Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/10 uku. 3
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2010
Huduma Yetu ya Ufalme—2010
km 10/10 uku. 3

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Oktoba 25, 2010. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 20 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Septemba 6 hadi Oktoba 25, 2010.

1. Tunaweza kujifunza nini kwa kuchunguza maisha ya Mfalme Azaria (Uzia)? (2 Fal. 15:1-6) [w91 7/15 uku. 29-30]

2. Kwa kuwa inasemekana kuwa Mfalme Yothamu wa Yuda alitawala kwa miaka 16 tu, kwa nini andiko la 2 Wafalme 15:30 linarejelea “mwaka wa 20” wa utawala wake? (2 Nya. 27:7, 8) [it-2-E uku. 119 fu. 5]

3. “Wasamaria” wanaotajwa katika 2 Wafalme 17:29, walikuwa akina nani? [it-2-E uku. 847 fu. 7; w90 12/1 uku. 3 fu. 3]

4. Kwa nini Yehova anasemwa kuwa ‘amelifanya’ kusudi lake? (2 Fal. 19:25) [w99 8/15 uku. 14 fu. 3]

5. Andiko la 2 Wafalme 25:8, 25, 26 linaonyeshaje kwa usahihi mwanzo wa kipindi cha miaka 70 ambayo jiji la Yerusalemu lingeachwa ukiwa? [it-1-E uku. 415 fu. 6–uku. 416 fu. 1-2; uku. 463 fu. 4; w06 1/15 uku. 9 fu. 3]

6. Kwa nini andiko la 1 Samweli 16:10, 11 linataja kuwa Daudi alikuwa mwana wa nane wa Yese ilhali Ezra anamtaja kuwa wa saba? (1 Nya. 2:15) [w02 9/15 uku. 31]

7. Tunaweza kuiga mfano wa makabila yaliyoishi mashariki ya Yordani kwa njia gani? (1 Nya. 5:10, 18-22) [w05 10/1 uku. 9 fu. 7]

8. Tunaweza kujifunza nini kutokana na Walawi waliokuwa watunza-malango? (1 Nya. 9:26, 27) [w05 10/1 uku. 9 fu. 8]

9. Kuimba kulikuwa muhimu kadiri gani katika taifa la kale la Israeli? (1 Nya. 9:33) [it-2-E uku. 452 fu. 9; w09 12/1 uku. 30 fu. 1-3; w93 12/1 uku. 25 fu. 5]

10. Je, ilifaa Daudi amkasirikie Yehova kama inavyoonyeshwa katika 1 Nyakati 13:11? [w05 10/1 uku. 11 fu. 2]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki