Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 11/96 uku. 3
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1996
Huduma Yetu ya Ufalme—1996
km 11/96 uku. 3

Matangazo

◼ Toleo la fasihi la Novemba: Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Jitihada ya pekee itafanywa kufuatia maangusho yote, tukiwa na kusudi la kuanzisha mafunzo ya Biblia nyumbani. Desemba: New World Translation pamoja na kitabu Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu? Januari: Kitabu chochote chenye kurasa 192 kilichotangazwa kabla ya 1984 ambacho kutaniko laweza kuwa nacho akibani kitatolewa kwa nusu bei. Vichapo ambavyo vimechapishwa kwenye karatasi isiyochakaa au kugeuka rangi havipaswi kutiwa ndani ya toleo hili lililopunguzwa bei. Makutaniko ambayo hayana ugavi wa vitabu hivyo yaweza kutoa Kuokolewa Kuingia Katika Dunia Mpya au Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani.” Februari: Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! Tumia kitabu chochote cha zamani chenye kurasa 192 ulicho nacho akibani, kiwe badala.

◼ Makutaniko ambayo bado yana ugavi wa Habari za Ufalme trakti Na. 34 yanaweza kutia moyo watangazaji wazitoe kwa namna sawa na zile trakti nyingine, iwe ni mlango hadi mlango au mahali penginepo. Ikiruhusiwa, watangazaji wanaweza kuacha moja kwa wasiokuweko nyumbani, wakihakikisha imewekwa vizuri mahali isipoweza kuonekana na mpita-njia. Jitihada zapaswa kufanywa ili kuangusha nakala zote za ujumbe huu wenye thamani.

◼ Makutaniko yapaswa kuanza kuagiza 1997 Yearbook of Jehovah’s Witnesses pamoja na agizo lao la fasihi la Novemba. Kitabu-Mwaka hicho kitapatikana katika Kiarabu, Kichina, Kifaransa na Kiingereza. Hadi wakati Kitabu-Mwaka hicho kitakapopatikana na upakizi ufanywe, kitaonekana kuwa “Vinavyokuja” katika orodha ya upakizi ya kutaniko. Vitabu-Mwaka ni vifaa vya kuombwa kipekee.

◼ Vichapo Vinavyopatikana:

Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1997 —Kiingereza

Lasting Peace and Happiness—How Can You Find Them? —Kichina (Sahili)

◼ Vidio Kaseti Zinazopatikana:

Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele (Buku la nne)

—Lugha ya Ishara ya Kimarekani

Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele—(Buku la tano)

—Lugha ya Ishara ya Kimarekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki