Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/14 uku. 3
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2014
Huduma Yetu ya Ufalme—2014
km 10/14 uku. 3

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi, juma linaloanza Oktoba 27, 2014.

  1. Kwa nini Waisraeli walinung’unika dhidi ya Mungu na Musa kama tunavyosoma katika Hesabu 21:5, nasi tunapata onyo gani kutokana na simulizi hilo? [Sept. 1, w99 8/15 uku. 26-27]

  2. Kwa nini hasira ya Yehova iliwaka dhidi ya Balaamu? (Hes. 22:20-22) [Sept. 8, w04 8/1 uku. 27 fu. 2]

  3. Andiko la Hesabu 25:11 linatuambia nini kuhusu mtazamo wa Finehasi, nasi tunawezaje kumwiga? [Sept. 8, w04 8/1 uku. 27 fu. 4]

  4. Ni katika njia gani Musa ni kielelezo kizuri cha unyenyekevu kwetu leo? (Hes. 27:5, 15-18) [Sept. 15, w13 2/1 uku. 5]

  5. Kielelezo cha Yoshua na Kalebu kinathibitishaje kwamba watu wasiokamilika wanaweza kufanikiwa kutembea katika njia za Mungu licha ya upinzani? (Hes. 32:12) [Sept. 22, w93 11/15 uku. 14 fu. 13]

  6. Utii wa binti za Selofehadi unapaswa kuathirije maoni ya Wakristo waseja kuhusu ndoa? (Hes. 36:10-12) [Sept. 29, w08 2/15 uku. 4-5 fu. 10]

  7. Waisraeli walipata matokeo gani kwa kuwa na mtazamo wa kulalamika na kusema mambo yasiyofaa, nasi tunajifunza somo gani kutokana na simulizi hilo? (Kum. 1:26-28, 34, 35) [Okt. 6, w13 8/15 uku. 11 fu. 7]

  8. Ili kupata mafanikio na baraka za Yehova katika Nchi ya Ahadi, Waisraeli walipaswa kutimiza matakwa gani mawili? (Kum. 4:9) [Okt. 13, w06 6/1 uku. 29 fu. 15]

  9. Ni katika njia gani nguo za Waisraeli hazikuchakaa wala miguu yao kuvimba katika safari yao nyikani? (Kum. 8:3, 4) [Okt. 20, w04 9/15 uku. 26 fu. 1]

  10. Tunawezaje kutumia himizo walilopewa Waisraeli la “kushikamana” na Yehova? (Kum. 13:4, 6-9) [Okt. 27, w02 10/15 uku. 16 fu. 14]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki