Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/02 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2002
Huduma Yetu ya Ufalme—2002
km 12/02 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Septemba 2 hadi Desemba 23, 2002. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu ya maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Kutafakari sifa za ajabu za Yehova ni hatua muhimu ya kuwa na uhusiano wa karibu naye. (Zab. 143:5) [w00-SW 10/15 uku. 4 fu. 6]

2. Kuunganishwa kwa vile vijiti viwili vinavyotajwa kwenye Ezekieli 37:15-24 kuna ulinganisho wa nyakati za kisasa wa kuonyesha kwamba mwaka wa 1919 watiwa-mafuta waaminifu waliunganishwa chini ya Kristo, “mfalme mmoja” na “mchungaji mmoja” wao. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 25 fu. 13.]

3. Ingawa wachambuzi wa Biblia wametilia shaka ukweli wa kihistoria wa kitabu cha Danieli, mavumbuzi ya kiakiolojia ya miaka iliyopita yameondoa kabisa maoni wanayoshikilia. [si-SW uku. 138 fu. 4]

4. Tunaposikia jambo fulani kutoka kwa chanzo au mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu, hatuwezi kuwa na sababu nzuri ya kupinga jambo hilo. [w00-SW 12/1 uku. 29 fu. 7-8]

5. Usemi “manabii wenye umaana mdogo” hufafanua kwa kufaa umuhimu mdogo wa vitabu 12 vya mwisho vya Maandiko ya Kiebrania. [ si-SW uku. 143 fu. 1]

6. Amosi alikuwa mmoja wa “wana wa manabii” wakati Yehova alipomwita na kumtuma atoe unabii kwa Yuda na Israeli. (2 Fal. 2:3) [si-SW uku. 148 fu. 1]

7. Andiko la Obadia mstari wa 16 latabiri kukatiliwa mbali kabisa kwa taifa la Edomu kwa sababu ya chuki yao kwa Yuda. (Oba. 12) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 4/15 uku. 30 sanduku.]

8. “Lugha iliyo safi” inayozungumzwa kwenye Sefania 3:9 hutia ndani kumwelewa kikweli Mungu na makusudi yake. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w01-SW 2/15 uku. 27 fu. 18.]

9. Kilichomletea Yesu mkazo mkali wa kihisia katika bustani ya Gethsemane ni kwamba alikuwa na wasiwasi jinsi ambavyo kifo chake kama mhalifu anayedharauliwa kingeathiri Yehova na jina Lake takatifu. (Mt. 26:38; Luka 22:44) [w00-SW 11/15 uku. 23 fu. 1]

10. “Mfilisti” anayekuwa “kama shehe katika Yuda,” kama inavyoelezwa kwenye Zekaria 9:6, 7, NW, ni mfano wa washiriki wa kondoo wengine leo ambao wamezoezwa na “mtumwa mwaminifu na mwenye busara” na wamepewa mamlaka kama inavyohitajiwa. (Mt. 24:45) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 7/1 uku. 23 fu. 14.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Daraka letu la kuhubiri laweza kulinganishwaje na daraka la Ezekieli kama mlinzi? (Eze. 33:1-11) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 1/1 uku. 28 fu. 13.]

12. Njozi ya Ezekieli kuhusu mifupa mikavu ilitimizwa jinsi gani katika nyakati zetu? (Eze. 37:5-10) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 24 fu. 12.]

13. Ni uthibitisho gani wenye kusadikisha wa kwamba kitabu cha Zekaria kimepuliziwa na Mungu? [si-SW uku. 169 fu. 5]

14. Ni nini kinachowakilishwa na jiji katika njozi ya Ezekieli? (Eze. 48:15-17, NW) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w99-SW 3/1 uku. 18 fu. 22.]

15. Kwa nini tunaweza kusababu kwamba kulingana na Isaya 2:2-4, matukio yanayoendelea huko Israeli leo hayatimizi kihususa unabii wa Biblia? [rs-SW uku. 414 fu. 1]

16. Twaweza kujifunza somo gani kutokana na jinsi Danieli alivyotenda kuhusu amri ya mfalme kwamba dua isitolewe kwa mungu yeyote au mwanadamu yeyote isipokuwa mfalme kwa siku 30? (Dan. 6:7-10) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona dp-SW uku. 125 fu. 25–uku. 126 fu. 28.]

17. Mabaki wamekuwa kama simba kati ya mataifa kwa kutangaza ujumbe gani wa Yehova? (Mika 5:8) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w82-SW 1/15 uku. 22 fu. 10 au w81-E 7/15 uku. 23 fu. 10.]

18. Ni nini kinachomaanishwa na usemi “ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe,” kwenye Habakuki 3:14? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w00-SW 2/1 uku. 22 fu. 15; w81-E uku. 29 fu. 6-7.]

19. Ni nini kinachoonyeshwa na matumizi ya neno “huenda” kwenye Sefania 2:3? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w01-SW 2/15 uku. 19 fu. 8.]

20. Kulingana na Zekaria 8:6, kuanzia mwaka 1919 na kuendelea, Yehova ametimizaje jambo ambalo huenda lilionekana haliwezekani kwa maoni ya binadamu? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 1/1 uku. 16 fu. 18-19.]

Toa neno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Twasema na Yehova kupitia _________________________ , ambayo yamaanisha kusema na Mungu kwa heshima kisha, njia kuu ambayo Mungu huongea nasi ni kupitia _________________________ . (Zab. 65:2; 2 Tim. 3:16) [w00-SW 10/15 uku. 5 fu. 2-3]

22. Yesu Kristo anaweza kutambulishwa kuwa Mikaeli kwa kulinganisha Yuda 9 na 1 Wathesalonike 4:16 (Revised Standard), ambapo amri ya Yesu Kristo kwamba ufufuo uanze inasimuliwa kuwa “ _________________________ ”; pia, jina Mikaeli lamaanisha “ _________________________ _________________________ ,” ikionyesha wazi kwamba Yesu ndiye huongoza katika kutetea enzi kuu ya Yehova na kuharibu maadui wa Mungu. [rs-SW uku. 436 fu. 5–uku. 437 fu. 1]

23. “Kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu” kulitokea mwaka wa _________________________ , ndipo majuma 69 ya miaka yalipoanza, ambayo yalimalizika Mesiya alipotokea mwaka wa _________________________  (Dan. 9:25) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona dp-SW uku. 190 fu. 20–​uku. 191 fu. 22.]

24. Andiko la Yoeli 2:31, linalosema kuhusu jua kugeuka kuwa giza, linalingana na Mathayo 24:29, 30, ambapo _________________________ anaonyesha kuja kwake akiwa Mwana wa binadamu akiwa na _________________________ . [si-SW uku. 147 fu. 13]

25. Unabii wa _________________________ kuhusu Ashuru na jiji lake kuu _________________________ , hutukuza haki na ukuu wa Yehova na kutuhakikishia kwamba atatekeleza haki yake kwa waovu wote. [si-SW uku. 160 fu. 11]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Kitabu cha Ezekieli hukazia kwamba Yehova ni (mkarimu; mnyenyekevu; mtakatifu) na chajulisha (jinsi utu wa mtu ulivyo; utakaso wa jina la Yehova; kuwa jirani mwema) ni muhimu zaidi ya kitu kingine chochote. [si-SW uku. 137 fu. 33]

27. Ezekieli, ambaye aliishi wakati mmoja na Danieli, anathibitisha kwamba Danieli alikuwa mtu halisi, akimtaja pamoja na (Noa na Yobu; Musa na Yoshua; Eliya na Elisha). [si-SW uku. 138 fu. 2]

28. Kupatana na Danieli 2:34, 35, 45, lile jiwe linalopiga na kuvunjavunja ile sanamu lawakilisha (Har–Magedoni; ujumbe mbalimbali mkali wa hukumu unaotangazwa na watu wa Mungu; Ufalme wa Kimesiya). [si-SW uku. 142 fu. 20, 23]

29. Taifa la mfano la nzige linalotajwa kwenye Yoeli 1:4-6 lawakilisha (taifa la Israeli; Wakristo watiwa-mafuta; majeshi ya Roma). (Mdo. 2:1, 14-17) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w98-SW 5/1 uku. 9 fu. 9.]

30. “Ufalme wa Mwana wa upendo wake” unaotajwa kwenye Wakolosai 1:13 ni (Ufalme wa Kimesiya; utawala wa Kristo juu ya kutaniko la Kikristo kuanzia Pentekoste 33 W.K. na kuendelea; Utawala wa Miaka Elfu wa Kristo). [rs-SW uku. 332 fu. 3]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Hos. 6:6; Yoe. 2:32; Zek. 4:6, 7; 13:3; Rom. 12:2

31. Hatupaswi kuruhusu viwango vya utamaduni vya ulimwengu huu vigeuze mawazo yetu. [w00-SW 11/1 uku. 21 fu. 5]

32. Si sadaka nyingi za sherehe za kidini ndizo zimpendezazo Mungu, bali wonyesho wa upendo mwaminifu unaotegemea kumjua yeye. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona si-SW uku. 145 fu. 16.]

33. Kujua jina la Mungu, kulistahi, na kumtegemea yeye ni muhimu ili kuokolewa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 3/15 uku. 30 sanduku.]

34. Kusudi la Mungu latimizwa si kwa sababu ya nguvu zozote za binadamu bali ni kupitia roho yake, ambayo huwawezesha watumishi wake washinde vizuizi vyovyote vilivyo kama milima na kuvumilia katika utumishi wa Mungu. [si-SW uku. 169 fu. 2]

35. Uaminifu wa tengenezo la Yehova hushinda uhusiano wote wa kibinadamu, kama ule kati ya watu wa familia au wa ukoo. [si-SW uku. 171 fu. 24]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki