Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/10 uku. 7
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2010
Huduma Yetu ya Ufalme—2010
km 8/10 uku. 7

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Agosti 30, 2010. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 20 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Julai 5 hadi Agosti 30, 2010.

1. Kutafakari sala ambayo Sulemani alitoa wakati wa kuwekwa wakfu kwa hekalu, kutatusaidiaje kuthamini sifa za Yehova zisizo na kifani? (1 Fal. 8:22-53) [w05 7/1 uku. 30 fu. 3; it-2-E uku. 989 fu. 4]

2. Kwa nini tunaweza kusema kuwa Daudi alitembea mbele ya Yehova “kwa utimilifu wa moyo,” licha ya makosa mengi aliyofanya? (1 Fal. 9:4) [w97 5/1 uku. 5 fu. 1-2]

3. Kwa nini malkia wa Sheba alisema hivi kumhusu Sulemani: “Ni wenye furaha hawa watumishi wako wanaosimama mbele yako daima, wakiisikiliza hekima yako!”? (1 Fal. 10:4-8) [w99 11/1 uku. 20 fu. 5-7]

4. Agizo la Yehova kwamba Abiya azikwe kwa heshima linatufunza nini? (1 Fal. 14:13) [cl uku. 244 fu. 11]

5. Eliya alimtembelea Ahabu kwa mara ya kwanza katika majira gani, na hivyo ujumbe wake ulikuwa na matokeo gani? (1 Fal. 17:1) [w08 4/1 uku. 19, sanduku]

6. Eliya alimaanisha nini alipotumia usemi ‘kuyumba-yumba juu ya maoni mawili tofauti’? (1 Fal. 18:21) [w08 1/1 uku. 19 fu. 2-3]

7. Kama inavyoonyeshwa na kisa cha Eliya, Yehova hutumia nguvu zake kuelekea watumishi wake kwa kusudi gani? (1 Fal. 19:1-12) [cl uku. 42-43 fu. 15-16]

8. Kwa nini Nabothi alikataa kumuuzia Ahabu shamba lake la mizabibu, na tunajifunza nini kutokana na hilo? (1 Fal. 21:3) [w97 8/1 uku. 13 fu. 18-20]

9. Mwanamke wa Shunemu ‘alijinyima’ au alijishughulisha kwa ajili ya Elisha katika njia gani? (2 Fal. 4:13) [w97 10/1 uku. 30 fu. 6-8]

10. Kwa nini Elisha alikataa zawadi ya Naamani? (2 Fal. 5:15, 16) [w05 8/1 uku. 9 fu. 2]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki