Habari Za Kitheokrasi
Habari fupi ya karibuni kuhusu ujenzi wa jengo jipya la tawi: Jengo la Makao la Ghorofa Moja sasa limekamilika na linakaliwa kabisa. Vifaa vya paa vimewekwa juu ya majengo ya Banda la Motokaa na Bohari na Udumishaji. Kuta za ndani za majengo haya zinajengwa. Kazi katika jengo la Makazi imefikia ghorofa ya pili na jengo la Usimamizi na Utumishi limefikia ghorofa ya kwanza. Kwa sasa kuna wajitoleaji wa wakati wote 160 na wajitoleaji kadhaa wasio wa wakati wote kutoka makutaniko tofauti-tofauti katika eneo la Nairobi.
Wengi walinufaika na hotuba ya mwangalizi wa eneo la kanda ya dunia katika nchi zile alizotembelea. Tarakimu zaonyesha hudhurio la ujumla 11,760 katika nchi zote tano.
Tunafurahi kuripoti kwamba Tanzania imefikia watangazaji 6,000 katika mwezi wa Februari kukiwa na kilele cha wakati wote cha watangazaji 6,084.
Jumba la Ufalme la Nairobi Westlands liliwekwa wakfu hivi majuzi, 301 walisikiliza programu yenye kutia moyo.