Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Oktoba 26, 2009.
1. Kwa nini Yehova alimkasirikia Balaamu kwa kuandamana na wanaume wa Balak, ilhali alikuwa amemwambia aende nao? (Hes. 22:20-22) [w04 8/1 uku. 27 fu. 3]
2. Sifa ya Finehasi ya ‘kutovumilia ushindani wowote’ kumwelekea Yehova, inatusaidiaje kutafakari kuhusu uamuzi wetu wa kujiweka wakfu kwa Mungu? (Hes. 25:11) [w95 3/1 uku. 16 fu. 13]
3. Kwa nini Yoshua alichaguliwa kuwa kiongozi baada ya Musa? (Hes. 27:15-19) [w02 12/1 uku. 12 fu. 1]
4. Andiko la Hesabu 31:27 linaweza kuwatia moyo Wakristo leo jinsi gani? [w05 3/15 uku. 24]
5. Waisraeli walinufaikaje na mpango wa majiji ya makimbilio? (Hes. 35:11, 12) [w95 11/15 uku. 14 fu. 17]
6. Kwa nini busara ni sifa muhimu kwa Wakristo, na ina matokeo gani? (Kum. 1:13) [w03 1/15 30; w00 10/1 uku. 32 fu. 1-3]
7. Sheria ya Musa ilionyesha uadilifu wa Mungu kwa njia zipi? (Kum. 4:8) [w02 6/1 uku. 14 fu. 8–uku. 15 fu. 10]
8. Eleza njia inayofaa na njia isiyofaa ya kumjaribu Yehova kupatana na Kumbukumbu la Torati 6:16-18. [w04 9/15 uku. 27 fu. 1]
9. Mahitaji ya Waisraeli yalikuwa yametimizwa jinsi gani kwa kila neno la kinywa cha Yehova, nasi tunaweza kulishwa jinsi gani kwa kila neno la Yehova leo? (Kum. 8:3) [w99 8/15 uku. 25-26]
10. Andiko la Kumbukumbu la Torati 12:16, 24 linaonyesha nini kuhusu matibabu yanayohusisha damu ya mgonjwa mwenyewe? [w00 10/15 uku. 30 fu. 7]