Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 2/13 uku. 2
  • Habari Kuu za Utumishi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Habari Kuu za Utumishi
  • Huduma ya Ufalme—2013
Huduma ya Ufalme—2013
km 2/13 uku. 2

Habari Kuu za Utumishi

Kenya: Mwezi wa Agosti, Kenya iliripoti kilele kipya cha wahubiri 25,417—mara ya kwanza kufikia idadi ya wahubiri 25,000 katika historia ya Kenya! Katika kipindi cha mwaka wa utumishi wa 2012, watu 1,303 walibatizwa na watu wakaachiwa magazeti 3,335,791. Mwaka huo kulikuwa na ongezeko la asilimia 3.

Tanzania: Kilele kipya cha wahubiri 16,476 kilifikiwa mwezi wa Agosti. Katika mwaka huo wa utumishi, kulikuwa na ongezeko la asilimia 3 la wahubiri na watu 862 walibatizwa. Kulikuwa na wastani wa funzo 1.1 la Biblia kwa kila mhubiri.

Uganda: Kilele kipya cha wahubiri kilifikiwa mwezi wa Agosti wahubiri 5,924 walipotoa ripoti. Hilo ni ongezeko lenye kutia moyo la asilimia 13 ikilinganishwa na mwezi wa Agosti mwaka uliokuwa umetangulia. Hicho pia kilikuwa kilele kipya cha tatu mfululizo cha wahubiri. Kilele kipya cha mapainia wa kawaida kilikuwa 671. Tarakimu hizo zinaonyesha kwamba kwa kweli wahubiri wanaendelea kuwa na “moyo wa kufanya kazi” kama tunavyotiwa moyo katika Nehemia 4:6.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki