Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr17 Februari uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
  • Vichwa vidogo
  • FEBRUARI 6-​12
Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
mwbr17 Februari uku. 1

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

FEBRUARI 6-​12

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 643 ¶4-5

Talaka

Talaka ya Mfano. Uhusiano wa ndoa unaelezwa kwa njia ya mfano katika Maandiko. (Isa 54:​1, 5, 6; 62:​1-6) Pia, Maandiko yanaeleza kuhusu talaka ya mfano, au kumfukuza mke.​—Yer 3:8.

Ufalme wa Yuda ulipinduliwa na Yerusalemu likaharibiwa mwaka wa 607 K.W.K., na wakazi wa nchi hiyo wakatekwa na kupelekwa uhamishoni huko Babiloni. Miaka mingi kabla ya hapo, Yehova alikuwa amesema hivi kwa njia ya kinabii akizungumza na Wayahudi ambao wangekuwa uhamishoni: “Basi, kiko wapi cheti cha talaka cha mama yenu, ambaye nilimfukuza?” (Isa 50:1) “Mama” yao, au taifa lao, lilikuwa limefukuzwa kwa haki, si kwa sababu Yehova alikuwa amevunja agano lake na kuanza mipango ya talaka, bali ni kwa sababu taifa hilo lilitenda kinyume na Sheria ya agano. Hata hivyo, mabaki ya Waisraeli walitubu na kusali ili Yehova arudishe uhusiano wake pamoja nao akiwa mume wao katika nchi yao. Kwa kuwa Yehova alihangaikia jina lake, katika mwaka wa 537 K.W.K., aliwarudisha watu wake katika nchi yao kama alivyoahidi, mwishoni mwa ile miaka 70 ya uhamisho.​—Zb 137:​1-9; ona NDOA.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki