Habari Za Kitheokrasi
Albania: Watangazaji 600 walioripoti Agosti walikuwa kilele cha mfululizo cha 28.
Angola: Kilele kilichopita vyote cha watangazaji 26,129 kilifikiwa mwishoni mwa mwaka wa utumishi. Pia kulikuwa na kilele cha mapainia wa kawaida cha 1,309. Watangazaji walifanya wastani wa saa 15 na mafunzo ya Biblia mawili katika Agosti.
Chile: Wakati wa mwezi wa Agosti, kilele kipya kuliko vyote cha watangazaji kilifikiwa, kukiwa jumla ya 50,283! Kwa mara ya kwanza, ile alama ya 50,000 ilipitwa. Watangazaji walitumia wastani wa saa 12 katika utumishi wa shambani. Jumla ya mafunzo ya Biblia nyumbani 63,732 yaliongozwa.
Uingereza: Tunafurahia kuripoti kwamba kilele kipya kilichopita vyote cha watangazaji 132,440 kilifikiwa katika Agosti. Hiki chawakilisha ongezeko la asilimia 2 kuliko mwaka wa utumishi uliopita.