Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/96 kur. 5-6
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1996
Huduma Yetu ya Ufalme—1996
km 4/96 kur. 5-6

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Januari 1 hadi Aprili 22, 1996. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Maadamu Mkristo ahisi kwamba anafanya jambo lililo sawa, maamuzi yake yatakuwa mazuri. (Mit. 14:12) [uw-SW uku. 8 fu. 8(2)]

2. Fundisho la Utatu lilitokana na Jumuiya ya Wakristo. [uw-SW uku. 15 fu. 8]

3. Ijapokuwa Sheria ya Musa ilipitilia mbali, Biblia haionyeshi chochote kwamba Amri Kumi zilitiwa ndani katika zile zilizofikia kikomo. [rs-SW uku. 272 fu. 1]

4. Kwa kulinganisha Warumi 8:16 na Warumi 1:7, inaweza kueleweka kwamba Paulo alikuwa akirejezea wanadamu wote kuwa “watoto wa Mungu.” [uw-SW uku. 26 fu. 12(3)]

5. Agano linalotajwa kwenye Yeremia 31:31, 33 hurejezea lile agano kwa ajili ya Ufalme ambalo Yesu hufanya pamoja na wafuasi wake watiwa-mafuta. [si-SW uku. 129 fu. 38]

6. Kitabu cha Maombolezo kina mashairi matano yenye kujaa maono ya moyoni, manne yakiwa ni mashairi ya muundo wa kialfabeti. [si-SW uku. 131 fu. 6]

7. Baada ya ufufuo wake, Yesu alijitokeza mara kadhaa—lakini mbele ya wanafunzi wake tu. [rs-SW uku. 335 fu. 1]

8. Wakristo wa kweli wanaingia katika pumziko la Mungu kwa kudhihirisha imani katika dhabihu ya Kristo na kwa kuacha kazi ambazo kwa hizo wanajaribu kujithibitisha wenyewe kuwa waadilifu. (Ebr. 4:10) [rs-SW uku. 274 fu. 1]

9. Usemi ulio katika vibano-duara kwenye Ufunuo 20:5 (NW), kuhusu “mabaki ya wafu” wanaokuja kwenye uhai, hurejezea ufufuo wa kidunia wa kondoo wengine. [rs-SW uku. 339 maf. 2-4]

10. Yesu alipojibu swali kuhusu ni amri gani iliyokuwa kubwa zaidi katika Sheria, hakutaja yoyote ya Amri Kumi. (Mt. 22:35-40) [rs-SW uku. 271 fu. 3]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Kwa kuwa upendo mwingi wa Yehova ulimchochea kumtuma Mwanawe ili atoe uhai wake kwa ajili yetu, upendo wetu kwa Mungu wapaswa utuchochee kufanya nini? (2 Kor. 5:14, 15) [uw-SW uku. 14 fu. 6]

12. Kutembea katika jina la Yehova kwamaanisha nini? [uw-SW uku. 18 fu. 14]

13. Twajifunza nini kuhusu sifa za Yehova kwa kusoma kitabu cha Maombolezo? (Omb. 3:22, 23, 32) [si-SW uku. 132 maf. 13, 15]

14. Ni usemi gani unaotumiwa kwa kurudiarudia kuwahusu Ezekieli na Yesu Kristo? (NW) [si-SW uku. 133 fu. 2]

15. Kwa nini ni jambo linalofaa kuamini kwamba wale wanaofufuliwa duniani watahukumiwa kwa msingi wa matendo yao ya wakati ujao? (Rum. 6:7) [rs-SW uku. 338 fu. 4]

16. Ni mambo gani makuu manne ambayo huchangia muungano unaofurahiwa na watu wa Yehova leo? [uw-SW kur. 8-9 maf. 8, 9]

17. Kwa nini twaweza kusema kwa haki kwamba matukio yanayohusiana na kuwapo kwa Kristo yafanyika kwa kipindi cha miaka mingi? (Mt. 24:37-39) [rs-SW uku. 127 fu. 2]

18. Kwa kuongezea sifa zenye kutokeza za Yehova za upendo, haki, hekima, na nguvu, twaweza kujifunza nini kuhusu utu wake wenye kuvutia kutokana na Kutoka 34:6, Zaburi 86:5, na Matendo 10:34, 35? [uw-SW uku. 13 fu. 3]

19. Baada ya kulinganisha Yohana 14:9, 10 na Luka 5:12, 13, kwa nini twaweza kukata kauli kwamba Yehova ni mwenye huruma nyororo kuelekea wanadamu wanaoteseka? [uw-SW uku. 25 fu. 12(1)]

20. Kwa nini Wakristo hawako chini ya wajibu wa kushika sabato ya kila juma? (Rum. 10:4) [rs-SW uku. 269 maf. 2, 3]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Ebed-meleki aliwakilisha ____________________ , watakaookolewa kwenye _________________________ kwa sababu walifanya urafiki na kusaidia ______________________ ya ndugu za Kristo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w83-SW 3/1 uku. 16 fu. 11.]

22. Ingawa Yesu anasemwa kuwa “mungu,” kwenye Yohana 17:3 yeye alimwita Yehova “Mungu wa _________________________ wa kweli,” na kwenye Yohana 20:17 yeye alimrejezea Yehova kuwa “Mungu ____________________________ naye ni Mungu _________________________ .” [uw-SW uku. 18 fu. 12]

23. Matukio yaliyosimuliwa kwenye Yeremia 52:5-11 yalitukia katika ________________________ K.W.K. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 4/1 uku. 14 fu. 18.]

24. Ufunuo 1:7 inaposema kwamba baada ya kurudi kwa Kristo “kila jicho litamwona,” inarejezea, si kuona kwa _________________________ , bali _________________________ wa akili. [rs-SW uku. 129 fu. 4]

25. Baada ya ufufuo wake Yesu hakuonekana sikuzote katika _________________________ uleule, labda ili kukazia kwenye akili za wanafunzi uhakika wa kwamba yeye wakati huo alikuwa _________________________ , na kwa hiyo _________________________ mara hiyo hata na washiriki wake wa karibu sana. [rs-SW uku. 335 fu. 4]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Biblia ni Neno la Mungu kwa sababu (watafsiri waliipa kibandiko hicho; watu wenye kujitolea kimungu waliiandika; Mungu kwa uwezo alielekeza kuandikwa kwayo). [uw-SW uku. 20 fu. 2]

27. Ukisoma kurasa (mmoja; mbili; nne) tu za Biblia kila siku, utaikamilisha kwa karibu (miezi sita; miezi tisa; mwaka mmoja). [uw-SW uku. 24 fu. 9]

28. Vizuizi vya adili havikuondolewa wakati Sheria ya Musa ilipoondolewa, ambayo ilitia ndani zile Amri Kumi, kwa sababu chini ya mpango wa Kikristo, (kila jumuiya ingesitawisha viwango vyayo yenyewe; watu wanapaswa kuongozwa tu na dhamiri yao; vingi vya viwango vya adili vya zile Amri Kumi vilisemwa tena katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo). [rs-SW uku. 273 fu. 1]

29. Yehova ‘alimhadaa’ Yeremia kwa habari ya kwamba (alimhadaa ahubiri ujumbe wa hukumu; alimtumia kutimiza jambo ambalo hangelifanya kwa uwezo wake mwenyewe; hakuleta uharibifu ambao Yeremia alikuwa ametabiri). (Yer. 20:7) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 5/1 uku. 31.]

30. Usemi “makaburi ya ukumbusho,” unaopatikana kwenye Yohana 5:28 (NW), hurejezea (makaburi yakiwa moja-moja; kaburi la kawaida la wanadamu; kukumbukwa na Mungu kwa mtu aliyekufa). [rs-SW uku. 340 par. 1]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Mit. 3:5, 6; Yer. 23:33; 32:9, 10; Omb. 3:44; Ufu. 15:3, 4

31. Msingi wa muungano wa kweli wa ibada ni kumjua Yehova na kuishi kupatana na njia zake za uadilifu. [uw-SW uku. 5 fu. 1]

32. Mwendo wetu wote wa maisha—haidhuru tuko wapi, haidhuru tunafanya nini—umepasa ushuhudie kwamba kufikiri kwetu na makusudi yetu ni yenye kumwelekea Mungu. [uw-SW uku. 10 fu. 11]

33. Yehova hasikilizi sala za waovu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 7/15 uku. 15.]

34. Ujumbe mzito wa kiunabii kutoka Neno la Mungu umejaa balaa, ukitangaza uharibifu unaokaribia wa Jumuiya ya Wakristo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 3/1 uku. 12 maf. 18, 20.]

35. Tunapoingia katika shughuli za biashara pamoja na waabudu wenzetu wa Yehova, mapatano yaliyoandikwa yaweza kuzuia kutoelewana ambako kwaweza kutokea baadaye. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 5/1 uku. 30.]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki