Usingizi Mtamu
Hali ya akili ya mtu ni ya maana zaidi kuliko hali ya mwili wake ili kupata usingizi mzuri usiku. Usemi mmoja wasema hivi: “Dhamiri ya mtu wala si godoro lake inahusika sana na usingizi wake.” Mwandikaji wa Mhubiri aliyeongozwa kwa roho alilisema hili: “Ulio mtamu ndio usingizi wa mfanya kazi ngumu awe anakula kidogo au sana; lakini tajiri ana mali nyingi mno naye hawezi kulala.”—Mhu. 5:12, New English Bible.