Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Agosti 26, 2013. Tarehe ya kuzungumzia kila sehemu imeonyeshwa ili wahubiri waweze kufanya utafiti wakati wanapojitayarisha kwa ajili ya shule kila juma.
1. Ni somo gani muhimu tunaloweza kujifunza kutokana na jinsi Mfalme Herode alivyokubali kwa kupenda sifa ambazo hakustahili na utukufu kutoka kwa wanadamu? (Mdo. 12:21-23) [Julai 1, w08 5/15 uku. 32 fu. 7]
2. Vijana Wakristo wanaweza kujinufaishaje wenyewe kwa kuchunguza na kufuata kielelezo cha Timotheo? (Mdo. 16:1, 2) [Julai 8, w08 5/15 uku. 32 fu. 10]
3. Akila na Prisila walimsaidiaje Apolo kwa upendo, baada ya kumsikia ‘akisema kwa ujasiri’ katika sinagogi huko Efeso? (Mdo. 18:24-26) [Julai 15, w10 6/15 uku. 11 fu. 4]
4. Kuna msingi gani wa Kimaandiko kwa Mashahidi wa Yehova kutumia mahakama za nchi ili kulinda haki yao ya kuhubiri? (Mdo. 25:10-12) [Julai 22, bt uku. 198 fu. 6]
5. Mtume Paulo aliendeleaje kutafuta njia za kutoa ushahidi hata alipokuwa kifungoni huko Roma, na watumishi wa Yehova leo hufuataje mfano wake? (Mdo. 28:17, 23, 30, 31) [Julai 29, bt uku. 215-217 fu. 19-23]
6. Kwa nini Biblia inasema kwamba ushoga ni kinyume cha asili na ni uchafu? (Rom. 1:26, 27) [Ago. 5, g 1/12 uku. 28 fu. 7]
7. “Fidia ambayo Kristo Yesu alilipa” katika mwaka wa 33 W.K. ingefunika jinsi gani “dhambi zilizotokea” kabla ya fidia kulipwa? (Rom. 3:24, 25) [Ago. 5, w08 6/15 uku. 29 fu. 6]
8. Yehova ameandaa msaada gani wakati tunapokabili hali zenye kutatanisha sana hivi kwamba hatujui ni mambo gani tutakayosema katika sala? (Rom. 8:26, 27) [Ago. 12, w08 6/15 uku. 30 fu. 10]
9. Ni nini maana ya maneno “fuateni mwendo wa ukaribishaji-wageni”? (Rom. 12:13) [Ago. 19, w09 10/15 uku. 5-6 fu. 12-13]
10. Kama mtume Paulo anavyoshauri, tunawezaje ‘kumvaa Bwana Yesu Kristo’? (Rom. 13:14) [Ago. 26, w05 1/1 uku. 11-12 fu. 20-22]