Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/03 uku. 6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2003
Huduma Yetu ya Ufalme—2003
km 8/03 uku. 6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatashughulikiwa kwa njia ya maswali na majibu katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanzia Agosti 25, 2003. Mwangalizi wa shule atashughulikia pitio la dakika 30 linalotegemea habari iliyozungumziwa kwenye hotuba zilizotolewa juma la kuanzia Julai 7 hadi Agosti 25, 2003. [Taarifa: Mahali ambapo vitabu vya marejezo havijatajwa baada ya swali, utahitaji kufanya utafiti wako mwenyewe ili kupata majibu.—Ona Shule ya Huduma, uku. 36-37.]

SIFA ZA USEMI

1. Kuna manufaa zipi za kuwatazama watu macho unapokuwa katika huduma? [be uku. 125 fu. 1-2; uku. 125 sanduku]

2. Ukishikwa na wasiwasi kabla ya kuanza huduma, ni nini kinachoweza kukusaidia? [be uku. 128 fu. 4-5]

3. Ni nini kitakachokusaidia kuongea kwa njia ya kawaida na ya maongezi unapotoa hotuba jukwaani? [be uku. 129 fu. 2; uku. 129 sanduku]

4. Kanuni zinazopatikana kwenye Mambo ya Walawi 16:4, 24, 26, 28; Yohana 13:10; na Ufunuo 19:8 zinapasa kuwa na matokeo gani kwa sura yetu na kwa nini jambo hilo ni muhimu? [be uku. 131 fu. 3; uku. 131 sanduku]

5. Fafanua mtu aliye na kiasi na “utimamu wa akili.” (1 Tim. 2:9, 10) [be uku. 132 fu. 1]

HOTUBA NA. 1

6. Ingawa lazima Wakristo wachukuliane kwa subira, ni nini ambacho hawawezi kuvumilia? (Kol. 3:13) [w01 7/15 uku. 22 fu. 7-8]

7. Kweli au Si Kweli: Namba mpango ni namba kamili. Eleza. [si uku. 282 fu. 24-25]

8. Ni sababu gani nzuri zaidi inayotufanya tusome Neno la Mungu, na kwa nini mtazamo huo ni wa maana? [be uku. 24 fu. 1]

9. Mwenye hekima ‘huhifadhije maarifa’? (Mit. 10:14) [w01 7/15 uku. 27 fu. 4-5]

10. Kwa nini mazoea mazuri ya Ayubu yanavutia? (Ayu. 1:1, 8; 2:3) [w01 8/1 uku. 20 fu. 4]

USOMAJI WA BIBLIA WA KILA JUMA

11. Washiriki wa baraza linaloongoza walifikiaje “kauli moja” kwamba waamini Wasio Wayahudi hawakuhitaji kutahiriwa ili waokolewe? (Mdo. 15:25)

12. Kwa nini baraza linaloongoza lilimwagiza Paulo atimize maagizo fulani ya Sheria ya Musa hali Mungu alikuwa amefutilia mbali Sheria hiyo? (Mdo. 21:20-26) [it-1 uku. 481 fu. 3; it-2 uku. 1163 fu. 6–uku. 1164 fu. 1]

13. Ni mashtaka gani ya uongo ambayo yalifanywa dhidi ya mtume Paulo yanayotukumbusha mashtaka ambayo yamefanywa dhidi ya Mashahidi wa Yehova nyakati za karibuni? (Mdo. 24:5, 6) [w01 12/15 uku. 22 fu. 7–uku. 23 fu. 2]

14. Paulo aliweka kielelezo gani akiwa mtangazaji wa Ufalme hata alipokuwa katika kifungo cha nyumbani kwa miaka miwili? (Mdo. 28:30, 31)

15. “Mamlaka zilizo kubwa” ni sehemu ya mpango wa Mungu katika njia gani, na hilo lapasa kuathirije Wakristo? (Rom. 13 1, 2) [w00 8/1 uku. 4 fu. 5]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki