Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr20 Oktoba kur. 1-3
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
  • Vichwa vidogo
  • OKTOBA 12-18
  • OKTOBA 26–NOVEMBA 1
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2020
mwbr20 Oktoba kur. 1-3

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

OKTOBA 12-18

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | KUTOKA 33-34

“Sifa za Yehova Zinazovutia”

it-2 466-467

Jina

Uumbaji unatoa ushahidi wa kutosha kwamba kuna Mungu lakini hautaji jina la Mungu. (Zb 19:1; Ro 1:20) Ili mtu aseme kwamba anamjua Mungu mengi yanahusika zaidi ya kulifahamu jina lake tu. (2Nya 6:33) Kunahusisha kumjua Yeye—makusudi yake, matendo yake, na sifa zake kama zinavyoonyeshwa katika Neno lake. (Linganisha na 1Fa 8:41-43; 9:3, 7; Ne 9:10.) Jambo hilo linaonyeshwa katika kisa cha Musa, mwanamume ambaye Yehova ‘alimjua kwa jina,’ yaani, walikuwa na uhusiano wa karibu sana. (Kut 33:12) Musa alipata pendeleo la kuona utukufu wa Yehova na ‘kusikia jina la Yehova likitangazwa.’ (Kut 34:5) Kutangazwa huko hakukuwa tu kurudiwa tena kwa jina la Yehova bali wonyesho wa sifa na matendo ya Mungu. “Yehova, Yehova, ni Mungu mwenye rehema na huruma, si mwepesi wa hasira, nina upendo mwingi mshikamanifu na kweli, ninawatendea maelfu kwa upendo mshikamanifu, ninasamehe makosa na uovu na dhambi, lakini sikosi kamwe kuwaadhibu wenye hatia, ninawaadhibu wana na wajukuu kufikia kizazi cha tatu na cha nne kwa sababu ya makosa ya baba zao.” (Kut 34:6, 7) Kwa kuongezea, wimbo wa Musa wenye maneno, “kwa maana nitalitangaza jina la Yehova,” unasimulia jinsi Mungu alivyoshughulika na Waisraeli na unaonyesha utu wake.—Kum 32:3-44.

OKTOBA 26–NOVEMBA 1

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | KUTOKA 37-38

“Madhabahu Katika Hema la Ibada na Fungu Lake Katika Ibada ya Kweli”

it-1 82 ¶3

Madhabahu

Madhabahu ya uvumba. Madhabahu ya uvumba (inayoitwa pia “madhabahu ya dhahabu” [Kut 39:38]) ilitengenezwa kwa kutumia mbao za mshita, na sehemu yake ya juu ilifunikwa na dhahabu. Juu yake kulikuwa na ukingo wa dhahabu. Madhabahu hiyo ilikuwa ya mraba wenye urefu wa sentimita 44.5 na kimo cha sentimita 89, pia ilikuwa na “pembe” zilizojitokeza katika pande zake nne. Pete mbili za dhahabu zilitengenezwa ili kushikilia fito za mshita za dhahabu zilizotumiwa kubebea madhabahu, na pete hizo za dhahabu ziliwekwa chini ya ukingo wa dhahabu kwenye pande mbili zinazoelekeana za madhabahu. (Kut 30:1-5; 37:25-28) Mara mbili kila siku, asubuhi na jioni, uvumba maalumu ulifukizwa katika madhabahu hiyo. (Kut 30:7-9, 34-38) Katika sehemu nyingine, chetezo kinatajwa kutumiwa katika kufukiza uvumba huenda kwenye madhabahu ya uvumba. (Law 16:12, 13; Ebr 9:4; Ufu 8:5; linganisha na 2Nya 26:16, 19.) Madhabahu ya kufukiza uvumba ilikuwa ndani ya hema la ibada mbele ya pazia la Patakatifu Zaidi hivi kwamba ilisemwa kuwa “mbele ya kifuniko kilicho juu ya sanduku la Ushahidi.”—Kut 30:1, 6; 40:5, 26, 27.

it-1 1195

Uvumba

Uvumba mtakatifu uliotumiwa katika hema la ibada nyikani ulitengenezwa kutokana na vitu vyenye gharama kubwa vilivyochangiwa na taifa. (Kut 25:1, 2, 6; 35:4, 5, 8, 27-29) Alipotoa maagizo ya jinsi ya kutayarisha manukato hayo yaliyochanganywa kwa kutumia viungo vinne, Yehova alimwambia Musa hivi: “Chukua vipimo vinavyolingana vya manukato haya: matone ya natafi, shekelethi, kelbena yenye manukato, na ubani safi. Yatumie kutengeneza uvumba; viungo hivyo vinapaswa kuchanganywa kwa ustadi, vitiwe chumvi, viwe safi, na vitakatifu. Utaponda baadhi ya viungo hivyo viwe unga laini na kuweka kiasi fulani mbele ya sanduku la Ushahidi katika hema la mkutano, mahali nitakapokutokea. Mchanganyiko huo unapaswa kuwa mtakatifu kabisa kwenu.” Kisha, ili kuwakumbusha jinsi uvumba huo ulivyokuwa wa pekee na mtakatifu, Yehova aliongeza kwa kusema: “Yeyote atakayetengeneza uvumba kama huo ili afurahie harufu yake ni lazima auawe.”—Kut 30:34-38; 37:29.

it-1 82 ¶1

Madhabahu

Madhabahu za hema la mkutano. Hema la ibada liliposimamishwa, madhabahu mbili zilijengwa kulingana na maagizo ya Mungu. Madhabahu ya dhabihu za kuteketezwa (huitwa pia “madhabahu ya shaba” [Kut 39:39]) ilitengenezwa kwa mbao za mshita na ilikuwa na umbo la sanduku lenye uwazi, yaani, bila sehemu ya juu au chini. Ilikuwa na urefu na upana wa mita 2.2 (futi 7.3) za mraba na kimo cha mita 1.3 (futi 4.4) na ilikuwa na “pembe” zilizojitokeza kwenye ncha zake nne za juu. Madhabahu hiyo ilifunikwa kwa shaba. Wavu wa shaba uliwekwa “chini ya” ukingo wa madhabahu, na ulishuka ndani ya madhabahu hiyo “kufikia katikati.” Pete nne ziliwekwa kwenye pembe nne za wavu huo, na huenda pete hizo ndizo zilizotumiwa kupitishia fito mbili za mshita zilizofunikwa kwa shaba ambazo zilitumiwa kubeba madhabahu hiyo. Huenda hilo linamaanisha kwamba tundu lilitobolewa pande mbili za madhabahu ili kuwezesha wavu kuingizwa, huku pete hizo zikitokeza pande zote mbili. Wasomi wana maoni mengi tofauti kuhusu jambo hilo, na wengi wanasema kwamba huenda kulikuwa na pete za aina mbili. Aina ya pili ya pete hizo ziliunganishwa kwa nje na ndizo zilizoingiziwa fito za kubebea madhabahu hiyo. Vyombo vya shaba vilivyotengenezwa vilitia ndani ndoo na sepetu za kuondolea majivu, mabakuli yaliyotumiwa kukusanya damu za wanyama, nyuma za kushikia nyama, na vyetezo.—Kut 27:1-8; 38:1-7, 30; Hes 4:14.

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 36

Mshita

Mshita una miiba mingi mirefu inayojitokeza katika matawi yake mapana. Matawi hayo mara nyingi huingiliana na ile ya mishita ya karibu na kufanyiza vichaka vilivyosongamana; jambo hilo linafafanua vizuri kwa nini wingi wa neno shit·timʹ ndilo hutumiwa mara nyingi katika masimulizi ya Biblia. Mshita hukua na kufikia urefu wa mita 6 hadi mita 8 (futi 20 hadi 26), lakini mara nyingi huonekana kama pori. Una majani laini, nao hufunikwa na maua ya manjano yenye harufu nzuri yaliyo na matunda. Mti huo umefunikwa na gome lenye rangi nyeusi, na mbao ngumu ambayo haiwezi kuathiriwa inaposhambuliwa na wadudu. Sifa hizo na upatikanaji wake katika maeneo ya jangwani, zilifanya mshita uwe wenye kufaa sana kujengea hema la ibada na vifaa vyake. Mshita ulitumiwa kujenga sanduku la agano (Kut 25:10; 37:1), meza ya mikate ya wonyesho (Kut 25:23; 37:10), madhabahu (Kut 27:1; 37:25; 38:1), fito za kubebea vyombo hivyo (Kut 25:13, 28; 27:6; 30:5; 37:4, 15, 28; 38:6), nguzo za pazia (Kut 26:32, 37; 36:36), na viunzi vyake (Kut 26:15; 36:20) pamoja na fito zinazounganisha viunzi (Kut 26:26; 36:31).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki