Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb25 Januari kur. 6-7
  • Januari 27–Februari 2

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Januari 27–Februari 2
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
mwb25 Januari kur. 6-7

JANUARI 27–FEBRUARI 2

ZABURI 140-143

Wimbo 44 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

1. Tenda Kupatana na Sala Yako ya Kuomba Msaada

(Dak. 10)

Uwe tayari kukubali mashauri (Zb 141:5; w22.02 12 ¶13-14)

Tafakari matendo ya Yehova ya wokovu (Zb 143:5; w10 3/15 32 ¶4)

Jitahidi kuona mambo kama Yehova anavyoyaona (Zb 143:10; w15 3/15 32 ¶2)

Ndugu kijana akifanya funzo la kibinafsi. Picha: 1. Anasali akiwa ameketi nje. 2. Anasikiliza mashauri ya ndugu mwenye umri mkubwa wanapokuwa katika huduma.

Zaburi 140-143 zinatia ndani mengi zaidi ya sala za Daudi za kuomba msaada. Zinaonyesha pia kwamba alitenda kupatana na sala zake.

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Zb 140:3—Kwa nini Daudi analinganisha ulimi wa waovu na wa nyoka? (it-2 1151)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Zb 141:​1-10 (th somo la 12)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 4) MAHUBIRI YASIYO RASMI. Anzisha mazungumzo baada ya kumsaidia mtu kwa njia hususa. (lmd somo la 3 jambo kuu la 5)

5. Kufuatia Upendezi

(Dak. 3) MAHUBIRI YA UMMA. Mtu huyo anakuambia kwamba ana shughuli. (lmd somo la 7 jambo kuu la 3)

6. Kufafanua Imani Yako

(Dak. 5) Onyesho. ijwfq makala ya 21—Kichwa: Kwa Nini Mashahidi wa Yehova Wanakataa Kutiwa Damu Mishipani? (th somo la 7)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 141

7. Jitayarishe Kushughulikia Hali za Kiafya Zinazohitaji Matibabu au Upasuaji

(Dak. 15) Mazungumzo.

Yehova anaahidi kuwa “msaada unaopatikana kwa urahisi nyakati za taabu.” (Zb 46:1) Mtu anapohitaji kupata matibabu au kufanyiwa upasuaji anaweza kuwa na hofu. Hata hivyo, Yehova ametuandalia kila kitu tunachohitaji ili tujitayarishe kwa ajili ya hali hizo. Kwa mfano, tengenezo lake limeandaa kadi ya mamlaka ya kudumu ya uwakilishi wa kitiba (DPA), Kadi ya Utambulisho,a majarida mengine yenye habari za kitibab kutia ndani Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali (HLC). Maandalizi hayo hutusaidia kutii amri ya Mungu kuhusu damu.—Mdo 15:​28, 29.

Dada akijaza kadi ya mamlaka ya kudumu ya uwakilishi wa kitiba.

Onyesha VIDEO Je, Umejitayarisha Kukabiliana na Masuala ya Kitiba? Kisha waulize wasikilizaji:

  • Baadhi ya watu wamenufaikaje kwa kujaza mapema kadi ya DPA?

  • Baadhi ya watu wamenufaikaje kutokana na fomu ya Habari kwa Akina Mama Wajawazito (S-401)?

  • Kwa nini inafaa kuwasiliana na HLC haraka iwezekanavyo hali inapotokea ambayo itakulazimu kulazwa, kufanyiwa upasuaji, au kupata matibabu fulani ya pekee kama vile ya kansa, hata ikiwa inaonekana kwamba suala la damu halitahusika?

JE UMEJITAYARISHA?

  • Andika maamuzi yako kwenye kadi yako ya DPA

  • Wasiliana na HLC haraka iwezekanavyo

  • Uwe tayari kumweleza daktari kuhusu msimamo wako wa kukataa kutiwa damu, kuhusu matumizi ya visehemu vya damu, na kuhusu mbinu zinazohusisha matumizi ya damu yako mwenyewe.—Ona lff somo la 39

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) bt sura ya 21 ¶14-22

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 103 na Sala

a Wahubiri waliobatizwa wanaweza kuchukua kadi ya DPA kutoka kwa mtumishi wa machapisho na Kadi ya Utambulisho kwa ajili ya watoto wao wadogo.

b Unaweza kupata fomu ya Habari kwa Akina Mama Wajawazito (S-401), Habari kwa Ajili ya Wagonjwa Wanaohitaji Upasuaji au Matibabu ya Mionzi (S-407), na Jinsi Wazazi Wanavyoweza Kuwalinda Watoto Wao Kutokana na Matumizi Mabaya ya Damu (S-55) kutoka kwa wazee unapoihitaji.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki