MAISHA YA MKRISTO
Jinsi Wenzi wa Ndoa Wanavyoweza Kuimarisha Ndoa Yao
Abrahamu na Sara ni mfano mzuri wa wenzi wa ndoa waliopendana na kuheshimiana. (Mwa 12:11-13; 1Pe 3:6) Ingawa hivyo, ndoa yao haikuwa kamilifu, na walivumilia changamoto mbalimbali maishani. Wenzi wa ndoa wanaweza kujifunza nini kwa kuchunguza mfano wa Abrahamu na Sara?
Muwe na mawasiliano mazuri kati yenu. Mjibu mwenzi wako kwa upole anapozungumza bila kufikiri au akiwa ameudhika. (Mwa 16:5, 6) Pangeni muda wa kuwa pamoja. Kupitia maneno na matendo yako, mhakikishie mwenzi wako kwamba unampenda. Zaidi ya yote, hakikisheni kwamba mnamhusisha Yehova kwa kujifunza, kusali, na kuabudu pamoja. (Mhu 4:12) Ndoa imara humletea Yehova sifa, ambaye ndiye Mwanzilishi wa mpango huu mtakatifu.
TAZAMA VIDEO YENYE KICHWA JINSI YA KUIMARISHA KIFUNGO CHA NDOA, KISHA UJIBU MASWALI YAFUATAYO:
Katika video hiyo, ni dalili gani zilizoonyesha kwamba Shaan na Kiara hawakuwa na uhusiano wa karibu?
Kwa nini mawasiliano ya unyoofu na yaliyo wazi ni muhimu katika ndoa?
Mfano wa Abrahamu na Sara uliwasaidiaje Shaan na Kiara?
Shaan na Kiara walichukua hatua zipi ili kuimarisha ndoa yao?
Kwa nini mume na mke hawapaswi kutarajia ndoa yao iwe kamilifu?
Unaweza kuimarisha ndoa yako!