Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 3/11 uku. 4
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2011
Huduma Yetu ya Ufalme—2011
km 3/11 uku. 4

Matangazo

◼ Toleo la mwezi wa Machi: Biblia Inafundisha Nini Hasa? Jitahidi sana kuanzisha mafunzo ya Biblia. Aprili na Mei: Gazeti la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Mtu akipendezwa, mtolee trakti Je, Ungependa Kujua Ukweli? na ujitahidi kuanzisha funzo la Biblia. Unapowarudia watu waliohudhuria Ukumbusho na/au mikutano na makusanyiko, lakini hawashirikiani na kutaniko kwa ukawaida, zingatia kuanzisha funzo ukitumia kitabu Biblia Inafundisha. Juni: Biblia Inafundisha Nini Hasa? Jitahidi kuanzisha funzo la Biblia katika ziara ya kwanza. Ikiwa mwenye nyumba tayari ana kitabu hiki na hakubali funzo la Biblia, mhubiri anaweza kumwachia kitabu Ujuzi, au broshua Anataka au Endeleeni Kukesha!

◼ Unapomhubiria mtu anayezungumza Kichina, mwonyeshe kijitabu Nations, ukurasa ulio na Kichina (cha Kitamaduni) (CH) na Kichina (Sahili) (CHS), ili ujue anapendelea kusoma Kichina gani. Kwa kawaida, watu kutoka Hong Kong au Taiwan hupendelea kusoma vitabu vya Kichina (cha Kitamaduni) (CH), ilhali watu wanaotoka China hupendelea kusoma Kichina (Sahili) (CHS). Hata hivyo, kuhusiana na machapisho yaliyorekodiwa kama vile CD au DVD, zingatia lahaja ambayo mwenye nyumba huongea na kuelewa vizuri zaidi. Kwa kawaida, watu kutoka China na Taiwan huelewa Kichina (Kimandarini) (CHM), lakini wale wa Hong Kong huelewa Kichina (Kikantoni) (CHC).

◼ Video Jehovah’s Witnesses—Organized to Share the Good News itazungumziwa kwenye Mkutano mmoja wa Utumishi mwezi wa Agosti. Ikiwa kuna uhitaji, agizeni nakala za video hiyo kupitia kutaniko upesi iwezekanavyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki