Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb25 Machi kur. 14-15
  • Aprili 28–Mei 4

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aprili 28–Mei 4
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
mwb25 Machi kur. 14-15

APRILI 28–MEI 4

METHALI 11

Wimbo 90 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

1. Usiseme!

(Dak. 10)

Usiseme jambo lolote linaloweza kumuumiza ‘jirani yako’ (Met 11:9; w02 5/15 26 ¶4)

Usiseme jambo linaloleta mgawanyiko (Met 11:11; w02 5/15 27 ¶2-3)

Usiseme jambo la siri la mwenzako (Met 11:​12, 13; w02 5/15 27 ¶5)

Ndugu wawili wakiwa na mazungumzo katika Jumba la Ufalme. Mmoja wao anamwongelea vibaya ndugu mwingine anayekuja kuzungumza nao.

JAMBO LA KUTAFAKARI: Maneno ya Yesu kwenye Luka 6:45 yanaweza kutusaidiaje tuepuke kusema mambo yenye kudhuru?

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Met 11:17—Kuonyesha fadhili kunatunufaishaje? (g20.1 11, sanduku)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Met 11:​1-20 (th somo la 5)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 4) MAHUBIRI YASIYO RASMI. Tafuta nafasi ya kumweleza mtu huyo jambo ambalo ulijifunza kwenye mkutano hivi karibuni. (lmd somo la 2 jambo kuu la 4)

5. Kufuatia Upendezi

(Dak. 4) MAHUBIRI YASIYO RASMI. Tumia video kutoka kwenye Sanduku la Vifaa vya Kufundishia. (lmd somo la 8 jambo kuu la 3)

6. Kufanya Wanafunzi

(Dak. 4) MAHUBIRI YA UMMA. Mwalike ajifunze Biblia na umwonyeshe jinsi linavyoongozwa. (lmd somo la 10 jambo kuu la 3)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 157

7. Usiache Ulimi Wako Uharibu Amani

(Dak. 15) Mazungumzo.

Kwa kuwa sisi si wakamilifu, tunaweza kujikwaa katika maneno yetu. (Yak 3:8) Hata hivyo, tukifikiria madhara yanayoweza kutokea, tutaepuka kusema mambo ambayo tutajutia baadaye. Ulimi wetu unaweza kuharibu amani ya kutaniko katika njia zifuatazo:

  • Kujisifu isivyofaa. Haya ni mazungumzo ya kujisifu na yanaweza kuchochea mashindano na wivu.—Met 27:2

  • Udanganyifu. Mbali na kusema uwongo moja kwa moja, mazungumzo haya yanatia ndani kuwapotosha watu kimakusudi. Hata udanganyifu mdogo unaweza kumfanya mtu asitumainiwe na kuharibu sifa yetu.—Mhu 10:1

  • Porojo Zenye Kuumiza. Haya ni mazungumzo ya ovyoovyo kuhusu watu na maisha yao. Mazungumzo hayo hupotosha ukweli au kufunua mambo ya siri. (1Ti 5:13) Yanaweza kutokeza ugomvi na migawanyiko

  • Maneno Yanayosemwa kwa Hasira. Haya ni maneno yanayosemwa kwa ukali na bila kujizuia dhidi ya mtu aliyetukasirisha. (Efe 4:26) Yanaweza kuwaumiza wengine.—Met 29:22

Picha kutoka kwenye video yenye kichwa “ ‘Vua’ Mazoea Yanayoharibu Amani​—⁠Kisehemu.” 1. Emily na Cecilia wakiwa ndani ya mkahawa wakiwa wametazamana. Cecilia anaangalia habari zilizowekwa mtandaoni na Hellen. 2. Hellen akizungumza kwa ukali na Cecilia kwenye sehemu ya maegesho ya magari ya Jumba la Ufalme.

Onyesha VIDEO ‘Vua’ Mazoea Yanayoharibu Amani—Kisehemu. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Umejifunza nini kuhusu jinsi mazungumzo yetu yanavyoweza kuharibu amani ya kutaniko?

Ili uone jinsi amani ilivyorudishwa, tazama video yenye kichwa “Tafuta Amani na Kuifuatilia.”

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) bt sura ya 25 ¶14-21

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo Mpya wa Kusanyiko la Eneo la 2025 na Sala

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki