Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/01 uku. 5
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2001
Huduma Yetu ya Ufalme—2001
km 8/01 uku. 5

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Mei 7 hadi Agosti 20, 2001. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Sala inayotajwa kwenye Nehemia 2:4 ilikuwa sala inayotokana na kukata matumaini, iliyotolewa dakika ya mwisho. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 21 fu. 8.]

2. Neno “kutaniko” linatafsiriwa kutoka neno la Kigiriki ek·kle·siʹa, ambalo latia ndani wazo la umoja na kutegemezana. [w99-SW 5/15 uku. 25 fu. 4]

3. Ijapokuwa watumishi wa Yehova wanaepuka desturi za kifo zinazopingana na Neno la Mungu, hawakatai desturi zote zinazohusiana na kifo. (Yn. 19:40) [rs-SW uku. 104 fu. 4]

4. Katika kipindi alimoishi Ayubu, alikuwa mwanadamu pekee aliyekuwa mwaminifu kwa Yehova. (Ayu. 1:8) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 8/1 uku. 31 fu. 3-4.]

5. Paulo au Sauli alijiruzuku kwa kutengeneza mahema kwa sababu alikuwa na malezi ya hali ya chini. (Mdo. 18:2, 3) [w99-SW 5/15 uku. 30 fu. 2–uku. 31 fu. 1]

6. Ijapokuwa Daudi alifanya dhambi nzito, Yehova aliweza kusema kwamba ‘alinifuata kwa moyo wake wote’ kwa sababu ya toba na sifa zake njema. (1 Fal. 14:8) [w99-SW 6/15 uku. 11 fu. 4]

7. Twapaswa kufanya yote tuwezayo ili kutimiza ahadi zetu hata kama baadaye tutaona vigumu kufanya hivyo, isipokuwa tuwe tumeahidi jambo lisilo la Kimaandiko. (Zab. 15:4) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 9/15 uku. 28 fu. 6.]

8. Zaburi 22:1 yaonyesha kwamba akiwa chini ya mkazo, Daudi alipoteza imani yake kwa muda mfupi. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 8/15 uku. 20 fu. 19.]

9. Huenda Mkristo “akaanguka” kuhusiana na usumbufu, matamauko, na matatizo ya kisheria au kifedha, lakini kwa msaada wa roho ya Mungu na watumishi Wake wenye upendo, “hatavurumishwa chini” kabisa kuhusiana na hali yake ya kiroho. (Zab. 37:23, 24, NW) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 11/1 uku. 30 fu. 14.]

10. Mwanzo sura ya 1 hufundisha kwamba Mungu aliumba kila kitu kwenye dunia hii katika siku sita zenye saa 24. [rs-SW uku. 163 fu. 5]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Ezra na wasaidizi wake ‘walielezaje maana’ ya Sheria? (Neh. 8:8) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 22 fu. 5.]

12. “Furaha ya BWANA [“Yehova,” NW]” yatokana na nini? (Neh. 8:10) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 22 fu. 10.]

13. Kwa nini wale “waliojitoa kwa hiari wakae Yerusalemu” walibarikiwa? (Neh. 11:2) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 22 fu. 13.]

14. Kwa nini Esta alichelewa kumweleza mfalme nia yake? (Esta 5:6-8) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 3/15 uku. 21 fu. 18.]

15. Ni maswali gani mawili ya maana yanayojibiwa katika kitabu cha Ayubu? [si-SW uku. 95 fu. 1]

16. Kwa nini shauri la Elifazi lilimvunja moyo Ayubu badala ya kumtia moyo? (Ayu. 21:34; 22:2, 3) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 2/15 uku. 27 fu. 5-6.]

17. Zaburi ni nini? [si-SW uku. 101 fu. 2]

18. Ni “ubatili” gani ambao mataifa yaliendelea ‘kutafakari,’ kama ilivyoandikwa kwenye Zaburi 2:1? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 8/15 uku. 20 fu. 5.]

19. Tunaweza kujifunza nini kuhusu kutokuwa na ubaguzi kutokana na huduma ya Filipo kwa Wasamaria na ofisa Mwethiopia? (Mdo. 8:6-13, 26-39) [w99-SW 7/15 uku. 25 fu. 2]

20. Ayubu alitoa kielezi gani kuonyesha usadikisho wake kwamba Mungu angemfufua kutoka kaburini, ambapo alipaona kama mahali pa kujificha matatizo yake? (Ayu. 14:7, 13-15) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w00-SW 5/15 uku. 27 fu. 7–​uku. 28 fu. 1.]

Toa neno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Esta 8:17 husema kwamba watu walikuwa ‘wakijifanya kuwa Wayahudi’; vivyo hivyo leo, “ _________________________ ” wa “kondoo wengine” wamechukua msimamo pamoja na _________________________ . (Ufu. 7:9; Yn. 10:16; Zek. 8:23) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 3/15 uku. 22 fu. 14.]

22. Kama Matendo 1:7 ionyeshavyo, ijapokuwa Yehova anajali sana _________________________ , siku yake ya kutoza hesabu itakuja kama _________________________ , bila watu kuitazamia. (2 Pet. 3:10) [w99-SW 6/1 uku. 4 fu. 6—uku. 5 fu. 1]

23. Kwenye 2 Petro 3:7, 10, “mbingu” na “dunia” zatumiwa katika _________________________ ; kama muktadha unavyoonyesha, “dunia” inamaanisha _________________________ . [rs-SW uku. 80 fu. 2-4]

24. Tumaini, imani, na kuelewana hufanya mawasiliano yenye kujenga yawezekane; sifa hizi hutokea wakati ndoa inapoonwa kuwa uhusiano wa _________________________ na kunapokuwa na _________________________ la kweli la kuifanikisha. [w99-SW 7/15 uku. 21 fu. 3]

25. Uvutano wa msongo wa marika unaojenga waweza kutusaidia _________________________ kulingana na adili na matakwa ya kiroho na hivyo kutusaidia tumtumikie Yehova kwa _________________________ . [w99-SW 8/1 uku. 24 fu. 3]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Mordekai ‘aliketi katika lango la mfalme,’ hiyo ikionyesha kwamba alikuwa (mlinzi wa mfalme; mmoja wa maafisa wa Mfalme Ahasuero; akingojea mahojiano na mfalme). (Esta 2:19, 20) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 3/15 uku. 21 fu. 9.]

27. Kulingana na Ayubu 19:25-27, Ayubu alionyesha imani kwamba ‘angemwona Mungu’ hiyo ikimaanisha kwamba (angependelewa kuona njozi; angefufuliwa aishi mbinguni; angepata kufunguliwa macho yake ya uelewevu ili aone kweli kuhusu Yehova). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 11/15 uku. 19 fu. 17.]

28. Ayubu akumbukwa zaidi kwa ajili ya (upendo wake; fadhili zake; uvumilivu wake). (Yak. 5:11) [si-SW uku. 100 fu. 41]

29. Uandikaji wa kitabu cha Zaburi ulichukua kipindi cha miaka (300; 500; 1,000) hivi. [si-SW uku. 101 fu. 4]

30. (Daudi; Asafu; Ezra) ndiye aliyekuwa mpangaji wa mwisho wa kitabu cha Zaburi. [si-SW uku. 102 fu. 6]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Neh. 3:5; Zab. 12:2; 19:7; 2 Tim. 3:16, 17; Yak. 5:14-16

31. Twapaswa kuwa tayari kujitoa kwa bidii na kutosita kwa kiburi, na kuona kwamba kazi ngumu haipatani na cheo chetu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 21 fu. 12, 19.]

32. Mkristo ambaye amehusika katika kosa zito apaswa kuungama dhambi yake kwa wazee. [rs-SW uku. 368 fu. 4]

33. Ijapokuwa Mungu alitumia ndoto kutoa maonyo, mafundisho, na unabii kwa watu wake wa zamani, sasa yeye hutupa wokovu kupitia Neno lake lililopuliziwa. [rs-SW uku. 248 fu. 4]

34. Tukitaka kuwa rafiki za Mungu lazima tuwe wanyofu moyoni, bila unafiki. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 9/15 uku. 27 fu. 1.]

35. Kutii sheria ya Mungu kwaweza kutia nguvu nafsi ya mtu na kuboresha hali yake. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w00-SW 10/1 uku. 13 fu. 4.]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki