Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/95 uku. 7
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1995
Huduma Yetu ya Ufalme—1995
km 12/95 uku. 7

Matangazo

◼ Fasihi itakayotumiwa wakati wa Desemba: Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Januari: Kitabu chochote chenye kurasa 192 kilichochapishwa kabla ya 1982 ambacho kutaniko laweza kuwa nacho akibani, kwa nusu-bei kwa wahubiri na pia mapainia kwa nusu-bei ya painia. Makutaniko ambayo hayana akiba ya vitabu hivyo yaweza kutoa Kuokolewa Kuingia Katika Dunia Mpya. Februari: Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! TAARIFA: Makutaniko ambayo bado hayajaagiza vifaa vya kampeni vilivyotajwa juu yapaswa kufanya hivyo katika Fomu ya Kuomba Fasihi yao ya kila mwezi itakayofuata (S-14-SW).

◼ Makutaniko yapaswa kuanza kuagiza mabuku yaliyojalidiwa ya Watchtower na Awake! ya 1995 pamoja na ombi lao la fasihi la Desemba. (Ona Orodha ya Bei, mafungu 6-8, 10.) Mabuku yaliyojalidiwa yatapatikana katika Kiingereza na Kifaransa. Hadi mabuku yaliyojalidiwa yatakapopatikana na upakizi umefanywa, haya yatakuwa “Yanayokuja” katika orodha ya upakizi ya kutaniko. Mabuku yaliyojalidiwa ni vifaa vya kuagizwa kipekee.

◼ Mwangalizi-msimamizi au mtu fulani aliyewekwa naye apaswa kukagua hesabu ya kutaniko Desemba 1 au upesi iwezekanavyo baada ya hapo. Tangazieni kutaniko jambo hilo lifanywapo.

◼ Ukumbusho wa 1997 utakuwa Jumapili, Machi 23, baada ya jua kushuka. Taarifa hii ya mapema ya tarehe ya mwadhimisho wa Ukumbusho wa 1997 imetolewa ili ndugu waweze kuhifadhi au kufanya maagano ya lazima kwa ajili ya majumba yapatikanayo ambapo kuna makutaniko kadhaa yatumiayo Jumba la Ufalme nayo yapaswa kutafuta majengo mengine.

◼ Kuanzia toleo la Mnara wa Mlinzi, la Agosti 1, 1995, toleo sawia la kila mwezi linatokezwa katika Punjabi.

◼ Kazi imemalizwa kuhusu CD-ROM, ambayo ni Watchtower Library—1995 Edition (Maktaba ya Watchtower—Toleo la 1995). Hii itakuwa na programu ambayo imefanyiwa marekebisho na itaongezea vichapo vilivyotolewa wakati wa 1995, 1994, na 1979-1970. Mambo hususa yatatolewa katika barua kutoka kwa Sosaiti yenye tarehe ya Novemba 25, 1995, kwa makutaniko yote. Maombi ya CD hii katika lugha moja au zaidi yapaswa kuletwa kutoka kwenye kutaniko kabla ya Januari 15, 1996.

◼ Tunafurahi kutangaza kwamba katika Oktoba 5, 1995, Association of Jehovah’s Witnesses of Tanzania ilisajiliwa tena.

◼ Andiko la mwaka wa 1996 litakuwa: “Iweni Watendaji wa Neno.”—Yakobo 1:22. Itakuwa vizuri kuwa nalo kwenye Majumba ya Ufalme yetu kwa wakati ufaao.

◼ Vichapo Vinavyopatikana:

Gujarati: Furahia Milele Maisha Duniani!, Faraja kwa Walioshuka Moyo (Trakti Na. 20), Furahia Maisha ya Familia (Trakti Na. 21). Kiingerza: Kingdom Interlinear Translation of the Greek Scriptures. Kinyarwanda: Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha. Punjabi: Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa. Urdu: Mashahidi wa Yehova Wanaamini Nini? (Trakti Na. 14); Uzima Katika Ulimwengu Mpya Wenye Amani (Trakti Na. 15).

◼ Vidiokaseti Zinazopatikana:

Kiingereza Kwa Ajili Ya Viziwi: You Can Live Forever in Paradise on Earth (Vidiokaseti Na. 1), Does God Really Care About Us?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki