Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/09 uku. 3
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma ya Ufalme—2009
Huduma ya Ufalme—2009
km 12/09 uku. 3

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Desemba 28, 2009.

1. Wakristo leo wanawezaje kufuata kanuni inayotajwa katika Kumbukumbu la Torati 14:1? [w05 1/1 uku. 28; w04 9/15 uku. 27 fu. 4]

2. Ndugu katika kutaniko la Kikristo leo wanawezaje kufuata kanuni inayoonyeshwa katika andiko la Kumbukumbu la Torati 20:5-7? [w04 9/15 uku. 27 fu. 5]

3. Waisraeli walikuwa tofauti jinsi gani na mataifa mengine kuhusiana na mambo ya vita? (Kum. 20:10-15, 19, 20; 21:10-13) [cl uku. 134-135, fu. 17]

4. Ni nini kinachoweza kutusaidia kumtumikia Yehova kwa shangwe ya moyo? (Kum. 28:47) [w95 1/15 uku. 16 fu. 4-5]

5. Wazazi wanawezaje kunufaika na ulinganisho (mfano) unaosimuliwa katika Kumbukumbu la Torati 32:9, 11, 12, ambao unaonyesha jinsi Yehova alivyowapenda Waisraeli? [w01 10/1 uku. 9 fu. 7–uku. 10 fu. 9]

6. Tunapaswa kuelewaje maneno yasiyo ya kweli ambayo Rahabu aliwaambia watu waliotumwa na mfalme kuwatafuta wale wapelelezi? (Yos. 2:4, 5) [w93 12/15 uku. 25 fu. 1]

7. Tendo la Waisraeli linalosimuliwa katika Yoshua 3:15, 16 linatufundisha nini? [w04 12/1 uku. 9 fu. 6]

8. Tunajifunza nini kutokana na jinsi Yoshua alivyoshughulikia wizi wa Akani? (Yos. 7:20-25) [w04 12/1 uku. 11 fu. 4]

9. Andiko la Yoshua 9:22, 23 linakaziaje kwamba Neno la Mungu linatimia hakika? [w04 12/1 uku. 11 fu. 3; si uku. 44, fu. 13]

10. Mfano wa Kalebu unatutia moyo jinsi gani? (Yos. 14:8, 10-12) [w04 12/1 uku. 12 fu. 2; w93 5/15 uku. 29 fu. 1]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki