Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb25 Machi kur. 4-5
  • Machi 17-23

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Machi 17-23
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
mwb25 Machi kur. 4-5

MACHI 17-23

METHALI 5

Wimbo 122 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

1. Kaa Mbali na Uasherati

(Dak. 10)

Ni rahisi sana kushawishiwa kufanya uasherati (Met 5:3; w00 7/15 29 ¶1)

Uasherati huleta maumivu makali (Met 5:​4, 5; w00 7/15 29 ¶2)

Kaa mbali na uasherati (Met 5:8; w00 7/15 29 ¶5)

Dada Mkristo akikataa kumpa mvulana namba yake ya simu

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Met 5:9—Ni katika njia gani kufanya uasherati ni ‘kuwapa wengine heshima yetu’? (w00 7/15 29 ¶7)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Met 5:​1-23 (th somo la 5)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 3) MAHUBIRI YA UMMA. Mwalike kwenye Ukumbusho mtu ambaye si Mkristo, kisha utumie jw.org kutafuta mahali ambapo tukio hilo litafanyiwa karibu naye. (lmd somo la 6 jambo kuu la 4)

5. Kufuatia Upendezi

(Dak. 4) NYUMBA KWA NYUMBA. Katika ziara iliyotangulia mwenye nyumba alikubali mwaliko wa Ukumbusho na akaonyesha upendezi. (lmd somo la 9 jambo kuu la 5)

6. Kufanya Wanafunzi

(Dak. 5) lff somo la 16 muhtasari, ungejibuje, na lengo. Mwanafunzi anapouliza ikiwa Yesu alikuwa ameoa, mwonyeshe jinsi ya kufanya utafiti ili kupata jibu. (lmd somo la 11 jambo kuu la 4)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 121

7. Unachoweza Kufanya Ili Kuendelea Kuwa Safi Unapokuwa na Urafiki wa Kimapenzi

(Dak. 15) Mazungumzo.

Urafiki wa kimapenzi unaweza kufafanuliwa kuwa “uhusiano kati ya watu wawili wanaoelekezeana upendezi wa kimahaba.” Uhusiano huo unaweza kuendelezwa katika kikundi au faraghani. Unaweza kuwa wa uso kwa uso, kwenye simu, au hata kupitia ujumbe mfupi. Urafiki wa kimapenzi si njia ya kujifurahisha, bali ni aina ya uchumba. Ni hatua muhimu inayoongoza kwenye ndoa. Ni tahadhari zipi zinazoweza kuwasaidia watu, iwe ni vijana au wazee, kuepuka kujihusisha katika uasherati wanapoendelea na urafiki wao?—Met 22:3.

Mwanamume na mwanamke wenye umri mkubwa walio na urafiki wa kimapenzi wakifurahia mazungumzo huku wakila chakula pamoja kwenye mkahawa.

Onyesha VIDEO Kujitayarisha kwa Ajili ya Ndoa—Sehemu ya 1: Je, Niko Tayari Kuanzisha Urafiki wa Kimapenzi?—Kisehemu. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Kwa nini mtu hapaswi kuanzisha urafiki wa kimapenzi hadi anapokuwa tayari kufunga ndoa? (Met 13:12; Lu 14:​28-30)

  • Ni nini kilichokupendeza kutokana na jinsi wazazi hao walivyomsaidia binti yao?

Soma Methali 28:26. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Ni mipango gani ambayo watu wanaochumbiana wanaweza kufanya mapema ili waepuke kuwa peke yao katika mazingira yenye kushawishi?

  • Kwa nini ni jambo la hekima kwa watu wanaochumbiana kuzungumza mapema kuhusu mipaka wanayopaswa kujiwekea ya kuonyeshana mahaba, kama vile kushikana mikono na kubusiana?

Soma Waefeso 5:​3, 4. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Watu wanaochumbiana wanapaswa kuzingatia nini kuhusu mazungumzo yao kwenye simu au mtandaoni?

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) bt sura ya 24 ¶1-6

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 3 na Sala

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki