Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Mei 6 hadi Agosti 19, 1996. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Dhabihu moja ya Yesu ilichukua mahali pa dhabihu zote zilizotolewa chini ya Torati ya Musa. [uw-SW uku. 33 fu. 8(4)]
2. ‘Gogu wa Magogu’ ni ufananisho unaorejezea serikali za ulimwengu huu. (Eze. 38:2) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 8/15 uku. 27 fu. 2.]
3. Kama vile Ohola alivyokuwa dada mkubwa wa Oholiba, kama ionyeshwavyo katika Ezekieli sura ya 23, vivyo hivyo Ukatoliki wa Kiroma ni dada mkubwa wa Uprotestanti, na matengenezo yote mawili yamejichafua kwa kufanya uzinzi wa kiroho pamoja na mamlaka za kibiashara na za kisiasa za ulimwengu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 4/1 30.]
4. Ili mtu awe mtakatifu, lazima afe. [rs-SW uku. 407 fu. 2]
5. Ukweli wa kwamba Biblia hujifasili yenyewe waweza kuonwa kutokana na njia ambayo Ufunuo 21:8 huelewesha wazi kinachomaanishwa na Shetani kutupwa katika “ziwa la moto na kiberiti,” kama ielezwavyo kwenye Ufunuo 20:10. [rs-SW uku. 288 fu. 4]
6. Yakobo 4:17 na Ezekieli 33:7-9 hupatana, kuonyesha kwamba ni ujuzi wa yale ambayo Mungu ataka kutoka kwetu unaotufanya tumtolee hesabu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 4/1 uku. 7 fu. 1.]
7. Danieli alijithibitisha kuwa nabii wa kweli kwa kueleza maana ya ule mfano katika ndoto baada ya Mfalme Nebukadreza kumfafanulia. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona Danieli 2:7-9, 26.]
8. Maji yanayotiririka kutoka kwenye hekalu la njozi inayofafanuliwa kwenye Ezekieli 47:1 huwakilisha nguvu ya kusafisha ya ubatizo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 27 fu. 20.]
9. Usiogope kamwe kukataa kujiunga na mtu anayekusihi ‘uone raha kidogo,’ hata kama mwaliko huo watoka kwa mtu anayejidai kuwa Mkristo. (2 Pet. 2:18, 19) [uw-SW uku. 43 fu. 11]
10. Mungu aliumba Ibilisi. [rs-SW uku. 286 fu. 2]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Jitihada ya Abrahamu ya kutoa Isaka yapaswa kutusaidia tuthamini nini? (Mwa. 22:1-18) [uw-SW uku. 32 fu. 8(1)]
12. Kwa nini inaweza kusemwa kwamba mgawo wa kazi ambao Yehova Mungu aliwapa Adamu na Hawa ulikuwa sheria? (Mwa. 1:28; 2:15) [uw-SW uku. 38 fu. 2]
13. Ni kwa njia gani Mashahidi wa Yehova watiwa-mafuta na washiriki wao lazima wawe kama Ezekieli? (Eze. 11:25) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 16 fu. 3.]
14. Ni nani wanaotiwa katika uzao wa Nyoka? [uw-SW uku. 30 fu. 3]
15. Zaidi ya kumshitaki Yehova kuwa mwongo, Shetani alidai kwamba Mungu alikuwa akinyima viumbe wake nini? (Mwa. 3:1-5) [uw-SW uku. 46 fu. 1]
16. Ni nini ule “mji” unaorejezewa kwenye Waebrania 11:10? [uw-SW uku. 48 fu. 6]
17. Ni katika njia zipi mbili inaweza kusemwa kwamba Adamu na Hawa walikufa “katika siku” ya kula kwao ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya? (Mwa. 2:17) [uw-SW uku. 56 fu. 5]
18. Ni nini maana ya jina la Mungu, Yehova? [kl-SW uku. 25 fu. 7]
19. Kwa sababu gani hakuna kupingana kati ya maneno ya Paulo kwamba twaokolewa kwa imani na maneno ya Yakobo kwamba lazima tuwe na matendo? (Efe. 2:8, 9; Yak. 2:14, 26) [rs-SW uku. 418 fu. 4-7]
20. Ni nini kilicho chanzo kikuu cha ithibati ya kwamba Ibilisi yuko, tuna ushuhuda wa nani wa kuona kwa macho usio na shaka, na kiwango cha uovu ulio ulimwenguni chatuhakikishiaje kuwapo kwa Shetani? [rs-SW uku. 284 maf. 3, 4]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Kwa utimizo wa Ezekieli 21:26, ufalme ‘ulioinuka juu’ wa _________________________ ‘ulishushwa chini’ kwa kuharibiwa katika _________________________ , na zile falme zilizokuwa “chini” za _________________________ ‘zilikwezwa,’ zikaachwa zikiwa kwenye kudhibiti dunia bila kuvurugwa na ____________________________________ wa Mungu ulio kifananishi. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 19 fu. 16.]
22. Sehemu ya kitabu cha _________________________ kwa kweli ni _________________________ iliyoandikwa mapema ikikazia fikira kung’ang’ania mamlaka kwa zile falme katika karne nyingi. [si-SW uku. 138 fu. 1]
23. Ule mtajo “mtumishi wangu Daudi” kwenye Ezekieli 34:23 uliandikwa muda mrefu baada ya kifo cha _________________________ ; ni mtajo wa kiunabii na warejezea _________________________ . [si-SW uku. 137 fu. 31]
24. Kutoka 34:7 hurejezea jambo ambalo lingetokea kwa Waisraeli wakiwa _________________________ ikiwa wangetenda dhambi dhidi ya Mungu na kuchukuliwa wakaingie katika utekwa, kwa upande ule mwingine, Ezekieli 18:4 hurejezea mhesabio-lawama wa _________________________ kwa Mungu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 2/1 uku. 6.]
25. Uisomapo Biblia, ni vizuri kujiuliza jinsi uwezavyo kutumia mambo unayosoma _________________________ na jinsi uwezavyo kuyatumia ili usaidie _________________________ . [uw-SW uku. 26 fu. 12(4) na uku. 28 fu. 12(5)]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Hangaikio kuu la Mkristo maishani lapasa kuwa (kuwa na mapendeleo kutanikoni; kuokoka Har–Magedoni; kuwa na uhusiano mzuri pamoja na Yehova). [uw-SW uku. 42 fu. 9]
27. Watu wengi hukataa kutambua kwamba matatizo tuwezayo kupata maishani mara nyingi hutokea kwa sababu ya (watu wanaotaka kutuumiza; wakati na hali zisizotazamiwa; tamaa zetu wenyewe za dhambi na mashirika mabaya). (1 Kor. 15:33; Yak. 1:14, 15) [uw-SW uku. 44 fu. 13]
28. (Ujuzi wetu; uwezo wetu wa kufundisha; mwenendo wetu) unaonyesha tuko upande gani kuhusiana na lile suala kuu linalotia ndani uaminifu-mshikamanifu wetu kwa Mungu. [uw-SW uku. 52 fu. 12]
29. Walio wa kwanza kuwa “vyombo vya rehema” walikuwa (Mataifa; Wayahudi; Wasamaria waliotahiriwa), kisha (Mataifa; Wayahudi; Wasamaria waliotahiriwa), na hatimaye (Mataifa; Wayahudi; Wasamaria waliotahiriwa). (Rum. 9:23, 24) [uw-SW uku. 57-58 maf. 8, 10]
30. Yule hayawani-mwitu apokeaye nguvu zake kutoka kwa Shetani ni (mamlaka ya Muungano wa Uingereza na Marekani; Umoja wa Mataifa; mfumo wa kisiasa wa utawala wa dunia yote). (Ufu. 13:1, 2) [rs-SW uku. 287 fu. 2-uku. 288 fu. 2]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini: Mit. 27:11; Isa. 55:10, 11; Eze. 18:25; Dan. 1:8, 11-13; Mdo. 8:32-38
31. Uthamini kwa ile kweli na kwa yale ambayo Yesu Kristo amefanya kwa kutimiza unabii wa Biblia huchochea watu wenye mioyo ya kufuatia haki wabatizwe. [uw-SW uku. 32 fu. 7]
32. Vijana Wakristo hawapaswi kusita kujulisha kwa heshima wenye mamlaka na wanafunzi wenzao kwamba hawataasi dhamiri yao ya kimungu iliyozoezwa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 11/1 uku. 14 fu. 17.]
33. Kusudi la Mungu la awali kwa wanadamu na dunia litatimizwa. [kl-SW uku. 9 fu. 10]
34. Lazima sikuzote Wakristo wa kweli wawe tayari kurekebisha kufikiri kwao kupatane na njia za Yehova, na hatupaswi kamwe kuhisi kwamba shauri halali la Kimaandiko halitumiki kwetu na kulipuuza. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 11/1 uku. 31.]
35. Sababu moja ambayo Yehova Mungu hakumhukumu Ibilisi mara moja baada ya uasi wake katika Edeni ilikuwa ili awape fursa watumishi wa Mungu duniani wathibitishe uaminifu-mshikamanifu wao Kwake kwa matendo yao ya utii wenye upendo na kumthibitisha Ibilisi kuwa mwongo. [rs-SW uku. 287 fu. 1]