Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb22 Machi uku. 9
  • Ni Nani Marafiki Wako Mtandaoni?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nani Marafiki Wako Mtandaoni?
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Ubaya Kufanya Urafiki Kupitia Intaneti?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Epuka Mitego ya Mitandao ya Kijamii
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Vituo vya Mawasiliano?—Sehemu ya 2
    Amkeni!—2011
  • Watoto na Intaneti—Mambo Ambayo Wazazi Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—2008
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
mwb22 Machi uku. 9

MAISHA YA MKRISTO

Ni Nani Marafiki Wako Mtandaoni?

Rafiki anafafanuliwa kuwa “mtu anayeshikamana na mwingine kwa sababu ya upendo au heshima.” Kwa mfano, Yonathani na Daudi walianzisha urafiki usiovunjika baada ya Daudi kumuua Goliathi. (1Sa 18:1) Kila mmoja wao alionyesha sifa zilizomvutia mwenzake. Hivyo, urafiki wenye nguvu unategemea ujuzi sahihi. Kwa kawaida kumfahamu mtu mwingine huchukua muda na jitihada. Hata hivyo, kwenye mitandao ya kijamii, watu wanaweza kuwa “marafiki” kwa kubofya kitufe tu. Kwa sababu watu mtandaoni wanaweza kupanga kihususa kabisa watasema nini na kudhibiti wengine wanawaonaje, ni rahisi kuficha jinsi walivyo hasa. Hivyo, ni vizuri kuwa mteuzi unachagua watu wa aina gani kuwa marafiki wako. Usiogope kupuuza au kukataa maombi ya watu fulani ya kuwa marafiki ikiwa huwafahamu vizuri eti tu kwa sababu unaogopa utaumiza hisia zao. Kwa sababu ya hatari zinazoweza kutokea, baadhi ya watu wamechagua kutotumia mitandao ya kijamii kabisa. Hata hivyo, ukichagua kutumia mtandao wa kijamii, unapaswa kuzingatia nini?

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA HEKIMA, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Picha kutoka kwenye video “Tumia Mitandao ya Kijamii kwa Hekima.” Msichana akitazama picha yake kwenye TV akiwa ameshtuka.

    Unapaswa kufikiria nini kabla ya kuandika maelezo au kupachika picha?

  • Picha kutoka kwenye video “Tumia Mitandao ya Kijamii kwa Hekima.” Mizani ikiwa na picha yenye kuvutia ya msichana upande mmoja na sarafu upande mwingine. Picha ina uzito mkubwa zaidi kuliko sarafu hizo.

    Kwa nini unapaswa kuchagua marafiki wako wa mtandaoni kwa uangalifu?

  • Picha kutoka kwenye video “Tumia Mitandao ya Kijamii kwa Hekima.” Wanaume wawili wanaoonekana wajeuri wakimwonyesha mvulana kitu kwenye mtandao wa kijamii huku mvulana huyo akifunika macho yake.

    Kwa nini unapaswa kuweka mipaka ya muda unaotumia kwenye mtandao wa kijamii?​—Efe 5:15, 16

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki