Habari Za Kitheokrasi
Kenya: Kuanzia Septemba 1 mizunguko mipya 4 imeanzishwa ikifikia idadi ya mizunguko 14 nchini.
Kuwekwa wakfu kwa Jumba la Ufalme la Maralal kulifanywa Juni 8 kukiwaletea kutaniko na wageni waliohudhuria shangwe.
Ujenzi wa Ofisi ya Tawi: Ijumaa Juni 21, 1996, ukuta wa mwisho wa jengo la Utumishi uliinuliwa ukawekwa mahali pao kwenye orofa ya kwanza. Familia ya ujenzi na ya Betheli zilifurahi kwa makofi yenye idili. Hii ni hatua ya maana ya maendeleo ya ujenzi! Yatazamiwa kwamba kufikia wakati mtakapopokea toleo hili la Huduma ya Ufalme Yetu jengo la Makazi na jengo la Usimamizi na Utumishi yatakuwa yamewekwa paa. Kuta za ndani, waya za umeme, na ufundibomba waendelea hima. Kutengenezwa kwa barabara na maegesho ya magari kwaendelea. Mradi huo waendelea kulingana na ratiba yenye lengo la kukamilishwa Juni 1997. Twathamini sana uungaji-mkono wenu wa kazi hii. Sisi sote twaendelea kuomba baraka na mwelekezo wa Yehova ili mradi huu ufikie ukamilisho wenye mafanikio.