Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Septemba 4 hadi Desemba 18, 1995. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. “Mtoto mwanamume” anayerejezewa katika Isaya 66:7 awakilisha kuzaliwa kwa taifa la kiroho la Wakristo watiwa-mafuta katika 1919, si kuzaliwa kwa Ufalme wa Kimesiya katika 1914. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 9/1 uku. 18.]
2. Isaya 38:5 hutusaidia tuelewe kwamba maombi ya kutoka moyoni yaweza kumsukuma Yehova afanye yale ambayo asingaliyafanya. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 4/1 uku. 14.]
3. Mwanadamu dhaifu sana aliye duniani aweza kumfanya Muumba wa ulimwengu wote mzima ahuzunike au aone shangwe. (Isa. 63:10) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 6/15 uku. 15.]
4. Yeremia 1:5 huunga mkono yale ambayo Biblia huonyesha juu ya uhai kuanza wakati wa kutungwa mimba. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 6/15 uku. 29.]
5. Isaya 53:5, 12 lilitabiri kwamba Yesu Kristo angekufa akiwa dhabihu ya fidia ili kufunika dhambi za wengine. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 10/1 uku. 14.]
6. Isaya 48:17 hasa latuambia tutumie Neno la Mungu maishani mwetu na tujionee kwamba kanuni zinazopatikana ndani yalo hufanya kazi kwelikweli. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 3/1 uku. 12.]
7. Ingawa Mashahidi wa Yehova hawashiriki kwa vyovyote mambo ya kisiasa, wao hawaingilii yale ambayo wengine wanafanya kama vile kujiunga na chama cha kisiasa, kugombea cheo, au kupiga kura katika mambo ya uchaguzi. [uw-SW uku. 166 fu. 12]
8. Watumishi waaminifu wa Mungu kabla ya wakati wa Kristo hawakujua juu ya ulimwengu mpya tunaotumaini. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 2/15 uku. 11.]
9. Sairasi alikuwa “mpakwa-mafuta” wa Yehova hata ingawa hakuna uthibitisho kwamba mafuta halisi yalimwagwa juu yake. (Isa. 45:1) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 11/15 uku. 30.]
10. Ili kumtumikia Mungu kwa ujitoaji kamili, Wakristo wahitaji kujua siku na saa ambayo Yehova ataondolea mbali mfumo wa kidunia wa Shetani. [uw-SW uku. 176 fu. 2]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Ni lini ambapo Mkristo apaswa kuzungumza na daktari wake juu ya uamuzi wake wa kujiepusha na damu? [uw-SW uku. 158 fu. 9]
12. Ni kwa njia gani Yesu hakuwa sehemu ya ulimwengu? [uw-SW uku. 161 fu. 2]
13. Kusema Neno la Mungu kwa ujasiri haimaanishi nini? [uw-SW uku. 175 fu. 13]
14. Ikiwa kwa kweli twathamini habari njema, tuna daraka gani? [uw-SW uku. 169 fu. 2]
15. Kati ya mataifa yote duniani, ni lipi lililo “taifa lenye uadilifu linaloshikilia mwenendo mwaminifu” kuelekea Mungu, na ni nani wanaoongezwa kwenye taifa hilo? (Isa. 26:2, 15) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 1/1 kur. 10, 11.]
16. Kulingana na Isaya 32:1, 2, ni nini lililo daraka kuu la wazee? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 4/1 uku. 30.]
17. Ufundishaji wa kimungu umekuwa na matokeo gani yanayoweza kuonwa waziwazi miongoni mwa Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote? (Isa. 54:13) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 3/1 uku. 17.]
18. Ni katika vitabu vipi na sura zipi ambapo tatu kati ya Gospeli huandaa habari juu ya ishara yenye mambo mengi inayotambulisha “umalizio wa mfumo wa mambo”? [uw-SW uku. 178 fu. 5]
19. Kwa nini katika rekodi ya historia ya Senakeribu yeye hakuweza kujivuna juu ya kushinda jiji kuu la Yuda, Yerusalemu, kama vile alivyojivuna juu ya ushindi wake wa ngome ya Yuda Lakishi? (Isa. 37:36) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 6/1 uku. 6.]
20. Ni nani na ni nini kinachofananishwa na “Leviathani” katika Isaya 27:1, NW? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 8/15 uku. 31.]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Mkristo anapolazwa hospitalini, anapaswa kuomba kwa _________________________ kwamba damu isitumiwe, na apaswa _________________________ kibinafsi juu ya hilo na daktari atakayeshughulikia kisa chake. [uw-SW uku. 158 fu. 9]
22. Njia mbili ambazo kwazo twaonyesha tegemeo letu kwa Yehova ni kwa kuhudhuria _________________________ kwa ukawaida na kwa kumgeukia Yeye katika _________________________. [uw-SW kur. 170-171 maf. 5-7]
23. Yesu alikuwa jiwe la _________________________ kwa Wayahudi, lakini akawa _________________________ la msingi ambalo juu yalo Yehova ajenga nyumba yake ya kiroho kwa utimizo wa Isaya 8:14 na 28:16. [si-SW uku. 123 fu. 36]
24. Usimamizi unaorejezewa katika Waefeso 1:9, 10 wamtegemea _________________________, na kupitia yeye wanadamu wanaletwa katika hali yenye _________________________ mbele za Mungu, baadhi yao wakiwa na taraja la kuwa _________________________, wengine _________________________. [uw-SW uku. 186 fu. 6]
25. “Wana wa Mungu” wanaorejezewa katika Warumi 8:19-21 ni wana wapakwa-mafuta wa kiroho ambao wamepata zawadi yao ya _________________________, nao watafunuliwa wakati wanadamu _________________________ waonapo uthibitisho kwamba wameanza kutenda, wakishiriki na Kristo katika _________________________ mfumo huu wa mambo ulio mbovu. [uw-SW uku. 188 fu. 11]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Wakristo wa mapema walishtakiwa kuwa wenye kuchukia jamii ya kibinadamu kwa sababu wao (wasingesema na wasioamini; hawakuabudu sanamu; waliepa vitumbuizo vya jeuri na visivyo vya adili). [uw-SW uku. 163 fu. 7]
27. Katika kielezi cha Yesu katika Mathayo 13:36-43, ngano yawakilisha (wanaume waaminifu wa kale; umati mkubwa; Wakristo waliopakwa mafuta), ilhali magugu yawakilisha (wote wasioamini; Wakristo wa uongo; Waandishi na Mafarisayo). [uw-SW uku. 180 fu. 7]
28. Baada ya watawala wa kisiasa kuharibu dini bandia, wao watageukia kwa chuki (mfumo wa kibiashara; Umoja wa Mataifa; wale wanaotegemeza enzi kuu ya Yehova). [uw-SW uku. 182 fu. 13]
29. Katika 1914 kulikuwa karibu (1,100; 5,100; 10,100) waliokuwa wakihubiri kwa bidii. [Usomaji wa Biblia kila juma; w94-SW 9/1 uku. 16]
30. Tuna wasifu kamili zaidi wa Yeremia kuliko wowote wa manabii wengineo wa kale isipokuwa (Danieli; Isaya; Musa). [si-SW uku. 124 fu. 5]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Law. 17:11, 12; Isa. 43:10; Yer. 7:31; Yn. 8:41, 44, 47; Mdo. 4:13
31. Elimu ya kilimwengu ya kiasi haimfanyi mtu asistahili kuwa mtangazaji wa habari njema mwenye ujasiri. [uw-SW uku. 172 fu. 8]
32. Utumizi pekee wa Kimaandiko ambao damu ingeweza kutumiwa wakazia utakatifu wayo na wakariri thamani ya dhabihu ya Kristo. [uw-SW uku. 159 fu. 11]
33. Vitendo vya mtu na mtazamo aonyeshao hufunua kwa wazi zaidi kuliko maneno baba yake wa kiroho ni nani. [uw-SW uku. 186 fu. 5]
34. Yehova hana mtangulizi; hakuna mungu aliyekuwako kabla yake, na hakutakuwa na yeyote baada yake kwa sababu yeye ni wa milele, akiwa Mwenye Enzi Kuu Mkuu Zaidi. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 1/15 uku. 22.]
35. Watu wazima walio wengi leo hata hawawezi kufikiri juu ya kutoa watoto wao kuwa dhabihu kwa sanamu, lakini mamilioni ya watoto huangamizwa kimakusudi kupitia utoaji-mimba, na mamilioni ya vijana wametolewa dhabihu juu ya madhabahu ya vita. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 1/15 uku. 31.]