Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb24 Machi kur. 10-11
  • Aprili 8-14

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aprili 8-14
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2024
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2024
mwb24 Machi kur. 10-11

APRILI 8-14

ZABURI 26-28

Wimbo 34 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

Mfalme Daudi akisali kwa bidii.

1. Mambo Ambayo Daudi Alifanya Ili Kuimarisha Azimio Lake la Kuwa Mtimilifu

(Dak. 10)

Daudi alimwomba Yehova amsaidie kuwa mtu mzuri zaidi (Zb 26:​1, 2; w04 12/1 14 ¶8-9)

Daudi aliepuka kushirikiana na watu wabaya (Zb 26:​4, 5; w04 12/1 15 ¶12-13)

Daudi alipenda kumwabudu Yehova (Zb 26:8; w04 12/1 16 ¶17-18)



Ingawa Daudi alifanya makosa fulani, bado alitembea kwa “utimilifu wa moyo.” (1Fa 9:4) Utimilifu wa Daudi ulionekana kutokana na jinsi alivyomtumikia na kumpenda Yehova kwa moyo wake wote.

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Zb 27:10—Mstari huu unatufariji jinsi gani ikiwa tunahisi tumeachwa na marafiki wa karibu? (w06 7/15 28 ¶15)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Zb 27:​1-14 (th somo la 2)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 2) NYUMBA KWA NYUMBA. Tumia mojawapo ya trakti kwenye Sanduku la Vifaa vya Kufundishia. (th somo la 3)

5. Kufuatia Upendezi

(Dak. 4) NYUMBA KWA NYUMBA. Zungumzia swali kwenye ukurasa wa mwisho wa trakti ambayo ulimwachia. Mwonyeshe tovuti ya jw.org na habari fulani inayopatikana humo. (lmd somo la 9 jambo kuu la 3)

6. Hotuba

(Dak. 5) lmd nyongeza A jambo kuu la 3—Kichwa: Mazingira Yatakuwa Bora na Dunia Itakuwa Paradiso. (th somo la 13)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 128

7. Vijana Wanaodumisha Utimilifu Katika Maadili

(Dak. 15) Mazungumzo.

Mvulana tineja akitafakari andiko ambalo ametoka kusoma. Kando yake kuna tablet inayoonyesha sehemu ya video “Maisha Yangu ya Utineja​—⁠Ninawezaje Kupinga Kishawishi cha Kufanya Ngono Kabla ya Ndoa? ” Sehemu hiyo inamwonyesha Yosefu akimkimbia mke wa Potifa.

Vijana Wakristo wanahitaji kupambana ili kuepuka ukosefu wa maadili. Pambano hilo ni kali kwa sababu wao si wakamilifu. Isitoshe, wako katika upeo wa ujana—kipindi ambacho tamaa ya kufanya ngono ni yenye nguvu sana hivi kwamba inafanya iwe vigumu kwa vijana kufanya maamuzi mazuri. (Ro 7:21; 1Ko 7:36) Pia, kila wakati wengine huwashinikiza wafanye ngono, iwe ni na watu wa jinsia tofauti au na watu wa jinsia yao. (Efe 2:2) Tunajivunia sana vijana ambao wanaendelea kudumisha utimilifu wao.

Onyesha VIDEO Maisha Yangu ya Utineja—Ninawezaje Kupinga Kishawishi cha Kufanya Ngono Kabla ya Ndoa? Kisha waulize wasikilizaji:

  • Cory na Kamryn walishinikizwa jinsi gani?

  • Ni nini kilichowasaidia kudumisha utimilifu wao?

  • Ni kanuni gani za Biblia zinazoweza kukusaidia kukabiliana na hali kama hiyo?

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) bt sura ya 8 ¶5-12

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 38 na Sala

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki