Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb25 Mei kur. 6-7
  • Mei 19-25

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mei 19-25
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2025
mwb25 Mei kur. 6-7

MEI 19-25

METHALI 14

Wimbo 89 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

1. Tafakari kwa Makini Kuhusu Kile Utakachofanya Janga Linapotokea

(Dak. 10)

Uwe mwangalifu usiamini “kila neno” unalosikia (Met 14:15; w23.02 22-23 ¶10-12)

Usitegemee tu hisia zako, au uzoefu wako wa wakati uliopita (Met 14:12)

Usiwasikilize wale wanaokataa mwongozo kutoka kwa tengenezo la Yehova (Met 14:7)

Familia ikitazama programu ya JW Broadcasting.

JAMBO LA KUTAFAKARI: Je, wazee mmejitayarisha kufuata mwongozo na kumtegemea Yehova janga linapotokea?—w24.07 5 ¶11.

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Met 14:17—Ni katika njia zipi “mtu anayechanganua mambo” anaweza kuchukiwa? (it-2 1094)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Met 14:​1-21 (th somo la 11)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 3) MAHUBIRI YA UMMA. Shiriki jambo fulani kutoka kwenye Biblia na mtu anayekueleza kwamba anahangaishwa na hali ya kiuchumi. (lmd somo la 3 jambo kuu la 3)

5. Kufuatia Upendezi

(Dak. 4) NYUMBA KWA NYUMBA. Toa gazeti kuhusu habari ambayo mwenye nyumba alipendezwa nayo mlipozungumza wakati uliopita. (lmd somo la 9 jambo kuu la 4)

6. Kufanya Wanafunzi

(Dak. 5) Mtie moyo mwanafunzi wako asome Biblia kila siku, na umwonyeshe jinsi anavyoweza kufikia lengo lake. (th somo la 19)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 126

7. Jitayarishe kwa Ajili ya Majanga

(Dak. 15) Mazungumzo.

Yaongozwe na mzee. Tia ndani vikumbusho kutoka kwa ofisi ya tawi na kutoka kwa baraza la wazee, ikiwa vipo.

Kadiri tunavyovumilia hali ngumu katika “siku za mwisho,” tunatarajia kwamba matatizo yataongezeka. (2Ti 3:1; nwtsty habari za utafiti Mt 24:8) Janga la asili linapotokea, mara nyingi watu wa Yehova hupokea mwongozo kwa wakati na unaookoa uhai. Hivyo, tunahitaji kutii na kujitayarisha sasa kiroho na kimwili ili tuokoke wakati huo.—Met 14:​6, 8.

  • Jitayarishe Kiroho: Dumisha ratiba nzuri. Jifunze njia mbalimbali za kushiriki katika huduma. Usiwe na hofu hata ikiwa utatenganishwa kwa muda mfupi na wengine kutanikoni. (Met 14:30) Hujatenganishwa na Yehova Mungu na Kristo Yesu.—od 176 ¶15-17

  • Jitayarishe Kimwili: Mbali na mikoba ya dharura, kila familia inapaswa kuwa na chakula cha ziada, maji, dawa, na mahitaji mengine ikiwa itakuwa lazima kukaa ndani kwa muda mrefu.—Met 22:3; g17.5 4

Familia iliyoonyeshwa kwenye picha iliyotangulia, ikiandaa mahitaji kwa ajili ya dharura.

Onyesha VIDEO Je, Umejitayarisha Kukabiliana na Majanga? Kisha waulize wasikilizaji:

  • Yehova anaweza kutusaidiaje wakati wa janga?

  • Tunaweza kuchukua hatua gani hususa ili kujitayarisha?

  • Tunawezaje kuwasaidia wengine ambao wameathiriwa na majanga?

JIULIZE:

‘Ni masomo gani muhimu niliyojifunza kuhusu kujitayarisha kutokana na janga lililotukia hivi karibuni?’

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30) bt sura ya 26 ¶18-22, sanduku uk. 209

Umalizio (Dak. 3) | Wimbo 116 na Sala

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki