Habari Kuu za Utumishi
Uganda: Tunafurahi kuripoti kwamba mwezi wa Februari kulikuwa na jumla ya wahubiri 6,037. Hiki ni kilele kipya cha wahubiri na ni ongezeko la asilimia nane ikilinganishwa na idadi ya wahubiri mwezi wa Februari mwaka wa 2012. Kwa kweli watu wa Yehova wana shughuli nyingi katika kazi ya kufundisha na kuokoa uhai wa watu!—1 Tim. 4:16.