Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr17 Aprili uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
  • Vichwa vidogo
  • APRILI 3-9
  • APRILI 24-​30
Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2017
mwbr17 Aprili uku. 1

Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

APRILI 3-9

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 17-​21

it-2 776 ¶4

Toba

Mfinyanzi anaweza kuanza kufinyanga chombo cha aina fulani na kisha kuamua kufinyanga chombo kingine ikiwa chombo hicho ‘kinaharibika mkononi mwake.’ (Yer 18:​3, 4) Kwa kutumia mfano huo Yehova anaonyesha kwamba yeye si sawa na mfinyanzi wa kibinadamu ambaye chombo ‘kinaharibikia mkononi mwake,’ bali ana mamlaka kamili juu ya wanadamu; ana mamlaka ya kushughulika na wanadamu kwa njia tofauti kulingana na jinsi wanavyokubali au kukataa uadilifu wake na rehema zake. (Linganisha na Isa 45:9; Rom 9:⁠​19-21) Hivyo, anaweza “[kujuta] juu ya ule msiba [aliokuwa amefikiria] kuutimiza” dhidi ya taifa, au ‘kujuta kwa yale mema ambayo alisema moyoni mwake kuwa atafanya kwa faida yake.’ Mambo hayo yote yalitegemea jinsi taifa hilo lilivyoitikia alipokuwa akishughulika nalo. (Yer 18:⁠​5-10) Jambo hilo halimaanishi kwamba Mfinyanzi Mkuu, Yehova, anakosea bali badala ya hivyo “udongo wa mfinyanzi” yaani wanadamu ndio wanaogeuka na kubadili hali ya moyo na hivyo kumfanya Yehova ajute, au abadili hisia zake.

APRILI 24-​30

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 29-​31

it-1 524 ¶3-4

Agano

Agano Jipya. Yehova alitabiri kuhusu agano jipya kupitia nabii Yeremia katika karne ya saba K.W.K., akieleza kwamba halingekuwa kama agano la Sheria ambalo Waisraeli walilivunja. (Yer 31:​31-34) Yesu Kristo alipoanzisha mwadhimisho wa Mlo wa Jioni wa Bwana katika usiku wa Nisani 14, 33 W.K., alitangaza kwamba agano jipya lingehalalishwa kwa dhabihu aliyotoa. (Lu 22:20) Siku 50 baada ya ufufuo wake na siku 10 baada ya kupaa kwenda kwa Baba yake, alimimina roho takatifu aliyopokea kutoka kwa Yehova juu wanafunzi wake waliokuwa wamekusanyika katika chumba cha juu huko Yerusalemu.​—Mdo 2:​1-4, 17, 33; 2 Ko 3:​6, 8, 9; Ebr 2:​3, 4.

Washiriki wa agano jipya ni Yehova na “Israeli wa Mungu,” waliozaliwa kwa roho katika muungano na Kristo ambao wanafanyiza kutaniko lake au mwili wake. (Ebr 8:10; 12:​22-24; Gal 6:​15, 16; 3:​26-28; Ro 2:​28, 29) Agano jipya linatendeshwa kwa damu iliyomwagwa (dhabihu ya uhai wa mwanadamu) ya Yesu Kristo, na aliwasilisha thamani yake mbele za Yehova baada ya kupaa kwenda mbinguni. (Mt 26:28) Mtu anapochaguliwa na Mungu na kupokea mwito wa kwenda mbinguni (Ebr 3:1), Mungu anamfanya mtu huyo awe mshiriki wa agano Lake kwa msingi wa dhabihu ya Kristo. (Zb 50:5; Ebr 9:​14, 15, 26) Yesu Kristo ndiye mpatanishi wa agano jipya (Ebr 8:6; 9:15) na ndiye sehemu kuu ya Uzao wa Abrahamu. (Gal 3:16) Kwa kuwapatanisha kwa njia ya agano jipya, Yesu anawasaidia wale walio kwenye agano hilo kuwa sehemu ya uzao halisi wa Abrahamu (Ebr 2:16; Gal 3:29) kupitia msamaha wa dhambi zao. Yehova anawatangaza kuwa waadilifu.​—Ro 5:​1, 2; 8:33; Ebr 10:​16, 17.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki