Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/99 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1999
Huduma Yetu ya Ufalme—1999
km 8/99 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Mei 3 hadi Agosti 23, 1999. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu ya maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Wazazi hawahitaji kuacha kanuni za Biblia ili washughulike kwa kiasi na watoto wao. [fy-SW uku. 108 fu. 14]

2. Kichwa cha Biblia nzima ni kutetewa kwa Yehova kupitia Ufalme unaotawalwa na “uzao [“mbegu,” NW]” ulioahidiwa. (Mwa. 3:15) [si-SW uku. 17 fu. 30]

3. Hakuna uthibitisho mwingi wa kiakiolojia na mwingineo wa nje unaoshuhudia usahihi wa matukio yaliyorekodiwa katika Kutoka. [si-SW uku. 20 fu. 4]

4. Wale walio katika ufukara kabisa hawawezi kuchanga kifedha ili kuendeleza masilahi za Ufalme. [w97-SW 9/15 uku. 5 fu. 7]

5. Kuwalipa wazazi na babu na nyanya malipo yapasayo ni sehemu ya ibada yetu kwa Yehova. (1 Tim. 5:4) [w97-SW 9/1 uku. 4 fu. 1-2]

6. Ushikaji wa Sabato hapo awali ulikuwa ishara kati ya Yehova na mataifa yote. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona rs-SW uku. 269 fu. 2.]

7. Mtoto anapokua mkubwa vya kutosha kuanza kufanya maamuzi yake mwenyewe, yeye huwa na kiasi kilichoongezeka cha daraka kwa matendo yake, hasa kuhusiana na sheria ya kimungu. (Rom. 14:12) [fy-SW uku. 134-135 fu. 17]

8. Musa aliandika kitabu cha Mambo ya Walawi mwaka wa 1513 K.W.K. [si-SW uku. 25 fu. 3-4]

9. Maneno ya Yesu yaliyorekodiwa kwenye Luka 21:20, 21 yalitimizwa mwaka wa 66 W.K. majeshi ya Waroma yakiwa chini ya Jenerali Tito yalipojiondoa Yerusalemu. [w97-SW 4/1 uku. 5 fu. 4-5]

10. Fundisho la Epikurasi lilikuwa hatari kwa Wakristo kwa sababu lilitegemea mtazamo wake wa ukosefu wa imani, ambao wafafanuliwa kwenye 1 Wakorintho 15:32. [w97-SW 11/1 uku. 24 fu. 4]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Twajifunza somo gani kutokana na katazo la kutokula mafuta lililoandikwa kwenye Mambo ya Walawi 3:17? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w84-SW 9/1 uku. 21 fu. 7.]

12. Kwa nini Yehova amemruhusu Shetani Ibilisi awepo? (Kut. 9:15, 16) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 3/15 uku. 10 fu. 14.]

13. Mshiriki wa familia anapokabili ugonjwa mbaya sana, ni hatua gani za kwanza ambazo familia inapaswa kuchukua ili kuweka mambo ya kutangulizwa? (Mit. 15:22) [fy-SW uku. 122 fu. 14]

14. Taifa la Israeli lilikuwa “ufalme wa makuhani” katika maana gani? (Kut. 19:6) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 7/1 uku. 16 fu. 8.]

15. Kuna tofauti gani kati ya jicho “sahili” na jicho “bovu”? (Mt. 6:22, 23) [w97-SW 10/1 uku. 26 fu. 5]

16. Daudi angeweza kusemwaje kuwa alitembea “kwa uaminifu-maadili wa moyo na unyoofu” ingawa alifanya makosa? (1 Fal. 9:4, NW) [w97-SW 5/1 uku. 5 fu. 2]

17. Ni mapendeleo gani ya siku ya kisasa yanayoonyeshwa kimbele na Waisraeli kufanya ‘vivyo hivyo’ kuhusu tabenakulo? (Kut. 39:32) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 12/15 uku. 13 fu. 9.]

18. Ni nini kinachoonyeshwa na uhakika wa kwamba Yehova alijifunua mwenyewe kuwa “Mimi nitathibitika kuwa kile ambacho mimi nitathibitika kuwa”? (Kut. 3:14) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 3/1 uku. 10 fu. 6.]

19. Ni somo gani twaweza kujifunza kutokana na kisa juu ya Nadabu na Abihu kilichorekodiwa kwenye Mambo ya Walawi 10:1, 2? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w84-SW 9/1 uku. 22 fu. 1.]

20. Chini ya Sheria ya Kimusa, kwa sababu gani kuzaa mtoto kulimfanya mwanamke “najisi”? (Law. 12:2, 5) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w84-SW 9/1 uku. 22 fu. 3.]

Toa neno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Ijapokuwa hakuna ponyo la kimuujiza la upweke, mzazi aliye peke yake aweza kuuvumilia kwa nguvu kutoka kwa _________________________ , ambayo yapatikana kupitia kudumu katika _________________________ . (1 Tim. 5:5) [fy-SW uku. 112 fu. 21]

22. Jambo lenye kuhuzunisha katika maisha ya mtu huenda likasababishwa na _________________________ au kwa sababu ya hali yetu wenyewe ya _________________________. [w97-SW 5/15 uku. 22 fu. 7]

23. Kitabu cha Kutoka humfafanua Yehova kuwa _________________________ mkuu na _________________________ na _________________________ wa makusudi yake mazuri sana. [si-SW uku. 24 fu. 26]

24. Kimsingi ni jinsi tutendavyo _________________________, wala si jinsi tutendavyo _________________________, ndivyo hufunua vile tulivyo kindani. [w97-SW 10/15 uku. 29 fu. 3]

25. Ikiwa misherehekeo ya mavuno ina vidokezo vya _________________________ au vya _________________________, Wakristo wa kweli waweza kuepuka kutompendeza Yehova kwa kukataa _________________________ kokote katika ibada iliyochafuliwa. [w97-SW 9/15 uku. 9 fu. 6]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Ile “miaka mia nne” ya kuteswa kwa mbegu ya Abrahamu, ilianza wakati Ishmaeli alipomfanyia mzaha Isaka katika mwaka wa (1943; 1919; 1913) K.W.K. na kuisha kwa kukombolewa kutoka Misri mwaka wa (1543; 1519; 1513) K.W.K. (Mwa. 15:13) [si-SW uku. 17 fu. 31]

27. Iwe familia yakabiliana kwa mafanikio na ugonjwa mbaya sana au sivyo yategemea kwa kadiri kubwa (usalama wa kifedha wa; mtazamo wa; bima ya) washiriki wayo. (Mit. 17:22) [fy-SW uku. 120 fu. 10]

28. Yule asemaye moyoni mwake “hakuna Mungu [“Yehova,” NW]” anaitwa “mpumbavu” kwa sababu huyu ni (mpungukiwa kiadili; asiye na elimu; amekosa uwezo wa kufikiri). (Zab. 14:1) [w97-SW 10/1 uku. 6 fu. 8]

29. Adamu na Hawa walipoasi, jambo la maana zaidi walilopoteza lilikuwa (ukamilifu; uhusiano na Mungu; makao ya kibustani), jambo lililokuwa ufunguo wa furaha yao. [w97-SW 10/15 uku. 6 fu. 2]

30. Kitabu cha (Mwanzo; Kutoka; Mambo ya Walawi) hutaja takwa la utakatifu mara nyingi zaidi ya kitabu kinginecho cha Biblia. [si-SW uku. 26 fu. 9]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Kut. 5:2; Kut. 21:29; Mit. 1:8; Gal. 5:20; Yak. 1:14, 15

31. Mtu yeyote anayedai kuwa Mkristo ambaye kwa kurudia-rudia na bila kutubu, hushindwa na hasira za ghafula zenye jeuri labda kutia ndani kutenda vibaya kimwili mwenzi au watoto, aweza kutengwa na ushirika. [fy-SW uku. 150 fu. 23]

32. Jinsi tunavyotenda huanza na jinsi tunavyofikiri. [fy-SW uku. 148 fu. 18]

33. Yehova Mungu hutahayarisha wale wote ambao hukataa kwa ukaidi kutambua Uungu wake. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 12/15 uku. 13 fu. 18.]

34. Ijapokuwa Biblia humpa baba daraka la msingi la kufundisha watoto wake, mama pia ana fungu la maana la kutimiza. [fy-SW uku. 133 fu. 12]

35. Sheria haikuruhusu ulegevu uwe dai la kuomba rehema mtu alipouawa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 11/15 uku. 11 fu. 5.]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki