Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Mei 1 hadi Agosti 21, 2000. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Jibu la Gideoni kwa shambulio la maneno lisilo la haki la wanaume Waefraimu lilionyesha upole na unyenyekevu na hivyo kukengeusha uchambuzi wao usio wa haki na kudumisha amani. (Amu. 8:1-3) [Usomaji wa Biblia kila juma] Kweli.
2. Ijapokuwa Manoa alisema “tumemwona Mungu,” kwa kweli yeye na mke wake walimwona mwakilishi mnenaji wa Mungu na si Yehova mwenyewe. (Amu. 13:22) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 5/15 uku. 23 fu. 3.] Kweli.
3. Kwenye Waamuzi 5:31 (Biblia Habari Njema), usemi “rafiki zako” hurejezea kiunabii wale warithi wa Ufalme 144,000. [si-SW uku. 50 fu. 28] Kweli.
4. Hakuna visehemu-sehemu vya kitabu cha Ruthu vilivyopatikana miongoni mwa Hati-Kunjo za Bahari ya Chumvi. [si-SW uku. 51 fu. 3] Si Kweli. Visehemu-sehemu vya kitabu cha Ruthu vilipatikana miongoni mwa Hati-Kunjo za Bahari ya Chumvi.
5. Waamuzi 21:25 hurejezea kipindi cha wakati ambapo Yehova aliliacha taifa la Israeli bila mtu wa kuliongoza hata kidogo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 6/15 uku. 22 fu. 16.] Kweli. Kila jiji katika Israeli lilikuwa na wanaume wazee ambao wangeandaa msaada mkomavu kwa maswali na matatizo. Kwa kuongezea, makuhani wa Kilawi walitenda wakiwa kani ya mema kwa kuelimisha watu sheria za Mungu. Hasa mambo magumu yalipotokea, kuhani mkuu angetafuta shauri kwa Mungu kwa kutumia Urimu na Thumimu.
6. Wakati askari-jeshi wa Sauli walipokula damu katika hali ya kukata tamaa na kukosa kuadhibiwa, hiyo ilionyesha kwamba huenda kukawa na sababu za haki za kutotii kwa muda mfupi sheria ya kimungu ili kuokoa uhai. (1 Sam. 14:24-35) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 4/15 uku. 31 fu. 7-9.] Si Kweli. Sauli alipotambua kile ambacho askari-jeshi wake walikuwa wamefanya, alichukua hatua za kusuluhisha hali hiyo na Mungu. Pia huenda ikawa Yehova aliona kwamba kiapo cha Sauli cha haraka-haraka kilisababisha hali hiyo ya kukata tamaa. (1 Sam. 14:24, 34, 35)
7. Ingawa watu fulani huhusianisha neno “ushawishi” na hila na werevu, laweza kutumiwa kwa njia ifaayo kumaanisha kusadikisha na kubadilisha nia kupitia kusababu timamu, kwenye mantiki. (2 Tim. 3:14, 15) [w98-SW 5/15 uku. 21 fu. 4] Kweli.
8. “Furushi ya uhai” hurejezea uandalizi wa kimungu wa ulinzi na himaya, ambao ungemfaidi Daudi kama angeepuka kuwa na hatia ya damu machoni pa Mungu. (1 Sam. 25:29) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 6/15 uku. 14 fu. 3.] Kweli.
9. Agano la Ufalme wa Kidaudi, linalorejezewa kwenye 2 Samweli 7:16 (NW), lilipunguziwa wahusika kufikia nasaba ya Mbegu iongozayo kwa Mesiya na ilikuwa uhakikisho wa kisheria kwamba mtu fulani katika nasaba ya Daudi angekuja kutawala “hadi wakati usiojulikana.” [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 2/1 uku. 14 fu. 21-uku. 15 fu. 22.] Kweli.
Jibu maswali yafuatayo:
10. Zaburi 34:18 yatoa uhakikisho gani? [w98-SW 4/1 uku. 31 fu. 2] Yehova yu tayari na ana nia ya kuwategemeza watumishi wake walazimikapo kukabili mshuko-moyo na hisia za kutofaa kitu.
11. Ni nini kilichoonyeshwa na uhakika wa kwamba Yosefu alipewa jina la ziada Barnaba? (Mdo. 4:36) [w98-SW 4/15 uku. 20 fu. 3, kielezi-chini] Yaelekea alikuwa mtu mchangamfu, mwenye huruma. Barnaba humaanisha “Mwana wa Faraja”; kumwita mtu “mwana wa” sifa fulani kulikazia tabia fulani yenye kutokeza ya mtu huyo.
12. Kwa nini simulizi la Biblia husema kwamba Eli aliendelea kuwaheshimu wana wake kuliko alivyomheshimu Yehova? (1 Sam. 2:12, 22-24, 29) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 9/15 uku. 13 fu. 14.] Akiwa baba yao na kuhani wa cheo cha juu wa Israeli, alikuwa na wajibu wa kutia nidhamu wanawe kwa sababu ya mwenendo wao wa kukufuru na ukosefu mzito wa adili, lakini aliwakaripia kwa upole.
13. Kwa nini kitabu cha Ruthu chapaswa kuimarisha uhakika wetu katika ahadi za Ufalme? [si-SW uku. 53 fu. 10] Kwa sababu chaonyesha kwamba Yehova ndiye aliyekuwa Mpangaji wa ndoa ya Boazi na Ruthu na kwamba aliitumia kuwa njia ya kuhifadhi nasaba isiyokatika ya kifalme ya Yuda ikiongoza kwa Daudi na hatimaye kwa Daudi Mkuu Zaidi, Yesu Kristo.
14. Kulingana na 1 Samweli 1:1-7, ni kielelezo gani chenye kutokeza kilichowekwa na familia ya Samweli? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w98-SW 3/1 uku. 16 fu. 12.] Ikiongozwa na baba ya Samweli, Elkana, familia yote ilikuwa ikishiriki kwa ukawaida katika mipango ya kukusanyika pamoja na waabudu wenzao kwenye tabenakulo huko Shilo.
15. Ni katika maana gani inaweza kusemwa kwamba ‘nguvu za mali ni za udanganyifu’? (Mt. 13:22) [w98-SW 5/15 uku. 5 fu. 1]. Ijapokuwa pesa zaweza kutumiwa kununua vitu vya kimwili, mali hizo hazileti uradhi au furaha ambayo yule anayezipata hutazamia kuwa nayo.
16. Yonathani aliyekuwa na umri mkubwa zaidi alionyeshaje kuwa anatambua mtiwa-mafuta wa Yehova, Daudi, na hilo lawakilisha nini leo? (1 Sam. 18:1, 3, 4) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 1/1 uku. 24, 26 fu. 4, 13.] Yonathani aliungana na Daudi katika kifungo chenye kudumu cha urafiki kupitia agano, akionyesha upendo wake na ujitiisho wake kwa Daudi. Kifungo hicho chawakilisha uhusiano kati ya “kondoo wengine” na mabaki ya Wakristo watiwa-mafuta.
17. Ijapokuwa Ayubu alikuwa mtu “mkamilifu na mwelekevu,” kitabu cha Ayubu chaonyeshaje kwamba hilo halimaanishi kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu? (Ayu. 1:8) [w98-SW 5/1 uku. 31 fu. 1] Ayubu alidhania kimakosa kwamba Mungu ndiye aliyesababisha afa lake, akachambua njia ya Mungu ya kushughulika na mwanadamu, naye akatangaza uadilifu wake mwenyewe badala ya kutangaza uadilifu wa Mungu. (Ayu. 27:2; 30:20, 21; 32:2)
18. Ni nini kinachomaanishwa na usemi “jikakamueni wenyewe kisulubu”? (Luka 13:24) [w98-SW 6/15 uku. 31 fu. 1, 4] Usemi huo humaanisha kung’ang’ana, kujitahidi sana, kuwa mwenye bidii, si kuwa na moyo nusu-nusu kuelekea ibada ya Yehova.
19. Tufanyapo kazi pamoja na wengine, ni somo gani la maana tuwezalo kuliweka moyoni, kama ilivyorekodiwa kwenye 2 Samweli 12:26-28? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 12/1 uku. 19 fu. 19.] Twapaswa kuwa tayari kuwasifu wengine tukifanya kazi bila kujionyesha na kutojipatia umashuhuri. Tukiwa tayari kufanya hivyo itakuwa ishara ya unyenyekevu.
Toa maneno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
20. Laana kali ya Yehova dhidi ya ibada ya Baali yapaswa kutusukuma tujiepushe kabisa na mambo ya kisasa yanayolingana ya kufuatia mali, uzalendo, na ukosefu wa adili katika ngono. (Amu. 2:11-18) [si-SW uku. 50 fu. 26]
21. Muhula wa waamuzi uliisha siku za Samweli kisha muhula wa wafalme wa kibinadamu ukaanza wakati ambao hatimaye Israeli wangepoteza kibali cha Yehova. [6, si-SW uku. 53 fu. 1]
22. Jina la Mungu, Yehova, humaanisha “Yeye Husababisha Iwe” nalo hudokeza kwamba Yehova anaweza kutimiza daraka lolote linalotakikana ili atimize makusudi yake. [7, w98-SW 5/1 uku. 5 fu. 3]
23. Eli na Sauli wote walishindwa kwa kuwa yule wa kwanza alipuuza kuchukua hatua na huyu wa pili alitenda kwa kujitanguliza. [14, si-SW uku. 57 fu. 27]
24. Mfano wenye somo wa Yesu wa Msamaria mwenye ujirani waonyesha kwamba mtu aliye mnyoofu kwa kweli ni yule ambaye hutii si sheria za Mungu tu, bali pia huiga sifa zake. (Luka 10:29-37) [17, w98-SW 7/1 uku. 31 fu. 2]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
25. Sifa yenye kupanuka ya (hekima ya; nguvu ya; upendo wa) Yehova yaonekana katika kuchagua Mmoabi wa kike (Ruthu; Naomi; Orpa), aliyekuwa hapo awali mwabudu wa mungu mpagani (Baali; Kemoshi; Dagoni), na ambaye aliongoka kwenye dini ya kweli, awe nyanya wa kale wa Yesu Kristo. (Mt. 1:3, 5, 16) [5, si-SW uku. 51 fu. 1]
26. Kipindi cha utawala wa waamuzi wa Israeli kilikwisha wakati (Samweli; Daudi; Sauli) alitiwa mafuta awe mfalme na punde baada ya hapo akashinda (Waamoni; Wamoabu; Wafilisti) kwa msaada wa Yehova. (1 Sam. 11:6, 11) [8, Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 12/15 uku. 9 fu. 2–uku. 10 fu. 1.]
27. Timotheo alielimishwa na (mtume Paulo; baba yake; mama na nyanya yake) katika “maandishi matakatifu” hadi kufikia hatua ya kumwona akiwa mishonari na mwangalizi bora kabisa. (2 Tim. 3:14, 15; Fil. 2:19-22) [10, w98-SW 5/15 uku. 8 fu. 3–uku. 9 fu. 5]
28. Huduma ya ujanani ya (Daudi; Samweli; Yonathani) yapaswa kutia moyo vijana wawe katika huduma leo, na kuendelea kwake bila kustaafu hadi mwisho wa siku zake kwapasa kutegemeza wale waliodhoofishwa na uzee. [14, si-SW uku. 58 fu. 30]
29. Kipindi kilichohusishwa na 2 Samweli ni kuanzia (1077 hadi karibu 1040; 1077 hadi karibu 1037; 1070 hadi karibu 1040) K.W.K. [15, si-SW uku. 59 fu. 3]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Amu. 11:30, 31; 1 Sam. 15:22; 30:24, 25; 2 Fal. 6:15-17; Yak. 5:11
30. Yehova hutoa uhakikisho kwamba atatumia majeshi yake ya kimbingu kulinda watu wake kulingana na mapenzi yake. [2 Fal. 6:15-17] [3, w98-SW 4/15 uku. 29 fu. 5]
31. Waangalizi wa makutaniko wana daraka la kutimiza mapatano yao hata ingawa huenda nyakati nyingine yakawa yenye kuumiza na yenye kugharimu. [Amu. 11:30, 31] [2, w99-SW 9/15 uku. 10 fu. 3-4]
32. Kushikilia uaminifu-maadili chini ya majaribu huongoza kwenye thawabu kubwa kutoka kwa Yehova Mungu. [Yak. 5:11] [8, w98-SW 5/1 uku. 31 fu. 4]
33. Kumpenda Mungu kutoka moyoni hutaka utii kwa mwelekezo wa kimungu na si kumtolea dhabihu tu. [1 Sam. 15:22] [10, Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 6/15 uku. 5 fu. 1.]
34. Yehova huwathamini sana wale ambao hutumikia katika madaraka ya kuunga mkono tengenezo lake leo. [1 Sam. 30:24, 25] [14, Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 9/1 uku. 28 fu. 4.]