Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatashughulikiwa kwa njia ya maswali na majibu katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Februari 27, 2006. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 30 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Januari 2 hadi Februari 27, 2006. [Taarifa: Mahali ambapo vichapo vya marejeo havijaonyeshwa baada ya swali, utahitaji kufanya utafiti wako mwenyewe ili kupata majibu.—Ona Shule ya Huduma, uku. 36-37.]
SIFA ZA USEMI
1. Shule ya Huduma ya Kitheokrasi hutusaidia katika njia zipi ‘kumtolea Mungu dhabihu ya sifa na kulifanyia jina lake tangazo la hadharani’? (Ebr. 13:15) [be uku. 5 fu. 3–uku. 6 fu. 1]
2. Kwa nini tujitahidi sana kusoma kwa usahihi? [be uku. 83 fu. 1-5]
3. Kwa nini ni muhimu kusoma na kusema kwa njia inayoeleweka wazi? [be uku. 86 fu. 1-6]
4. Kwa nini ni muhimu kutamka maneno vizuri, na tunahitaji kuzingatia mambo gani? [be uku. 89 fu. 1–uku. 90 fu. 2, sanduku]
5. Ni mapendekezo gani yatakayotusaidia tuzungumze kwa ufasaha? [be uku. 94 fu. 4-5, sanduku]
HOTUBA NA. 1
6. Andiko la 2 Mambo ya Nyakati 36:17-23 linathibitishaje kwamba unabii wa Biblia unategemeka? [si uku. 84 fu. 35]
7. Ni matukio gani yenye kufuatana yaliyowawezesha Wayahudi kurudi kwenye nchi yao katika 537 K.W.K. ili kujenga upya nyumba ya Yehova? [si uku. 85 fu. 1-3]
8. Kitabu cha Ezra kinamteteaje Yehova kuwa Mungu wa kweli, nacho kinaimarishaje uhakika katika Yehova? [si uku. 87 fu. 14, 18]
9. Kwa nini “mwaka wa 20 wa Mfalme Artashasta,” ni muhimu katika kukadiria tarehe za matukio ya Biblia? (Neh. 2:1, 5, 6, 11, 17, 18) [si uku. 88 fu. 2, 5]
10. Nehemia ni mfano mzuri kwa watumishi wa Mungu leo katika njia gani? [si uku. 90 fu. 16-17]
USOMAJI WA BIBLIA KILA JUMA
11. Je, Wayahudi waliorudi kutoka uhamishoni walitumia Urimu na Thumimu, ambazo zilikuwa zikitumiwa kutafuta jibu kutoka kwa Yehova? (Ezra 2:61-63)
12. Kwa nini Wayahudi wengi waliokuwa Babiloni hawakutaka kurudi Yerusalemu pamoja na Ezra? (Ezra 7:28–8:20)
13. Kazi ya kujenga upya ukuta ingewezaje kufanywa kwa mkono mmoja tu? (Neh. 4:17, 18)
14. Kwa kuwa barua za siri ziliwekwa katika mfuko uliotiwa muhuri, kwa nini Sanbalati alimpelekea Nehemia “barua iliyokuwa wazi”? (Neh. 6:5)
15. Mbali na “kuwalaumu” Wayahudi waliokuwa wakirudi nyuma kama alivyokuwa amewalaumu wakuu na watu wenye vyeo, ni hatua gani nyingine za kuwarekebisha ambazo Nehemia alichukua? (Neh. 13:25, 28)