Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/97 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1997
Huduma Yetu ya Ufalme—1997
km 12/97 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Septemba 1 hadi Desemba 22, 1997. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Hakungekuwako uovu ikiwa Mungu hangaliwapa viumbe wenye akili hiari. [rs-SW uku. 370 fu. 2]

2. Kwenye Luka 22:30, “makabila kumi na mawili ya Israeli” yana maana ileile kama katika Mathayo 19:28, ambapo linahusu zaidi ya makuhani wa cheo cha chini wa Yesu peke yao waliozaliwa kwa roho na kutia ndani wanadamu wengine wote. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 3/1 uku. 27 fu. 10; uku. 28 fu. 12.]

3. Sababu iliyofanya wanafunzi wa Yesu wastaajabie kusema kwake pamoja na mwanamke Msamaria ilikuwa kwamba mwanamke huyo alikuwa na maisha yasiyo na adili. (Yn. 4:27) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 7/15 uku. 15 fu. 1-2.]

4. Usemi “kutoka mwanzo” kwenye Yohana 6:64 huonyesha kwamba Yesu alijua wakati ambapo Yudasi alichaguliwa kuwa mtume kwamba ndiye angemsaliti Yeye. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona it-2 uku. 129 fu. 4-6.]

5. Kufurahia maisha ya familia ya Kikristo ni kuacha tu ukosefu wa adili katika ngono na kuwa na ndoa iliyosajiliwa kisheria. [uw-SW uku. 139 fu. 1]

6. Andiko la Kutoka 21:22, 23 hutusaidia kung’amua kwamba Mungu huona mtoto wa kibinadamu ambaye hajazaliwa kuwa mwenye thamani. [kl-SW uku. 128 fu. 21]

7. “Msherehekeo wa Wayahudi” unaotajwa kwenye Yohana 5:1 unarejezea Sikukuu ya Kupitwa ya 31 W.K. [si-SW uku. 194 fu. 8]

8. Mkristo mwenzetu akitukosea, ingekuwa vibaya kumwondoa mkosaji maishani mwetu, tukiepuka uhusiano wote naye. [uw-SW uku. 134 fu. 7]

9. Sisi sote twahitaji shauri na nidhamu. [uw-SW uku. 130 fu. 12]

10. Haidhuru mamlaka za serikali zaonwa kuwa ni zenye haki au si zenye haki, Wakristo wa kweli wapaswa kuziendea ili kusajili ndoa zao ifaavyo. [kl-SW uku. 122 fu. 11]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Kwa kupatana na kielelezo cha Wakristo wa Efeso wa karne ya kwanza, ni hatua gani moja inayohitajika ambayo ni lazima ichukuliwe ili kukinza roho waovu? (Mdo. 19:19) [kl-SW uku. 114 fu. 14]

12. Eleza kwa nini matumizi ya usemi “msaidizi [“kikamilisho,” NW],” kwenye Mwanzo 2:18, hayashushi wanawake. [rs-SW uku. 401 fu. 4]

13. Kwa nini Yesu alikataa kujihusisha katika mabishano ya urithi? (Luka 12:13, 14) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 4/1 uku. 28.]

14. Wanafunzi walikuwa hawajui nini walipomwuliza Yesu kama alikuwa anarudishia Israeli Ufalme, kama ilivyorekodiwa kwenye Matendo 1:6? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 6/1 uku. 11 fu. 4.]

15. Taja mambo mawili ambayo yanaweza kuchangia ndoa yenye kudumu. [uw-SW uku. 140 fu. 4]

16. Kwa nini mwanamke Mkristo huvaa kifuniko cha kichwa katika pindi fulani-fulani? [rs-SW uku. 404 fu. 1]

17. Kwa nini Tafsiri ya Ulimwengu Mpya husema “Neno alikuwa mungu” na si “Neno alikuwa Mungu,” kama zinavyofanya tafsiri nyinginezo kwenye Yohana 1:1? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona rs-SW uku. 431 fu. 4.]

18. Kulingana na kitabu cha Ufunuo, mwisho wa “wale wanaozoea kuwasiliana na roho” utakuwa nini wasipotubu na kubadili njia zao? [kl-SW uku. 111 fu. 8]

19. Kwa kuwa Yesu alikuwa mwanadamu mkamilifu naye alikubali daraka lake akiwa Mwalimu, kwa nini hakukubali kuitwa “Mwalimu Mwema”? (Luka 18:18, 19) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 3/1 uku. 15 fu. 7.]

20. Ni nini kilichokuwa kipya kuhusu amri iliyoandikwa kwenye Yohana 13:34? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 2/1 uku. 21 fu. 5-6.]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Tukijua kwamba ndugu yetu ana jambo dhidi yetu, yataka _________________________ ukiandamana na ____________________________ ili kuchukua hatua ya kwanza na kujitahidi kurudisha ____________________________ . [uw-SW uku. 135 fu. 10]

22. Zile “mina kumi” zinawakilisha _________________________ ambazo wanafunzi wa kuzaliwa kwa roho wangezitumia kwa manufaa katika kutokeza _________________________ zaidi wa Ufalme wa kimbingu. (Luka 19:13) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 10/1 uku. 8.]

23. Mashtaka matatu yasiyo ya kweli ambayo Wayahudi walimshtaki Yesu kwa Pilato, gavana Mroma wa Yudea, yalitia ndani kupindua _________________________ , kukataza watu wasimlipe _________________________ , na kusema Yeye Mwenyewe alikuwa _________________________ . (Luka 23:2) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 12/1 uku. 9 fu. 1.]

24. Wakristo wa kweli hawasherehekei Krismasi au sikukuu nyingine inayotegemea imani zisizo za kweli za kidini kwa sababu wao humpa Yehova _________________________ ; wao pia hawaadhimishi sikukuu zinazofanya wanadamu wenye dhambi au mataifa _________________________ . [kl-SW uku. 126 fu. 16]

25. Tukiwa wanafunzi wa Biblia, twapaswa kujifunza kutumia fahirisi zinazopatikana ili kufanya utafiti wa habari, hatupaswi kutazamia jibu _________________________ au _________________________ kwa kila swali, na twapaswa kufanya _________________________ ambayo yanaonyesha upendo wetu kwa _________________________ na washiriki wa familia yetu. [uw-SW uku. 144 fu. 13]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Kulingana na mtume Petro, (fadhili; upendo, subira) ya Yehova imeendelea hadi siku yetu ili kutupatia fursa ya kuonyesha kwamba sisi (ni wenye kutubu; ni waaminifu; ni watiifu). (2 Pet. 3:9) [rs-SW uku. 371 fu. 2]

27. Kweli inayoweka watu huru ni kweli kuhusu (sayansi; dini isiyo ya kweli; Yesu Kristo) kwa sababu ni kupitia hiyo tu tunapoweza kuwa huru na (mafundisho yasiyo ya kweli; propaganda ya kilimwengu; dhambi inayoleta kifo). (Yn. 8:12-36) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 5/1 uku. 9 fu. 5.]

28. Kuishi kwetu maisha ya kimungu kwatuhakikishia kwamba (sikuzote tutatendewa vizuri na wengine; tutafurahia wingi wa vitu vya kimwili sasa; tutakuwa na kibali cha Mungu kwa sababu tunafanya yaliyo sawa). [kl-SW uku. 118 fu. 2]

29. Yesu alipomwuliza mtume Petro, “Je, wanipenda mimi kuliko hawa?,” Alikuwa anamwuliza Petro kama alimpenda Yeye kuliko (alivyowapenda wale wanafunzi wengine; vile hawa wanafunzi wengine walivyompenda Yesu; alivyopenda vitu hivi, kama wale samaki). (Yn. 21:15) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 11/1 uku. 31 fu. 9.]

30. Ni katika kielelezo cha (“mzabibu wa kweli”; “mchungaji mwema”; “kondoo na mbuzi”) ambapo Yesu anajulisha si muungano wa ajabu tu uliopo kati ya wafuasi wake wa kweli na yeye mwenyewe bali pia na Baba yake. (Yn. 15:1) [si-SW uku. 198 fu. 32]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Kut. 31:12, 13; Mt. 5:14-16; Luka 9:60, 62; 13:4, 5; Mit. 3:9, 10

31. Yesu alibisha dhidi ya kusababu kwa kinadhariajali, akirejezea msiba uliojulikana sana na wasikilizaji wake na kwamba ni dhahiri aliona wakati na tukio lisilotazamiwa kuwa sababu ya huo msiba. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 9/1 uku. 5 fu. 5.]

32. Sheria ya Kimusa haikukusudiwa kamwe iwahusu wanadamu wote. [uw-SW uku. 147 fu. 5]

33. Ujitoaji wa akili moja unahitajiwa ili kuingia katika Ufalme. [si-SW uku. 192 fu. 32]

34. Yehova atatubariki tukitumia wakati, nishati na mali nyinginezo zetu, kutia na fedha zetu ili kutegemeza ibada ya kweli. [kl-SW uku. 121 fu. 8]

35. Wale ambao ni Wakristo lazima wawe mashahidi watendaji kwa ulimwengu kuhusu jina la Mungu na makusudi yake. [rs-SW uku. 361 fu. 4]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki