Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb17 Desemba uku. 5
  • Sehemu Mpya ya Mkutano wa Katikati ya Juma

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sehemu Mpya ya Mkutano wa Katikati ya Juma
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Ungeuzima Utambi Ufukao Moshi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Kuingia kwa Kristo Katika Yerusalemu kwa Shangwe ya Ushindi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kristo Aingia Katika Yerusalemu kwa Shangwe ya Ushindi
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Mfalme Aingia Yerusalemu Akiwa Juu ya Mwanapunda
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
mwb17 Desemba uku. 5
Injili ya Mathayo katika toleo la funzo la Tafsiri ya Ulimwengu Mpya lililo kwenye mtandao

MAISHA YA MKRISTO

Sehemu Mpya ya Mkutano wa Katikati ya Juma

Kuanzia Januari 2018, mkutano wa katikati ya juma utatia ndani habari za utafiti, picha, na video kutoka katika toleo la funzo la Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya (nwtsty) la mtandaoni, hata ikiwa toleo la funzo halipatikani katika lugha yenu. Bila shaka, habari hizo zitaboresha jinsi unavyotayarisha mikutano. Jambo muhimu hata zaidi ni kwamba tunatumaini zitakusaidia kumkaribia Baba yetu mwenye upendo, Yehova.

HABARI ZA UTAFITI

Habari hizo zinatia ndani mambo kuhusu jiografia, utamaduni, na uchambuzi wa lugha iliyotumika katika mistari mingi ya Biblia.

Mathayo 12:20

Utambi unaofifia: Taa ndogo iliyotumiwa nyumbani ilitengenezwa kwa udongo na kujazwa mafuta ya zeituni. Utambi wa kitani ulifyonza mafuta ili taa iendelee kuwaka. Msemo wa Kigiriki “utambi unaofifia” huenda ulirejelea utambi unaotoa moshi kwa sababu bado una moto lakini mwangaza wa taa unafifia au umezimwa. Unabii wa Isaya 42:3 ulitabiri kwamba Yesu angekuwa mwenye huruma; kamwe hangezima tumaini dogo la watu wa hali ya chini na walionyanyaswa.

Mathayo 26:13

Kwa kweli: Neno la Kigiriki, a·menʹ, limetoholewa kutokana na neno la Kiebrania ʼa·menʹ, linalomaanisha “na iwe hivyo,” au “bila shaka.” Mara nyingi, Yesu alitumia maneno hayo kabla ya kueleza jambo, kutoa ahadi, au unabii fulani, na hivyo kusisitiza ukweli na kutegemeka kwa alichosema. Hakuna mtu mwingine anayetumia maneno “kwa kweli,” au amina, kwa njia hiyo katika vitabu vitakatifu. Yanapotumiwa mara mbili kwa mfuatano (a·menʹ a·menʹ), kama ilivyo kotekote katika Injili ya Yohana, maneno ya Yesu yanatafsiriwa “kwa kweli kabisa.”—Yoh 1:51.

PICHA NA VIDEO

Picha, ramani, video zisizo na sauti zinaonyesha habari zilizo katika Biblia.

Bethfage, Mlima wa Mizeituni, na Yerusalemu

Video hii fupi inaonyesha njia inayoelekea Yerusalemu kutoka mashariki, kutoka kijiji cha leo cha et-Tur—kinachodhaniwa kuwa eneo la Bethfage linalotajwa katika Biblia—hadi mojawapo ya sehemu za juu zaidi za Mlima wa Mizeituni. Bethania liko mashariki ya Bethfage upande wa mashariki wa Mlima wa Mizeituni. Kwa kawaida Yesu na wanafunzi wake walipokuwa Yerusalemu, walilala huko Bethania. Leo linadhaniwa kuwa mji wa el-ʽAzariyeh (El ʽEizariya), jina la Kiarabu linalomaanisha “Mahali pa Lazaro.” Bila shaka, Yesu alikaa nyumbani kwa Martha, Maria, na Lazaro. (Mt 21:17; Mk 11:11; Lu 21:37; Yoh 11:1) Alipokuwa akisafiri kutoka nyumbani kwao kwenda Yerusalemu, huenda Yesu alitumia njia kama ile inayoonyeshwa katika video hii. Nisani 9, 33 W.K., Yesu alipopanda mwana-punda juu ya Mlima wa Mizeituni kuelekea Yerusalemu, inawezekana alikuwa ametoka Bethfage, akitumia barabara ya kwenda Yerusalemu.

Huenda Yesu alitumia njia hii kutoka Bethania kwenda Yerusalemu
  1. Barabara kutoka Bethania kwenda Bethfage

  2. Bethfage

  3. Mlima wa Mizeituni

  4. Bonde la Kidroni

  5. Hekalu la Mlimani

Msumari Ndani ya Mfupa wa Kisigino

Mfupa wa kisigino cha mwanadamu uliopigiliwa msumari

Hii ni picha ya umbo la mfupa wa kisigino cha mwanadamu uliopigiliwa msumari wenye urefu wa sentimita 11.5. Mfupa halisi wa kisigino cha mwanadamu ulipatikana mwaka wa 1968, uchimbuzi ulipofanywa katika eneo la kaskazini la Yerusalemu. Inakadiriwa kuwa mfupa huo ni wa enzi za Waroma. Huo ni uthibitisho wa kiakiolojia unaoonyesha kwamba labda misumari ilitumiwa kuwaning’iniza watu kwenye nguzo za mbao. Huenda msumari kama huo ulitumiwa na askari-jeshi Waroma kumpigilia Yesu Kristo kwenye mti. Kisigino hicho kilipatikana kwenye sanduku la mifupa lililotengenezwa kwa mawe ya chokaa (ossuary) ambalo lilitumiwa kuhifadhi mifupa ya mtu aliyekufa baada ya nyama kuoza. Hilo linaonyesha kwamba mtu aliyetundikwa mtini angeweza kuzikwa.—Mt 27:35.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki