Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Septemba 6 hadi Desemba 20, 1999. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu ya maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Yehova ameruhusu utawala wa kujitegemea wa kibinadamu ili athibitishe kwamba njia Yake ya kutawala sikuzote huwa sawa na ya haki. (Kum. 32:4; Ayu. 34:10-12; Yer. 10:23) [w97-SW 2/15 uku. 5 fu. 3]
2. Biblia huonyesha kwamba Mungu hulaumu kulalamika kwa namna zote. [w97-SW 12/1 uku. 30 fu. 3-4]
3. Wazazi hudumisha uhusiano wao na watoto wao waliofunga ndoa wakitambua kanuni za kimungu za ukichwa na utaratibu mzuri kwa kuweka mambo katika mahali pake pafaapo. (Mwa. 2:24; 1 Kor. 11:3; 14:33, 40) [fy-SW uku. 164 fu. 6]
4. Marko 6:31-34 huonyesha kwamba Yesu alisikitikia umati kwa sababu tu ya ugonjwa na umaskini wao. [w97-SW 12/15 uku. 29 fu. 1]
5. Ikiwa Mkristo wa jamii ya kondoo wengine hawezi kuhudhuria Ukumbusho wa kifo cha Yesu, apaswa kuuadhimisha mwezi mmoja baadaye kupatana na kanuni iliyoandikwa kwenye Hesabu 9:10, 11. (Yn. 10:16) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 2/1 uku. 31 fu. 9.]
6. Ingawa wazakuu Wakristo hawachukui daraka la baba na mama la kukazia kikiki kweli za Biblia katika watoto wao, wazakuu wanaweza kukamilisha daraka hilo kwa ajili ya usitawi wa kiroho wa mtoto. (Kum. 6:7; 2 Tim. 1:5; 3:14, 15) [fy-SW uku. 168 fu. 15]
7. Mithali 6:30 huonyesha kwamba kuiba kwaweza kutolewa udhuru au kuwa jambo la haki kwa sababu ya hali fulani. [g97-SW 11/8 uku. 19 fu. 2]
8. Katika 1530, William Tyndale alikuwa mtu wa kwanza kutumia jina la Mungu, Yehova, katika tafsiri ya Kiingereza ya Maandiko ya Kiebrania. [w97-SW 9/15 uku. 28 fu. 3]
9. Leo, jiji la makimbilio la ufananisho ni uandalizi wa Mungu wa kutulinda kutoka katika kifo kwa kuvunja amri zake kuhusu utakaso wa damu. (Hes. 35:11) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 11/15 uku. 17 fu. 8.]
10. Jina Kumbukumbu la Torati, linalomaanisha “Sheria ya Pili,” linafaa kwa sababu kitabu hiki cha Biblia ni kukaririwa tu kwa Sheria. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona si-SW uku. 36 fu. 4.]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Ni nini kinachofananishwa na mikate miwili iliyotiwa chachu iliyotolewa na kuhani wa cheo cha juu wakati wa Msherehekeo wa Pentekoste? (Law. 23:15-17) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w98-SW 3/1 uku. 13 fu. 21.]
12. Yubile ya Kikristo ilianza lini, na ilileta uhuru wa aina gani wakati huo? (Law. 25:10) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 5/15 uku. 24 fu. 14.]
13. Kulingana na masimulizi yaliyo katika kitabu cha Hesabu, kuokoka kwategemea mambo gani matatu? [si-SW uku. 30 fu. 1]
14. Musa alikuwa kielelezo kizuri kwa njia gani katika kuonyesha kwamba hakuwa na roho ya wivu? (Hes. 11:29) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 9/15 uku. 18 fu. 11.]
15. Kisa cha Kora, Dathani, na Abiramu chaonyeshaje kwamba sikuzote kuona hakuongozi kwenye kuamini? [w97-SW 3/15 uku. 4 fu. 2]
16. Ni njia zipi mbili za kuheshimu wazazi wazee-wazee zinazokaziwa kwenye Mathayo 15:3-6 na 1 Timotheo 5:4? [fy-SW uku. 173-175 fu. 2-5]
17. Ni somo gani la maana linalokaziwa kwenye Hesabu 26:64, 65? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona g95-SW 8/8 uku. 10-11 fu. 5-8.]
18. Kielelezo cha Finehasi kinatusaidiaje kuelewa kinachotiwa ndani ya wakfu kwa Yehova? (Hes. 25:11) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 3/1 uku. 16 fu. 12-13.]
19. Mtu aliye katika jiji la makimbilio la ufananisho anaweza ‘kwendaje kwenye ukingo’ wa jiji hilo? (Hes. 35:26) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 11/15 uku. 20 fu. 20.]
20. Ni katika njia gani Codex Sinaiticus ilikuwa yenye manufaa katika kutafsiri Biblia? [w97-SW 10/15 uku. 11 fu. 2]
Toa neno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Yehova ameruhusu uovu uwepo ili kuthibitisha mara moja kwa wakati wote kweli ya msingi kwamba yeye peke yake ndiye _________________________ na kwamba _________________________ sheria zake ni kwa lazima kwa ajili ya amani na furaha yenye kuendelea ya viumbe wake wote. (Zab. 1:1-3; Mit. 3:5, 6; Mhu. 8:9) [w97-SW 2/15 uku. 5 fu. 4]
22. Kitabu cha Mambo ya Walawi ni chenye kutokeza katika kukazia _________________________ wa damu, kikionyesha kwamba matumizi yanayoruhusiwa pekee ya damu ni _________________________ . [si-SW uku. 29 fu. 33]
23. Kupatana na Zaburi 144:15b, furaha ya kweli ni hali ya moyoni, inayotegemea _________________________ ya kweli na _________________________ mzuri pamoja na Yehova. [w97-SW 3/15 uku. 23 fu. 7]
24. Biblia iliyotokana na tafsiri ya Biblia ya Kiebrania hadi Kigiriki cha kawaida, iliyomalizwa wapata mwaka wa 150 K.W.K., ilikuja kujulikana kuwa _________________________ ; tafsiri ya Jerome ya Biblia hiyo katika Kilatini ilikuja kujulikana kuwa _________________________ , _________________________ , ikimalizwa wapata mwaka wa 400 W.K. [w97-SW 8/15 uku. 9 fu. 1; uku. 10 fu. 4]
25. Akitumia masimulizi kuhusu Balaamu na Kora kama ilivyorekodiwa katika kitabu cha Hesabu, Yuda alionya Wakristo wajilinde dhidi ya _________________________ na _________________________ . [si-SW uku. 35 fu. 35]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Mara moja kwa mwaka, kwenye (Msherehekeo wa Vibanda; Siku ya Kufunikwa; Sikukuu ya Kupitwa), taifa lote la Israeli, kutia ndani wakazi wageni ambao walimwabudu Yehova, walipaswa (kuacha kazi zote; kulipa sehemu ya kumi; kutoa mazao ya kwanza) na kufunga. (Law. 16:29-31) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 7/1 uku. 10 fu. 12.]
27. Mojawapo ya miradi ya Halmashauri ya Tafsiri ya Biblia ya Ulimwengu Mpya ulikuwa kutokeza tafsiri (ya neno kwa neno kwa kadiri iwezekanavyo; ya kusimulia kwa maneno mengine lugha za awali; ya kupatana na uelewevu hususa wa kimafundisho) ili kumpa msomaji ladha ya lugha za awali na ule utaratibu wa mawazo unaohusianishwa. [w97-SW 10/15 uku. 11 fu. 5]
28. Kulingana na Waebrania 13:19, sala zenye kudumu za waamini wenzetu zaweza kubadili hali kuhusu (kile anachoruhusu Mungu; wakati Mungu atakapotenda; jinsi Mungu atakavyoongoza mambo). [w97-SW 4/15 uku. 6 fu. 1]
29. ‘Nyuzi za rangi ya samawi katika ncha za nguo’ za Waisraeli zilihitajiwa ili kuwa (mapambo matakatifu; ishara ya kiasi; kikumbusha cha kuwa tofauti na ulimwengu wakiwa watu wa Yehova). (Hes. 15:38, 39) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w84-SW 3/15 uku. 18 fu. 16.]
30. Wakati uliohusishwa wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati ni (miezi miwili; mwaka mmoja; miaka miwili), na uandikaji wake ulikamilishwa mapema mwaka wa (1513; 1473; 1467) K.W.K. [si-SW uku. 36 fu. 6]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Hes. 16:41, 49; Mt. 19:9; Luka 2:36-38; Kol. 2:8; 3:14
31. Kujinyima sana raha na anasa hakuongozi kwenye utakatifu au hekima. [g97-SW 10/8 uku. 21 fu. 3]
32. Uasherati ndio msingi pekee wa Kimaandiko wa talaka kukiwa na uwezekano wa kuoa au kuolewa tena. [fy-SW uku. 158-159 fu. 15]
33. Kuwa mtendaji sana katika mambo ya kitheokrasi, hata katika miaka ya baadaye, kwaweza kumsaidia mtu akabiliane na kifo cha mwenzi wa ndoa. [fy-SW uku. 170-171 fu. 21]
34. Kutafuta lawama katika njia ya Yehova ya kutekeleza haki kupitia watumishi wake waliowekwa kwaweza kuleta matokeo yenye kuleta msiba. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 6/15 uku. 21 fu. 13.]
35. Upendo usio na ubinafsi huwaunganisha wenzi wa ndoa pamoja na kuwafanya watake kunufaishana zaidi na kunufaisha watoto wao. [fy-SW uku. 187 fu. 11]