Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/99 uku. 7
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1999
Huduma Yetu ya Ufalme—1999
km 12/99 uku. 7

Matangazo

◼ Toleo la fasihi la Desemba: Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele pamoja na Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Januari: Kitabu chochote chenye kurasa 192 kilichochapishwa kabla ya 1986 ambacho huenda kutaniko likawa nacho akibani. Makutaniko ambayo hayana vitabu hivyo yaweza kutoa Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? au Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani, au vichapo vingine vyovyote vilivyo kutanikoni. Februari: Siri ya Kupata Furaha ya Familia. Machi: Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Jitihada ya pekee itafanywa ili kuanzisha mafunzo ya Biblia ya nyumbani.

◼ Makutaniko yapaswa kuanza kuomba mabuku yaliyojalidiwa ya The Watchtower na Awake! ya 1998 katika ombi lao la fasihi la Desemba. Mabuku yaliyojalidiwa yatapatikana katika Kichina, Kifaransa, na Kiingereza. Mabuku yaliyojalidiwa yatakuwa katika sehemu ya “Vitatumwa Vikipatikana” katika orodha ya upakizi ya kutaniko mpaka yapatikane na upelekaji ufanywe. Mabuku yaliyojalidiwa ni bidhaa za kuagizwa kipekee.

◼ Mwangalizi-msimamizi au mtu fulani aliyewekwa naye apaswa kukagua hesabu ya kutaniko Desemba 1 au upesi iwezekanavyo baada ya hapo. Jambo hili lifanywapo, tangazieni kutaniko baada ya ripoti ya hesabu itakayofuata kusomwa.

◼ Ukumbusho wa mwaka wa 2001 utafanywa Jumapili, Aprili 8, baada ya jua kushuka. Taarifa hii ya mapema imetolewa ili akina ndugu waweze kukodi au kufanya maagano ya lazima kwa majumba yanayopatikana mahali ambako kuna makutaniko kadhaa yanayotumia Jumba la Ufalme na majengo mengine lazima yatafutwe. Wazee wanapaswa kuwa na mapatano pamoja na wasimamizi wa jengo wakihakikisha kwamba hakutakuwa na usumbufu kutokana na utendaji mwingine katika jengo hilo ili kwamba mwadhimisho wa Ukumbusho uweze kuendelea kwa njia ya amani na kwa utaratibu. Kwa sababu ya umuhimu wa tukio hili, baraza la wazee linapompa mgawo msemaji wa Ukumbusho, lapaswa kuteua mmoja wa wazee mwenye kustahili zaidi badala ya kupokezana zamu tu au kutumia ndugu yuleyule kila mwaka. Isipokuwa tu kuwe na mzee mwenye uwezo kati ya watiwa-mafuta anayeweza kutoa hotuba hiyo.

◼ Kaseti Zinazopatikana:

Kumsikiliza Mwalimu Mkuu—Kiingereza, Kiswahili

Mungu Anataka Tufanye Nini?—Kiingereza

Yehova Huokoa Wale Wanaoita Juu ya Jina Lake—Kiingereza, Kiswahili

Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi—Kiingereza

Doing God’s Will With Zeal—Kiingereza

Doing What Is Right in Jehovah’s Eyes—Kiingereza

Families—Make Daily Bible Reading Your Way of Life!—Kiingereza

Jehovah’s Judgment Against Law-Defying People—Kiingereza

Jehovah’s Name to Be Declared in All the Earth—Kiingereza

Keep Your Eye Simple—Kiingereza

Preserving Life in Time of Famine—Kiingereza

Why Respect Theocratic Arrangements?—Kiingereza

◼ Vidiokaseti Zinazopatikana:

Siri ya Kupata Furaha ya Familia—Lugha ya Ishara ya Marekani

“Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya”—Lugha ya Ishara ya Marekani

Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele—Lugha ya Ishara ya Marekani

Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani—Lugha ya Ishara ya Marekani

Jehovah’s Witnesses—The Organization Behind the Name—Lugha ya Ishara ya Marekani, Kiingereza

Noah—He Walked With God—Kiingereza

The Bible—Accurate History, Reliable Prophecy—Lugha ya Ishara ya Marekani, Kiingereza

The Bible—Its Power in Your Life—Kiingereza

The Bible—Mankind’s Oldest Modern Book—Kiingereza

The New World Society in Action—Kiingereza

United by Divine Teaching—Kiingereza

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki