Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb25 Mei kur. 4-5
  • Mei 12-18

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mei 12-18
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
mwb25 Mei kur. 4-5

MEI 12-18

METHALI 13

Wimbo 34 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

1. Usipumbazwe na “Taa ya Waovu”

(Dak. 10)

Watu waovu hawana tumaini la wakati ujao (Met 13:9; it-2 196 ¶2-3)

Usishirikiane na wale wanaofanya mambo mabaya yaonekane kuwa mazuri (Met 13:20; w12 7/15 12 ¶3)

Yehova huwabariki waadilifu (Met 13:25; w04 7/15 31 ¶6)

Mkusanyo wa picha: Kulinganisha maamuzi mabaya yanayofanywa na mwanamume ambaye si Shahidi na maamuzi mazuri yanayofanywa na baadhi ya Mashahidi. 1. Mwanamume akicheza dansi usiku katika ukumbi wa starehe huku akiwa ameshika kinywaji mkononi. 2. Baadaye, anaumwa na anaanza kunywa dawa. 3. Ndugu na dada wakiwa kwenye tafrija wakati wa jioni. Wanafurahia kuimba, kucheza muziki, na kula pamoja. 4. Siku inayofuata, wanashiriki katika huduma ya shambani.

Mara nyingi, maisha ya wale wanaofuatia tamaa za ulimwengu huu huwa kinyume na matarajio yao. Lakini wale wanaofanya mapenzi ya Yehova wanafurahia maisha yanayoridhisha kikweli

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Met 13:24—Watu wana maoni gani yasiyofaa kuhusu upendo na nidhamu? (it-2 276 ¶2)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Met 13:​1-17 (th somo la 10)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 3) NYUMBA KWA NYUMBA. Baada ya kuzungumza kuhusu tukio fulani la karibuni, mwonyeshe mwenye nyumba jambo litakalomvutia kutoka katika Biblia. (lmd somo la 2 jambo kuu la 5)

5. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 4) MAHUBIRI YASIYO RASMI. Mwalike mtu huyo ahudhurie mikutano. (lmd somo la 2 jambo kuu la 3)

6. Hotuba

(Dak. 5) lmd nyongeza A jambo kuu la 9—Kichwa: Watoto Wanaowaheshimu na Kuwatii Wazazi Wao Watafanikiwa. (th somo la 16)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 77

7. “Nuru ya Waadilifu Hung’aa kwa Uangavu”

(Dak. 8) Mazungumzo.

Tunapata ujuzi na hekima nyingi kutoka katika Neno la Mungu. Tunapotumia maishani mwetu mambo tuliyojifunza, tunapata mafanikio na furaha ya kudumu. Hilo ni jambo ambalo ulimwengu huu hauwezi kutupatia.

Picha kutoka kwenye video yenye kichwa “Ulimwengu Hauwezi Kukupa Kitu Ambacho Hauna.” Dada Gainanshina akiwa ameketi kwenye bustani huku akitazama angani.

Onyesha VIDEO Ulimwengu Hauwezi Kukupa Kitu Ambacho Hauna. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Hali ambayo Dada Gainanshina alikabili inaonyeshaje ubora wa “nuru ya waadilifu” inapolinganishwa na “taa ya waovu”?—Met 13:9

Usipoteze muda wako kamwe ukiwazia kuhusu mambo ya ulimwengu huu, au kujutia maamuzi uliyofanya yanayokuruhusu umtumikie Yehova. (1Yo 2:​15-17) Badala yake, kazia fikira ‘thamani bora zaidi ya ujuzi’ ambao umepata.—Flp 3:8.

PENDEKEZO KWA AJILI YA IBADA YA FAMILIA:

Tazama kwa ukawaida video moja au mbili kutoka katika mfululizo wenye kichwa Kweli Hubadili Maisha. Chunguza jinsi video hizo zinavyokazia thamani ya kweli.

8. Mahitaji ya Kutaniko

(Dak. 7)

9. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) bt sura ya 26 ¶9-17

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 43 na Sala

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki