Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Septemba 2 hadi Desemba 23, 1996. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. “Mnyama-mwitu” mwenye vichwa saba na pembe kumi anayefafanuliwa kwenye Ufunuo 13:1 kwa kweli ni Shetani Ibilisi. [uw-SW uku. 63 fu. 4]
2. Kwa kweli hakuna “samaki mkubwa” awezaye kummeza binadamu mzima. (Yona 1:17) [si-SW uku. 153 fu. 4]
3. Maoni ya Biblia kuhusu ngono yalianzishwa na binadamu walioishi miaka mingi iliyopita. [rs-SW uku. 255 fu. 2]
4. Unabii ulio kwenye Danieli 9:24, 25 huelekeza kwenye kuzaliwa kwa Yesu. [kl-SW uku. 36 fu. 8]
5. Mwanadamu mkamilifu hawezi kufanya kosa. [rs-SW uku. 63 fu. 3]
6. Kwa kuwa Shetani aweza kujigeuza mwenyewe kuwa malaika wa nuru, hatupaswi kuongozwa vibaya wakati baadhi ya vitu vinavyofanywa kwa njia ya uwasiliani-roho vionekanapo kuwa na manufaa za muda tu. [rs-SW uku. 146 fu. 2]
7. Unabii wa Hosea ulielekezwa hasa kwenye ufalme wa makabila mawili ya Yuda. [si-SW uku. 144 fu. 8]
8. Wale wanaotaka urafiki na himaya ya Yehova lazima waachane na ushiriki wote wa mikutano ya uwasiliani-roho na wafuate kielelezo kilichowekwa kwenye Matendo 19:19. [rs-SW uku. 149 fu. 4]
9. Kulingana na Sefania 3:9, watu wa Mungu wataunganishwa katika ulimwengu mpya kwa sababu wote watasema lugha moja—Kiebrania. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 6/1 uku. 30.]
10. Katika kutimizwa kwa Danieli 12:1, Mikaeli amekuwa “akisimama” tangu 1914 alipokuwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu wa kimbingu; hivi karibuni “atasimama” kwa jina la Yehova akiwa Mfalme-Mwanavita asiyeshindika, aletaye uharibifu kwenye mfumo huu mbovu. [Usomaji wa Biblia wa kila juma; ona w93-SW 11/1 uku. 23 fu. 23.]
Jibu maswali yafuatayo:
11. “Vitu vinavyotamanika vya mataifa yote” vinavyorejezewa kwenye Hagai 2:7 ni akina nani, na ‘vinakuja’ kwa njia gani? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 6/1 uku. 31 fu. 5.]
12. Ni ripoti gani ya Kimaandiko ya Waebrania watatu inayoonyesha kwamba utii wao kwa Mungu haukutegemea ulinzi na ukombozi wa kimungu? (Dan. 3:16-18) [si-SW uku. 141 fu. 19]
13. Ni andiko gani linalotabiri mahali pa kuzaliwa pa Mesiya? [si-SW uku. 156 fu. 6]
14. Kwa nini miujiza mingi inayofanywa kwa jina la Yesu haingekuwa uthibitisho wa kibali au utegemezo wa Mungu? [kl-SW uku. 46 maf. 6-7]
15. Ni katika njia gani 1 Wakorintho 15:45 huunga mkono yale ambayo Maandiko ya Kiebrania husema kuhusu nafsi? [rs-SW uku. 232 fu. 3]
16. Yesu alipomlilia Baba yake akisema “mikononi mwako naiweka roho yangu,” alikuwa akirejezea nini? (Luka 23:46) [rs-SW uku. 264 fu. 2]
17. Zaburi 146:4 (NW), hutumia msemo gani kuonyesha kwamba nguvu ya uhai iliyo ndani ya mtu hukoma kutenda wakati wa kifo? [rs-SW uku. 145 fu. 4]
18. Ni nani aliyetunga wazo la kwamba wanadamu hawafi kwelikweli, na ni wapi katika Biblia palipo na uwongo wa kwanza unaohusiana na fundisho hili la uwongo? [rs-SW uku. 146 fu. 1]
19. Kwenye Hagai 2:9, ni hekalu jipi lililokuwa ‘nyumba ya mwisho,’ ni jipi lililokuwa la ‘kwanza,’ na kwa nini utukufu wa ‘nyumba ya mwisho’ ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa lile la ‘kwanza’? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 6/1 uku. 30.]
20. Hosea 14:2 lilikuwa likisihi Waisraeli wafanye nini, na Mashahidi wa Yehova wanatimizaje unabii huo leo? (Ebr. 13:15) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 9/15 uku. 10 fu. 1-2.]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Mji wa _________________________ uliitwa mji wa damu na nabii _________________________ yapata miaka 200 baada ya _________________________ kutimiza kazi yake ya kupewa na Mungu huko. [si-SW uku. 154 fu. 10, uku. 160 fu. 10]
22. Twahitaji kumwabudu Mungu katika _________________________, tukichochewa na mioyo iliyojaa imani na upendo; lazima pia tumwabudu katika _________________________ kwa kujifunza Neno lake. [kl-SW uku. 45 fu. 4]
23. Ili tulindwe kiroho, hatupaswi kupuuza kuvaa sehemu yoyote ya suti kamili ya silaha kutoka kwa Mungu, ambayo ina “_________________________,” “bamba la kifuani la _________________________,” “vifaa vya _________________________ za amani,” “ngao kubwa ya _________________________,” “kofia ya chuma ya _________________________ ,” na “_________________________ wa roho.” (NW) [uw-SW uku. 68 fu. 14]
24. Wale wanaofuata dini za kimapokeo, ndani na nje ya Jumuiya ya Wakristo, wanafikiri wana nafsi _________________________ , ambayo ingefanya kusiwe na lazima ya _________________________. [uw-SW uku. 71 fu. 3]
25. Njia tatu za kuthibitisha kwamba Yesu alikuwa Mesiya ni (1) ________________________, (2) ___________ ______________, na (3) _________________________. [kl-SW kur. 34-38 maf. 6-10]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Uelewevu wa Amosi (8:11; 9:2, 3; 9:11, 12) ulisaidia baraza linaloongoza la karne ya kwanza kutambua kwamba yalikuwa mapenzi ya Mungu kwamba wasio Waisraeli wakusanywe katika kutaniko la Kikristo. (Mdo. 15:13-19) [si-SW uku. 150 fu. 16]
27. Wakati (Amosi; Yoeli; Habakuki) alipoitwa na Yehova, hakuwa nabii wala mwana wa nabii bali alikuwa mfuga kondoo na mkata (tende; tini; zeituni) za mikuyu. [si-SW uku. 148 fu. 1]
28. Utambulisho ulio sahihi wa roho takatifu lazima upatane na (mawazo ya kidini; desturi za Jumuiya ya Wakristo; Maandiko yote) yanayoelekeza kwenye roho hiyo, na huongoza kwenye uamuzi wa kiakili kwamba roho takatifu ni (mtu; sehemu ya Utatu; kani-tendaji ya Mungu). [rs-SW uku. 261 fu. 4]
29. Yoeli 2:32 lilinukuliwa na (Petro; Yohana; Paulo) kwenye (Matendo 2:40; Warumi 10:13; 1 Timotheo 2:4), ambamo hukazia umaana wa kuliitia jina la Yehova. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 4/1 uku. 20 fu. 16.]
30. Twatoa uthibitisho wa kuwa na roho ya Mungu kwa (upayukaji wa kidini wenye juhudi nyingi mno; kutetemeka na kujiviringisha; kutoa ushuhuda kwa bidii) na kwa kuonyesha matunda ya roho (tano; saba; tisa). [rs-SW uku. 262 fu. 4-uku. 263 fu. 1]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini: Kum. 18:10-12; Hos. 10:12; Sef. 2:3; Yak. 1:26, 27; 1 Yoh. 2:15-17
31. Ili ibada yetu ikubaliwe na Mungu, lazima iwe isiyochafuliwa na ulimwengu na pia itie ndani mambo yote ambayo Mungu huyaona kuwa ya muhimu. [kl-SW uku. 51 fu. 20]
32. Kwa kufanya mema katika maisha yetu ya kila siku, tutavuna fadhili zenye upendo za Yehova. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 3/15 uku. 23 maf. 2-3.]
33. Aina zote za uaguzi ni kualika uwasiliani au kupagawa na roho zisizo safi, na kujiingiza katika mambo hayo ni ukosefu mkubwa wa uaminifu kwa Yehova. [rs-SW uku. 148 fu. 1]
34. Tukiwa Wakristo wa kweli, lazima tuepuke mazoea yoyote ambayo huonyesha roho isiyo ya kimungu ya ulimwengu inayotuzunguka. [kl-SW uku. 50 fu. 17]
35. Hatuwezi kuchukua rehema ya Mungu kivivi hivi tu. [si-SW uku. 165 fu. 11]