Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/01 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2001
Huduma Yetu ya Ufalme—2001
km 4/01 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Januari 1 hadi Aprili 23, 2001. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Ijapokuwa hatupaswi kuruhusu hisia za kijuujuu tu zitufanye tupuuze makosa mazito, twaweza kuiga kielelezo cha Yosefu kwa kusamehe kwa rehema mtu aliyetukosea ambaye ametubu. (Mwa. 42:21; 45:4, 5) [w99-SW 1/1 uku. 31 fu. 2-3]

2. Mbali na orodha ya nasaba, kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati ni marudio tu ya vitabu vya Samweli na Wafalme. [si-SW uku. 75 fu. 1]

3. Biblia hutaja “mpinga-Kristo” mmoja tu, ambaye atatokea wakati fulani siku zijazo. [rs-SW uku. 212]

4. Yesu alionyesha unyenyekevu wake kwa kukubali mgawo wa pekee wa kuja duniani kutoka mbinguni na kuwa binadamu wa hali ya chini, wa cheo cha chini kuliko malaika. (Flp. 2:5-8; Ebr. 2:7) [w99-SW 2/1 uku. 6 fu. 3]

5. Uvamizi wa Shishaki dhidi ya Yuda na kuchukua ‘hazina za nyumba ya Yehova, na hazina za nyumba ya mfalme’ wathibitishwa na akiolojia. (2 Nya. 12:9) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 2/1 uku. 26 fu. 4.]

6. Ubatizo wa watoto wachanga haukufanywa na Wakristo wa karne ya kwanza. [rs-SW uku. 322]

7. Mtu apaswa kumtumikia Mungu bila kutarajia zawadi. [w99-SW 4/15 uku. 16 fu. 1]

8. Kwa kurejezea “matendo” ya Yehova kama ilivyorekodiwa kwenye Zaburi 103:2, Daudi alikuwa akifikiria uumbaji wa asili wa Yehova. [w99-SW 5/15 uku. 21 fu. 5-6]

9. Mahekalu yaliyojengwa na Solomoni, Zerubabeli, na Herode, na vilevile tabenakulo iliyojengwa na Musa, yote yanafananisha jambo moja. [si-SW uku. 87 fu. 16]

10. Nasaba zinazopatikana katika 1 Mambo ya Nyakati hazikuwa na faida kubwa kwa kutaniko la kwanza la Kikristo. [si-SW uku. 78 fu. 23]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Kwa nini hukumu ya Yehova ilikuwa kali sana kwa nyumba ya Ahabu? (1 Fal. 16:31; 2 Fal. 9:7, 26) [si-SW uku. 74 fu. 34]

12. Kama ionyeshwavyo kwenye Mathayo 24:45-51, wale ambao huwa waasi-imani wana sifa gani? [rs-SW uku. 319]

13. Ni somo gani kuhusu uwezo tuwezalo kujifunza kutokana na kisa cha Mfalme Myudea Uzia? (2 Nya. 26:15-21) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w99-SW 12/1 uku. 26 fu. 1-2.]

14. Badala ya kuanzisha desturi tu, ni somo gani muhimu ambalo Yesu alitutolea kwa kuosha miguu ya mitume wake? (Yn. 13:4, 5) [w99-SW 3/1 uku. 31 fu. 1]

15. Kwa nini simulizi lililo kwenye 1 Mambo ya Nyakati 14:8-17 lilipendeza katika siku za Isaya, na kwa sababu gani lapaswa kupendeza Jumuiya ya Wakristo leo? (Isa. 28:21) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w91-SW 6/1 uku. 21 fu. 2-3.]

16. Ni sehemu gani za ibada ya Baali zilizowavutia sana Waisraeli wengi? [w99-SW 4/1 uku. 29 fu. 3-6]

17. Jitihada za Hezekia za kulinda na kuongeza ugavi wa maji wa Yerusalemu zaweza kutufundisha somo gani lenye kutumika? (2 Nya. 32:3, 4) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 8/15 uku. 6 fu. 1-2.]

18. Mfano wa Yosia wawezaje kuwa kitia-moyo kwa vijana leo wamtumikie Mungu na kusimama imara dhidi ya ibada isiyo ya kweli? (2 Nya. 34:3, 8, 33) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 8/1 uku. 5 fu. 2.]

19. Je, Wayahudi wote waliobaki Babiloni walikuwa wasio waaminifu, na ni somo gani tuwezalo kujifunza kutokana nao? (Ezra 1:3-6) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 1/15 uku. 8 fu. 4, 7.]

20. Katika simulizi la 2 Mambo ya Nyakati 5:13, 14, ni nini kinachoonyesha kwamba Yehova alikuwa akisikiliza wimbo mtamu wa kumsifu kutoka kwa watu wake na kwamba aliufurahia sana pia? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 5/1 uku. 10 fu. 7.]

Toa maneno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Mtu anayemtolea Mkristo mwenzake shauri lazima ahakikishe kuwa msingi wa yale anayosema ni _________________________ , ya kimungu, wala si _________________________ na _________________________ za kibinadamu. (Kol. 2:8) [w99-SW 1/15 uku. 22 fu. 1]

22. Haitawezekana kuchukua msimamo wa _________________________ wakati wa vita ya _________________________ . (Mt. 12:30; 2 The. 1:8) [rs-SW uku. 91]

23. Kama vile miiba iwezavyo kuzuia miche isifikie ukomavu na kuzaa matunda, ndivyo _________________________ lisilodhibitiwa na nguvu za udanganyifu wa _________________________ ziwezavyo kumzuia mtu asifanye maendeleo kufikia ukomavu wa kiroho. (Mt. 13:19, 22) [w99-SW 3/15 uku. 22 fu. 5]

24. ‘Kubatizwa kwa kusudi la kuwa wafu,’ kama Paulo alivyosema kwenye 1 Wakorintho 15:29, humaanisha kuzamishwa katika mwendo wa maisha ambao utaongoza kwenye _________________________ kama kile cha Kristo na kisha _________________________ kwenye uhai wa kiroho kama yeye. [rs-SW uku. 324]

25. Ili Mkristo wa kweli afanikiwe mahali aliposhindwa Solomoni, lazima aweke kando hali yote ya kuwa na _________________________ au _________________________ katika ibada yake na ayakubali maneno ya _________________________ ya ‘kumpenda Yehova Mungu wake kwa moyo wake wote.’ (Mt. 22:37; 1 Nya. 28:9) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 6/1 uku. 19 fu. 17-18.]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Simulizi la 2 Wafalme 17:5, 6 husimulia jinsi (Tiglathi-pileseri; Shalmaneseri wa Tano; Esari-hadoni) alivyovamia ufalme wa kaskazini wa Israeli wenye makabila kumi na kuanza mazingiwa ya miaka mitatu dhidi ya Samaria, mji ambao uliangushwa na Waashuru mwaka wa (740; 607; 537) K.W.K. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 2/15 uku. 27 fu. 1.]

27. Linaposimulia matukio yaliyofanyika Yerusalemu baada ya uhamisho wa Babiloni kuanza, andiko la 2 Wafalme sura ya 25 huelekeza kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa (Danieli; Ezekieli; Yeremia) kuwa mwandikaji wa kitabu hicho na pia huonyesha kwamba kuandikwa kulikamilishwa karibu mwaka wa (580; 537; 455) K.W.K. (2 Fal. 25:27) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona si-SW uku. 64 fu. 3.]

28. Kama Kutoka 4:11 inavyoonyesha, Yehova Mungu ‘anafanya mtu kuwa bubu, kiziwi, na kipofu’ kwa njia ya kwamba (yeye ndiye wa kulaumiwa kwa sababu ya kasoro ambazo watu wanazo; huweka watu tofauti-tofauti kwa mapendeleo ya utumishi; ameruhusu kasoro za kimwili zidhihirike miongoni mwa wanadamu). [w99-SW 5/1 uku. 28 fu. 2]

29. Kipindi cha miaka 70 inayotajwa kwenye 2 Mambo ya Nyakati 36:17-23 kilimalizika mwaka wa (537; 607; 677) K.W.K. [si-SW uku. 84 fu. 35]

30. Marejezo mawili tu ya moja kwa moja kuhusu maadhimisho ya siku za kuzaliwa katika Biblia (huyaweka katika njia ya kuyakubali; huyaweka katika njia ya kutoyakubali; hayataji chochote kuhusu maadhimisho ya siku za kuzaliwa). (Mwa. 40:20-22; Mt. 14:6-10) [rs-SW uku. 356]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Kut. 21:22, 23; Mit. 25:11; Rom. 12:2; 2 Pet. 3:15, 16; Ufu. 16:13, 14

31. Jitihada yahitajiwa ili kubadili kufikiri kwetu na kujaza akili zetu na kweli za Mungu. [w99-SW 4/1 uku. 22 fu. 2]

32. Unapotoa shauri, ni muhimu kuchagua maneno yanayofaa. [w99-SW 1/15 uku. 23 fu. 1]

33. Yehova ameonyesha kwamba mtu atatozwa hesabu kwa kumwumiza mtoto asiyezaliwa. [rs-SW uku. 396]

34. Uvutano wa Shetani Ibilisi ndio unaosukuma mataifa kwenye hali ya ulimwengu itakayosababisha vita dhidi ya Mungu. [rs-SW uku. 91]

35. Kupotoa Maandiko ili yafae mawazo yetu wenyewe kwaweza kutokeza madhara ya kudumu. [rs-SW uku. 47]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki