Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb18 Juni uku. 7
  • Epuka Mitego ya Mitandao ya Kijamii

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Epuka Mitego ya Mitandao ya Kijamii
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nani Marafiki Wako Mtandaoni?
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
  • Kwa Nini Vinavutia?
    Amkeni!—2012
  • Maswali Manne Unayopaswa Kujiuliza Kuhusu Vituo vya Mawasiliano
    Amkeni!—2012
  • Mitandao ya Kijamii Inaniathirije?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
mwb18 Juni uku. 7

MAISHA YA MKRISTO

Epuka Mitego ya Mitandao ya Kijamii

Yesu akikataa kugeuza mawe kuwa mkate

KWA NINI NI MUHIMU?: Kama tu vifaa vingi, mitandao ya kijamii inaweza kuwa na faida na madhara. Baadhi ya Wakristo wamechagua kutotumia mitandao ya kijamii. Wakristo wengine hutumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na watu wa familia na marafiki. Hata hivyo, Ibilisi anataka tutumie mitandao ya kijamii kwa njia isiyo na hekima, na hilo litaharibu sifa yetu na hali yetu ya kiroho. Kama Yesu, tunaweza kutumia kanuni za Neno la Mungu ili kutambua na kuepuka hatari.—Lu 4:4, 8, 12.

MITEGO YA KUEPUKA:

  • Kutumia mitandao ya kijamii kupita kiasi. Kutumia mitandao ya kijamii kwa saa nyingi kunaweza kutunyima wakati wenye thamani tunaohitaji ili kufanya mambo ya kiroho

    Kanuni za Biblia: Efe 5:15, 16; Flp 1:10

  • Kutazama mambo yasiyofaa. Kutazama picha zisizofaa kunaweza kutufanya tuwe waraibu wa ponografia au kujihusisha katika maadili mapotovu. Kusoma habari za waasi-imani kunaweza kuharibu imani ya mtu

    Kanuni za Biblia: Mt 5:28; Flp 4:8

  • Kuweka picha au maelezo yasiyofaa. Kwa kuwa moyo ni wenye hila, huenda mtu akawa na mwelekeo wa kuweka picha au maelezo yasiyofaa kwenye mtandao wa kijamii. Hata hivyo, hilo linaweza kuharibu sifa ya mtu au kudhoofisha imani yake

    Kanuni za Biblia: Ro 14:13; Efe 4:29

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA HEKIMA, KISHA ZUNGUMZIENI JINSI YA KUEPUKA HALI ZIFUATAZO:

Mwizi akitumia mtandao wa kijamii kujua wakati mwenye nyumba ameenda likizo
Mwajiri akitazama picha isiyofaa kwenye mtandao wa kijamii
Kusoma matusi kwenye mtandao wa kijami
Kwa sababu ya kutumia mtandao wa kijamii hadi usiku sana anashindwa kuamka asubuhi
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki