50 iliwasili mahali pa ujenzi hatimaye. Kikundi cha akina ndugu kiliondoka Mombasa mapema Jumatano asubuhi na kwa sababu ya pancha na matatizo mengineyo, hakikuwasili Nairobi hadi asubuhi iliyofuata. Kujapokuwa kuwasili kwa kreni katikati ya usiku, ilikuwa imesimamishwa Alhamisi alasiri, ikiwa tayari kuinua hadi katika mahali pazo sehemu za ukuta za kwanza za Jumba la Ufalme. Saa 7:30 alasiri sehemu ya ukuta kwenye upande wa jengo unaokabili barabara ya Elgeyo Marakwet ilikuwa imetenganishwa, kuinuliwa, kisha kuteremshwa katika mahali payo. Halafu walehemishaji wakaanza kazi ya kufungamanisha yale mabamba ya feleji pamoja na mabamba ya ile nguzo iliyo wima na paneli ya kwanza ilikuwa imesimamishwa mahali payo katika muda wa dakika 25 hivi. Kazi zote zilikuwa zimesimama kabisa katika mahali pa ujenzi na familia ya ujenzi ikapiga makofi kwa mshindo wakati paneli ya kwanza ilipofungamanishwa.

Tangu wakati huo paneli zote za ukuta za Jumba la Ufalme zimesimamishwa na kuanzia Septemba 1 vifaa vya paa vinawekwa. Twatumaini kutumia Jumba la Ufalme kwa makao ya muda kwa ajili ya baadhi ya wajitoleaji wengi walio katika mahali pa ujenzi. Kuelekea mwisho wa huu mradi zile kuta za ndani za muda tu zitaondolewa na Jumba la Ufalme litakamilishwa. Kwa hiyo hatupangi kutumia Jumba la Ufalme kwa ajili ya mikutano hadi karibu na ukamilisho wa huu mradi.

Paneli za ukuta za Jengo la Ghorofa Moja la Makazi, za Banda la Motokaa, na kuta mbili za Jengo la Bohari na Udumishaji zimesimamishwa. Kuwekwa kwa vifaa vya paa kwa ajili ya Jengo la Ghorofa Moja la Makazi kunaendelea na inatumainiwa kwamba jengo hili litakuwa tayari kukaliwa na wajitoleaji wa ujenzi kuanzia Desemba 1.

Kazi ya kuchimba kwa ajili ya Majengo ya Makao, Huduma za Makao na Usimamizi na pia barabara za mahali pa ujenzi imekamilishwa. Msingi wa chini wa Jengo la Makao umekamilika na matayarisho yanaendelea kwa ajili ya muundo mkuu wa jengo hili.

Kumekuwa na itikio zuri kwa mwito wa wajitoleaji zaidi nasi twatumaini kwamba kukiwa na makao mengi zaidi tutaweza bado kualika ndugu na dada wengine zaidi walio tayari. Kuanzia Septemba 1 tuna wajitoleaji 120 katika mahali pa ujenzi nasi twatumaini kuongeza idadi hii hatimaye kufikia 200 hivi. Hivyo mwaweza kuona kwamba wajitoleaji zaidi wanahitajiwa. Twarudia kwamba uhitaji mkubwa zaidi ni wa wanaume vijana walio waseja wenye afya. Ili kutoa ombi kwa ajili ya utumishi wa ujenzi, ni lazima mwanamume kijana awe amejiweka wakfu na kubatizwa kwa angalau mwaka mmoja na awe mkazi wa Kenya. Ni lazima awe mtu mwenye kujitoa, wa kiroho, aliye tayari kufanya kazi ngumu. Ikiwa wewe una umri wa angalau miaka 19 na huzidi umri wa miaka 55, una afya nzuri kimwili na kihisiamoyo, ni mtu wa kiroho apendaye sana tengenezo la Yehova, basi waweza kustahili kushiriki katika kazi ya ujenzi wa tawi jipya. Waweza kumwomba mwangalizi-msimamizi wa kutaniko lako au kuandika moja kwa moja kwa ofisi ya tawi ili upate fomu ya kutoa ombi.

Twatoa shukrani zetu na uthamini wetu kwa watu mmoja-mmoja na makutaniko ambayo yamefanya michango yenye ukarimu kwa mradi huu wa ujenzi. Hakikisheni mmeandika waziwazi juu ya michango yenu hivi: “Mchango wa Ujenzi wa Betheli.” Sisi sote twaendelea kumtegemea Yehova ili kupata mwongozo, mwelekezo, na baraka juu ya jitihada hii ya kuendeleza masilahi ya Ufalme katika eneo hili. Twawapongeza kwa kazi yenu nzuri na kuwapelekea maonyesho ya upendo wetu mchangamfu wa Kikristo na kuwatakia mema.

Ndugu zenu,

Ofisi ya Tawi ya Nairobi

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki