Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Januari 5 hadi Aprili 20, 1998. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Kwenye Matendo 15:29, lile elezo “Afya njema kwenu” lilikuwa ahadi likimaanisha, ‘Mkijiepusha na damu na uasherati, mtakuwa na afya bora.’ [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 6/15 uku. 9 fu. 7 kzch.]
2. Hangaiko la kina kirefu kuhusu hali njema ya kiroho ya Wakristo Wakorintho lilimsukuma Paulo kuandika barua yake ya kwanza kwao akiwa katika safari yake ya pili ya umishonari. [si-SW uku. 210 fu. 3]
3. Neno “usimoni,” ambalo latokana na tukio lililorekodiwa kwenye Matendo 8:9-24, hurejezea zoea la ufundi wa mizungu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 6/1 uku. 17 fu. 8.]
4. Kwenye Waroma 8:6, 7, “mwili” hurejezea hali yetu ya dhambi tukiwa wanadamu wasio wakamilifu wenye mielekeo ya dhambi iliyorithiwa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 3/1 uku. 21 fu. 4.]
5. Kupatana na Waefeso 5:33, mke kuwa mwenye staha yenye kina kirefu kwa mume wake hakumaanishi kwamba hawezi kueleza maoni yake, hasa ikiwa jambo fulani lamsumbua. [kl-SW uku. 144 fu. 12-13]
6. Kama vile kusudi la Mungu la kuwaleta Wasio Wayahudi katika kutaniko halikueleweka wazi hadi mitume walipoona yale yaliyokuwa yakitukia hasa katika kutimizwa kwa unabii, Mashahidi wa Yehova hukubali kwamba uelewevu wao wa mambo fulani umepata marekebisho kadiri ambavyo Mungu ameandaa mnurusho wa hatua kwa hatua. [jv-SW uku. 629 fu. 3-4]
7. Kwenye Matendo 20:20, usemi “nyumba hadi nyumba” hurejezea tu ziara za uchungaji nyumbani mwa waabudu wenzi kwa sababu muktadha waonyesha Paulo alikuwa akihutubia wanaume wazee wa kutaniko. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 1/15 uku. 11 fu. 5.]
8. Tukizoeza moyo wetu kuthamini mambo ya kiroho, kusali ili roho ya Mungu itusaidie katika jambo hilo, basi tutaepuka “kuweka akili juu ya mwili.” (Rom. 8:6, 7) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 3/1 uku. 21 fu. 5.]
Jibu maswali yafuatayo:
9. Ni simulizi gani katika kitabu cha Matendo linaloonyesha kwamba kuwa tu na Neno la Mungu na kulisoma kibinafsi hakutoshi ili kupata ujuzi sahihi unaomweka mtu kwenye barabara iongozayo kwenye uhai? [Usomaji wa Biblia; ona w91-SW 9/1 uku. 19 fu. 16.]
10. Ni nini kinachoonyeshwa na uhakika wa kwamba Paulo aliandika: “Mamlaka zilizopo zimesimama zikiwa zimewekwa na Mungu”? (Rom. 13:1) [kl-SW uku. 131 fu. 7]
11. Kwenye Matendo 11:26, kwa nini Tafsiri ya Ulimwengu Mpya hutumia usemi “kwa uongozi wa kimungu waliitwa Wakristo,” ilhali tafsiri nyingine za Biblia hazitii wazo hilo la “uongozi wa kimungu”? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 6/1 uku. 19 fu. 19.]
12. Ni usadikisho gani wa Mashahidi wa Yehova ambao huwachochea kuwa wahubiri na wagawanyaji wa Biblia wenye bidii? [jv-SW uku. 603 fu. 3]
13. Ni funzo la kibinafsi la aina gani linalotiwa moyo kwenye Matendo 17:11? [si-SW uku. 205 fu. 38]
14. Katika barua yake kwa Wakristo katika Roma, Paulo alithibitisha sana nini kuhusu Wayahudi na Wasio Wayahudi? [si-SW uku. 206 fu. 2]
15. Kulingana na Waroma 12:2, ni kwa kadiri gani nyutu za Wakristo hubadilishwa kwa nguvu ya Neno la Mungu? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 4/1 uku. 16 fu. 3.]
16. Ni nini ile “siri takatifu” iliyotajwa na Paulo katika Waroma 11:25? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w84-SW 1/15 uku. 10 fu. 16.]
17. Kwa nini kutaniko la Kikristo lina haki ya kuwatenga watenda-dhambi wasiotubu? (1 Kor. 5:11, 13) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona g96-SW 9/8 uku. 27 fu. 3-4.]
18. Kurundika makaa-mawe yenye moto juu ya kichwa cha adui kutasaidiaje kushinda ovu? (Rom. 12:20, 21) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona g87-SW 2/8 uku. 6 fu. 4.]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
19. Filipo alieleza towashi Mwethiopia jinsi ambavyo unabii wa _________________________ ulikuwa umetimizwa, na alipoelimishwa, kwa unyenyekevu yeye aliomba _________________________ . (Mdo. 8:28-35) [si-SW uku. 204 fu. 33]
20. Wakati habari ya _________________________ ilipokuwa ikijadiliwa, _________________________ alitegemeza uamuzi wake kwa kusema: “Pamoja na hili maneno ya Manabii yapatana, kama vile imeandikwa.” (Mdo. 15:15-18) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona si-SW uku. 204 fu. 33.]
21. Kulingana na kielezi cha Paulo cha mzeituni wa ufananisho katika Waroma sura ya 11, kama vile makabila 12 ya Israeli yalivyotokana na Abrahamu kupitia Isaka, ndivyo yale makabila 12 ya ufananisho ya _____________________________ yanavyotokana na _____________________________ kupitia _____________________________ . [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w84-SW 1/15 uku. 10 fu. 15.]
22. Ilikuwa katika Julai 1917, baada ya kifo cha Russell, kwamba Watch Tower Society ilitoa kitabu _________________________ , ufafanuzi juu ya _________________________ na _________________________ pamoja na _________________________ . [jv-SW uku. 647 fu. 2]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
23. Kwa hotuba yake katika Matendo sura ya 17, Paulo athibitisha kwa busara (enzi kuu ya; uadilifu wa; upendo wa) Mungu aliye hai. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona si-SW uku. 204 fu. 37.]
24. (Paulo; Petro; Luka) aliwapongeza kwa uchangamfu watu wa (Beroya; Makedonia; Yerusalemu) kwa sababu ya bidii yao ya kuchunguza Maandiko. (Mdo. 17:11) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 5/1 uku. 14 fu. 3.]
25. Uwongo, au jambo lisilo la kweli, linalotajwa kwenye Waroma 1:25 larejezea (ibada ya sanamu; mazoea yasiyo safi ya ngono; zoea la kusema uwongo). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 11/15 uku. 6 fu. 6.]
26. Katika 1878, C. T. Russell na washiriki wake walikabiliwa na mtihani mkubwa wa imani yao na uaminifu-mshikamanifu wao kwa Neno la Mungu. Suala lilikuwa juu ya (utambulisho wa “mtumwa mwaminifu na mwenye busara”; kuwapo kwa Yesu kusikoonekana; thamani ya dhabihu ya mwili na damu ya Yesu). [jv-SW uku. 619 fu. 3]
27. Paulo aliandika barua yake ya kwanza kwa Wakorintho akiwa (Roma; Efeso; Korintho) wapata mwaka wa (52; 55; 56) W.K. [si-SW uku. 210 fu. 3]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Zab. 73:38; Mit. 24:3; Isa. 65:13; Mdo. 10:34, 35; 2 Kor. 12:7-9
28. Tukiwa watumishi wa Yehova, twapaswa kuwaona watu wa vikundi vyote vya jamii kama awaonavyo yeye. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 5/15 uku. 16 fu. 6.]
29. Biblia huandaa kanuni zilizo kama vyombo ambavyo husaidia mtu kujenga familia yenye furaha. [kl-SW uku. 140 fu. 3]
30. Wale wanaomkaribia Yehova huwa na furaha ya kweli na amani ya akilini. [kl-SW uku. 151 fu. 3]
31. Muda wote wa historia, Yehova amewatolea watu wake chakula cha kiroho wakiwa kikundi. [kl-SW uku. 162 fu. 6]
32. Huenda Yehova akaruhusu hali fulani yenye kujaribu iendelee kwa muda, lakini yeye hujibu sala na ajua wakati bora zaidi wa kufanya hivyo. [kl-SW uku. 156 fu. 15]