Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Aprili 30, 2012. Tarehe ambayo kila sehemu itazungumziwa imeonyeshwa ili wahubiri waweze kufanya utafiti wanapojitayarisha kwa ajili ya shule kila juma.
1. Kwa nini kitabu cha Yeremia ni chenye faida kwetu? [Mac. 5, si uku. 129 fu. 36]
2. Yehova anaweza kutukomboa kutoka kwa mnyanyaso katika njia gani leo? (Yer. 1:8) [Mac. 5, w05 12/15 uku. 23 fu. 18]
3. Watiwa-mafuta walirudi kwenye “barabara za zamani za kale” lini na kwa njia gani? (Yer. 6:16) [Mac. 12, w05 11/1 uku. 24 fu. 12]
4. Kwa nini tunaweza kusema kwamba kuna “zeri katika Gileadi” leo? (Yer. 8:22) [Mac. 19, w10 6/1 uku. 22 fu. 3–uku. 23 fu. 3]
5. Yehova ‘hujuta’ katika njia gani baada ya kutoa hukumu? (Yer. 18:7, 8) [Apr. 2, jr uku. 151 sanduku]
6. Yehova alimpumbaza Yeremia katika njia gani, na tunaweza kujifunza nini kutokana na hilo? (Yer. 20:7) [Apr. 2, jr uku. 36 fu. 8]
7. Adui za Israeli walitakaswa katika njia gani? (Yer. 22:6-9) [Apr. 9, it-2-E uku. 1166 fu. 8]
8. Je, ilifaa Yehova awaambie watu wake wa kale: ‘Nimewavuta kwa fadhili zenye upendo’? Eleza. (Yer. 31:3) [Apr. 23, jr uku. 142-145 fu. 8-11]
9. Sheria ya Mungu imeandikwa katika mioyo kwa njia gani? (Yer. 31:33) [Apr. 23, w07 3/15 uku. 11 fu. 2]
10. Ni nini lililokuwa kusudi la kuandika hati mbili za makubaliano au mapatano yaleyale? (Yer. 32:10-15) [Apr. 30, w07 3/15 uku. 11 fu. 3]