Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr18 Mei kur. 1-3
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2018
  • Vichwa vidogo
  • MEI 7-13
  • MEI 14-20
  • MEI 21-27
  • MEI 28–JUNI 3
Marejeo ya Daftari la Huduma na Maisha—2018
mwbr18 Mei kur. 1-3

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

MEI 7-13

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MARKO 7-8

“Beba Mti Wako wa Mateso na Uendelee Kunifuata”

nwtsty habari za utafiti—Mk 8:34

lazima ajikane mwenyewe: Au “lazima aache kabisa haki yote aliyo nayo.” Hilo linaonyesha utayari wa mtu kujikana kabisa au kumruhusu Mungu ammiliki kikamili. Maneno hayo ya Kigiriki yanaweza kutafsiriwa “lazima ajikatae,” na yanafaa kwa sababu yanahusisha kutotanguliza tamaa, miradi, na starehe zetu. (2Ko 5:14, 15) Neno hilohilo la Kigiriki lilitumiwa na Marko alipoandika kuhusu Petro kumkana Yesu.—Mk 14:30, 31, 72.

MEI 14-20

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MARKO 9-10

“Maono Yenye Kuimarisha Imani”

nwtsty habari za utafiti–Mk 9:7

sauti: Mara ya pili kati ya mara tatu ambazo vitabu vya Injili vinataja kwamba Yehova anazungumza moja kwa moja na wanadamu.—Habari za utafiti—Mk 1:11; Yoh 12:28.

Kutafuta Hazina za Kiroho

nwtsty habari za utafiti–Mk 10:17, 18

Mwalimu Mwema: Ni wazi kwamba mwanamume huyo alikuwa akitumia maneno “Mwalimu Mwema” kama cheo rasmi na cha kumkweza, kwa kuwa viongozi wa kidini walidai waheshimiwe hivyo. Ingawa Yesu hakupinga alipotambulishwa kwa njia inayofaa kuwa “Mwalimu” na “Bwana” (Yoh 13:13), alimwelekezea Baba yake utukufu wote.

Hakuna aliye mwema, isipokuwa mmoja, Mungu: Kwa maneno hayo Yesu anaonyesha kuwa anatambua Yehova ndiye kiwango cha juu zaidi cha wema, Yeye ndiye mwenye haki kamili ya kuamua mema na mabaya. Adamu na Hawa walipoasi kwa kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya, walitaka kunyakua haki hiyo. Tofauti nao, kwa unyenyekevu Yesu anatambua Baba yake ndiye anayepaswa kuweka viwango. Mungu ameeleza na kufafanua yaliyo mema kupitia mambo aliyoamuru katika Neno lake.—Mk 10:19.

MAISHA YA MKRISTO

“Kile Ambacho Mungu Ameunganisha . . . ”

nwtsty habari za utafiti–Mk 10:4

cheti cha kumfukuza: Au “cheti cha talaka.” Kwa kutaka mtu ambaye anafikiria kutoa talaka atayarishe hati ya kisheria na ikiwezekana azungumze na wazee, Sheria ilimpa mtu huyo muda wa kufikiria upya uamuzi huo mzito. Kusudi la Sheria hiyo lilikuwa kuzuia talaka zilizotolewa ovyoovyo na kuwapa wanawake kiwango fulani cha ulinzi wa kisheria. (Kum 24:1) Lakini katika siku za Yesu, viongozi wa kidini walifanya iwe rahisi kutoa talaka. Mwanahistoria wa karne ya kwanza Yosefo, ambaye alikuwa Farisayo aliyemtaliki mke wake, alipendekeza kwamba talaka ingeweza kutolewa “kwa sababu yoyote ile (na wanaume wana sababu nyingi).”—Ona habari za utafiti—Mt 5:31.

nwtsty habari za utafiti–Mk 10:11

anayetaliki mke wake: Au “anayemfukuza mke wake.” Maneno ya Yesu yaliyorekodiwa kwenye Marko yanapaswa kueleweka kwa kulinganishwa na sentensi kamili iliyo kwenye Mt 19:9, inayotia ndani maneno haya “isipokuwa kwa sababu ya uasherati.” (Ona habari za utafiti—Mt 5:32.) Maneno ya Yesu ambayo Marko ananukuu kuhusu talaka yanahusika ikiwa msingi wa kupata talaka ni kitu kingine isipokuwa “uasherati” (Kigiriki, por·neiʹa) uliofanywa na mwenzi asiye mwaminifu.

anafanya uzinzi dhidi yake: Hapa Yesu anapinga fundisho lililokuwa likiendelezwa na Marabi kwamba mwanamume anaruhusiwa kumtaliki mke wake “kwa sababu yoyote ile.” (Mt 19:3, 9) Wazo la kwamba mwanamume anaweza kufanya uzinzi dhidi ya mke lilikuwa geni kwa Wayahudi wengi. Marabi walifundisha kwamba mume hawezi kufanya uzinzi dhidi ya mke wake—ni mwanamke tu anayeweza kukosa kuwa mwaminifu. Lakini kwa kuonyesha kwamba mume ana wajibu uleule wa kufuata maadili kama mke, Yesu aliwaheshimu wanawake na kuwastahi.

MEI 21-27

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MARKO 11-12

“Ametumbukiza Zaidi ya Wote”

nwtsty habari za utafiti–Mk 12:41, 42

masanduku ya hazina: Vyanzo fulani vya zamani vya Kiyahudi vinasema kwamba masanduku hayo ya michango yalikuwa na umbo la pembe, na labda yalikuwa na matundu madogo ya kutumbukizia michango kwenye sehemu ya juu. Watu walitumbukiza matoleo ya aina mbalimbali humo. Neno la Kigiriki lililotumiwa hapa linapatikana katika andiko la Yoh 8:20, ambapo limetafsiriwa “chumba cha hazina.” Inaonekana maneno hayo yanarejelea sehemu fulani iliyo katika Ua wa Wanawake. (Habari za utafiti–Mt 27:6 na Nyongeza B11.) Kulingana na marabi fulani, masanduku 13 ya hazina yalikuwepo kuzunguka kuta za ua huo. Inaaminika kwamba hekalu pia lilikuwa na chumba kikubwa cha hazina ambako pesa kutoka kwa masanduku ya hazina zililetwa.

sarafu mbili ndogo: Tnn., “leptoni mbili,” wingi wa neno la Kigiriki le·ptonʹ, linamaanisha kitu kidogo na chembamba. Leptoni ilikuwa sarafu yenye thamani iliyolingana na 1/128 ya dinari na ilikuwa sarafu ya shaba au shaba nyekundu na inaonekana ilikuwa sarafu ndogo zaidi iliyotumiwa nchini Israeli.—Tazama Kamusi, “Leptoni,” na Nyongeza B14.

zenye thamani ndogo sana: Tnn., “ambazo ni kwadrani moja.” Neno la Kigiriki ko·dranʹtes (linatokana na neno la Kilatini quadrans) linarejelea sarafu ya Kiroma shaba au shaba nyekundu iliyokuwa na thamani ya 1/64 ya dinari. Hapa Marko anatumia pesa za Waroma kueleza thamani ya sarafu zilizotumiwa kwa ukawaida na Wayahudi.—Tazama Nyongeza B14.

w87 12/1 30 ¶1

Je! Upaji Wako Ni Dhabihu?

Kuna masomo mengi yenye thamani kubwa ambayo sisi tunaweza kujifunza kutokana na usimulizi huo. Labda lile lililo la kutokeza zaidi, ni kwamba, ingawa sisi sote tuna lile pendeleo la kutoa tegemezo kwenye ibada ya kweli kwa mali zetu za kimwili, jambo lililo la thamani kweli kweli machoni pa Mungu, si kutoa kwetu kile ambacho sisi tunaweza kuondolea mbali na bado tusipate hasara sana, bali ni kutoa kile ambacho ni cha thamani kubwa kwetu sisi. Kwa maneno mengine, je! sisi tunatoa kitu fulani ambacho hatutakikosa kweli kweli? Au utoaji wetu ni dhabihu kweli kweli?

Kutafuta Hazina za Kiroho

nwtsty habari za utafiti–Mk 11:17

nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote: Kati ya waandikaji watatu wa Injili walionukuu Isa 56:7, ni Marko tu anayetaja maneno “kwa ajili ya [watu wa] mataifa yote.” (Mt 21:13; Lu 19:46) Hekalu la Yerusalemu lilikusudiwa kuwa mahali ambapo Waisraeli na wageni waliomwogopa Mungu wangeweza kuabudu na kusali kwa Yehova. (1Fa 8:41-43) Ilifaa kwamba Yesu aliwashutumu Wayahudi waliolitumia hekalu kwa biashara na hivyo kulifanya pango la wanyang’anyi. Matendo yao yaliwavunja moyo watu wa mataifa yote wasimkaribie Yehova katika nyumba yake ya sala na hivyo kuwanyima fursa ya kumjua.

MEI 28–JUNI 3

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MARKO 11-12

“Epuka Mtego wa Kuwaogopa Wanadamu”

it-2 619 ¶6

Petro

Akisaidiwa na mwanafunzi mwingine, ambaye ni wazi alimfuata au kuandamana naye kwenda kwenye makao ya kuhani mkuu, Petro aliingia ndani kabisa ya ua. (Yoh 18:15, 16) Hakusimama kimya kwenye kona fulani lenye giza bali alienda ndani na kusimama kando ya moto ili ajipashe joto. Mwangaza wa moto uliwawezesha watu kutambua kwamba alikuwa mwandamani wa Yesu, na lafudhi yake ya Kigalilaya iliwafanya wamshuku zaidi. Akiwa ameshtakiwa, Petro alikana mara tatu kwamba hakumjua Yesu, mwishowe hata akaapa kwa nguvu. Mahali fulani jijini jogoo akawika kwa mara ya pili, na Yesu “akageuka, akamtazama Petro moja kwa moja.” Petro akatoka nje, akaanza kulia, akalia kwa uchungu. (Mt 26:69-75; Mk 14:66-72; Lu 22:54-62; Yoh 18:17, 18; ona JOGOO KUWIKA; KIAPO.) Hata hivyo, dua ambayo Yesu alimtolea Petro mapema ilijibiwa, na imani ya Petro haikudhoofika kabisa.—Lu 22:31, 32.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki